kiplagati26
JF-Expert Member
- Jul 24, 2012
- 305
- 135
Mfuko wa Akiba kwa watumishi wa serikali ulianzishwa kwa sheria namba 51 (R.E 2002) Baada ya kufanyika kwa melekebisho makubwa ya na kuanzishwa kwa sheria ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii SSRA namba 5 (2012), ndipo mfuko huu wa GEPF ukajipambanua ili kuongeza ushindani wa kibiashara dhidi ya mifuko mingine.
Mfuko huu ulikuwa nyuma sana kiushindani ndipo ukaazisha mchakato wa sheria mpya kutoka mfuko wa Akiba kuwa Mfuko wa Pensheni,mabadiliko hayo ya muundo kutoka akiba kuwa pensheni yatawezesha wanachama kupata mafao ya muda mrefu na muda Mfupi baada ya kutungwa na kupitishwa kwa sheria namba 8 ya mwaka 2013.
Baada ya mabadiliko hayo sheria mfuko huu ulianza kutoza Asilimia tano 5% ya mafao katika mshahara wa mtumishi baada ya Asilimia 10% ya Awali.. mfano ukiwa na mshahara wa TShs 660,000/= Awali alikatwa kiasi cha Tshs 66,000/= na kwa sasa mtumishi mwenye mshahara huo atakatwa Tshs 33,000 wakati huo serikali ikawa inachangia Asilimia 15% ya mshahara wa mtumishi husika. ukiwa na mshahara wa Tshs 580,000/= asilimia 10% yake ni 58,000/= na Asilimia 5% ni Tshs, 29,000/=. Ukiwa na Mshahara wa Tshs 440,000/= asilimia 10% ni Tshs. 44,000/= na Asilimia 5% ni 22,000/=.
Ukiwa na mshahara wa Tshs.380,000 Asilimia 10% ni Tshs. 38,000/= na Asilimia 5% ni Tshs.19,000/=.Hivyo baada ya malekebisho hayo mwaka jana mwezi Januari Hazina ya serikali waliendelea kupeleka fedha za mafao kwa kila mwananchama wa GEPF kwa kiwango cha Asilimia 10 bila kufanyika marekebisho,na baadhi ya wanachama walioangalia mafao yao waligundua kuna tofauti yani GEPF waliweka kwenye akaunti ya mafao ya mtumishi kwa makato ya Asilimia 5% hivyo wakati huo mwanachama anaendelea kukatwa Asilimia 10 Hadi mwaka huu bila maabadiliko wa kulejeshewa fedha zao huu ni ufisadi wa kutisha unaofanywa na menejimeti ya GEPF au watendaji wachache wa GEPF kwa kushirikiana na Hazina ama Waajiri wa wanachama husika. kuna udanganyifu mkubwa,wizi na ufisadi wa fedha hizo.
Je nikiasi gani kina weza kuibiwa na watendaji wa GEPF kwa mfano wa viwango hivyo vya mishahara.
Mshahara wa Tshs.660,000 asilimia 5% Inayoibiwa ya Tshs 33,000 tufanye kuna wanachama 2400 wa kiwango hicho cha mshahara 33,000 x 2400 x miezi 12 fedha inayoibiwa ni Tshs.950,400,000
Mshahara wa Tshs. 580,000 asilimia 5% Inayoibiwa ya Tshs 29,000 tufanye kiwango hiki cha mshahara kinawanachama 8900 x 29,000x miezi 12 fedha inayoibiwa ni Tshs. 3,097,200,000.
Mshahara wa Tshs. 440,000 asilimia 5% Inayoibiwa ya Tshs 22,000 tufanye kiwango hiki cha mshahara kinawanachama 5700 x 22,000x miezi 12 fedha inayoibiwa ni Tshs. 1,504,800,000.
Mshahara wa Tshs. 380,000 asilimia 5% Inayoibiwa ya Tshs 19,000 tufanye kiwango hiki cha mshahara kinawanachama 6850 x 19,000x miezi 12 fedha inayoibiwa ni Tshs. 1,561,800,000.
Hivyo kufanya Jumla ya upotevu wa fedha za wananchama kiasi Tshs. 7,114,200,000. ambazo uenda watumishi wachache wa GEPF wamekula na familia zao hao wameziingaza kwenye biashara zao Tunawaomba TAKUKURU na JESHI LA POLISI kufwatilia jambo ili kwa karibu hata polisi nao hatuna imani nao maana wanaweza kukuta madudu na kupiga ah aha TAKUKURU tunawaamini sasa fuatilieni jamabo ili kama mlivyofanya kwa kina Sioi Sumari ,Kamishina mstafu wa TRA Harry Kitilya na Shose Sinare
Note. Viwango hivyo vya mishahara havitofautiani sana na viwango halisi ...pia idadi hiyo ya wananchama ni kadirio lakini ufisadi upo tena wakutisha.