Ufisadi wa kutisha kupitia kampuni ya AGRISOL: Serikali, Iddi Simba na Lawrence Masha wanahusika

Pamoja na kuanikwa huu uozo toka mwaka jana tunafanyaje juhusu hili? Manake hii habari ipo humu toka last year, Zitto, Mnyika, tunategemea kuwasikia mkihoji juu ya haya. Ili hata kama hakuna matokeo chanya walau watu wengi zaidi wajue hii manake hakuna gazeti wala tv itataja hii. Naanza kusikia harufu ya zimbabwe hapa, akiingia mwenye uchungu na nchi hii anaweza kujikuta anafanya yale ya Mugabe. Dah!
 
Wakina chief mangungo wamerudi tena upya.
Watoto na wajukuu zetu watatucheka sana baba na babu zao tulivokubali nchi kuuzwa kwa faida ya wachache, watatucheka kuliko hata wakina mangungo wa karne ya 18.
 
Sisi wenye kuweza kupata internet tuko wachache sana Tanzania hii, na wenye internet ya kuhakika ndio wachache zaidi.

Mimi ningeshauri hivi,
Mwenye uwezo a-download the whole thing, halafu aichome kwa CD watu wengi zaidi waione, waelewe na mwisho waamue wenyewe tunafanyaje kuikomboa nchi yetu.

Gawa copies kwa watu wanaoweza kuzalisha copy zingine wazigawe mitaani vijiji nk.. Kuanzia kwenye vyuo ndio safi zaidi.
 
Pamoja na kuanikwa huu uozo toka mwaka jana tunafanyaje juhusu hili? Manake hii habari ipo humu toka last year, Zitto, Mnyika, tunategemea kuwasikia mkihoji juu ya haya. Ili hata kama hakuna matokeo chanya walau watu wengi zaidi wajue hii manake hakuna gazeti wala tv itataja hii. Naanza kusikia harufu ya zimbabwe hapa, akiingia mwenye uchungu na nchi hii anaweza kujikuta anafanya yale ya Mugabe. Dah!

Sidhani kama kuna mtu atahoji zaidi ya kuendelea kuishawishi serikali ipeleke makampuni yakawekeze hayo maeneo kwa kisingizio cha kuwa nyuma kimaendeleo.
 
Nina wasi wasi na uraia wa baadhi ya watu mbona wanakosa ata chembe ya uzalendo?
 
Mkuu Jasusi niliandika hapa kama sikosei mwaka 2009 kwamba Kilimo Kwanza ni usanii wa hali ya juu katika kuelekea kampeni za uchaguzi za 2010 na wakadai mikopo itatolewa ili watu wakope na kuweza kushiriki kilimo kwanza. Kukazuka mtafaruku mkubwa wa kugombea nani anastahili kupata mkataba wa kuleta matrekta fake toka India kati ja Jeetu Patel na Yusuf Manji. Sasa inaelekea maneno yangu yamekuwa kweli kwani kilimo kwanza ni maalum kwa ajili ya kuendeleza ufisadi dhidi ya nchi yetu.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/40579-ufisadi-mwingine-kilimo-kwanza.html


Kila neno jipya tunalolitunga linaendana na matumizi makubwa ya fedha za walipa kodi. Maana lazima kuwe na branding. Nenda kwenye maonyesho ya sabasaba au kwenye shughuli nyingine za kijamii ukaone
 
Looh......hii inadhihirisha hii nchi ni tajiri sana...yaani pamoja na kutafunwa hivi bado inaendelea kuwepo...Laah!!!!!
Kimsingi wa CCM wote ni mafisadi ila tu bado wengine hawajajulikana!!!
 
IDHAA YA KISWAHILI / Masuala ya Jamii
0,,15639672_401,00.jpg

[h=4]Masuala ya Jamii[/h]
[h=2]
large.jpg
[/h]

Kampuni ya Kimarekani, AgriSol Energy, inatuhumiwa kupokonya ardhi Tanzania na inakadiriwa kuwa zaidi ya wakimbizi 160,000 wenye asili ya Kirundi waliokuwa wakiishi katika maeneo hayo kwa miongo kadhaa wameadhirika.
Kampuni moja kubwa ya nishati ya Kimarekani, AgriSol Energy, inatuhumiwa kwa kupokonya ardhi nchini Tanzania na inakadiriwa kuwa zaidi ya wakimbizi 160,000 wenye asili ya Kirundi waliokuwa wakiishi katika maeneo hayo kwa miongo kadhaa wataathirika na kadhia hiyo.
Pendo Paul na taarifa zaidi
Kwa mujibu waTaasisi ya Oakland, inayoshughulikia masuala ya mazingira, kuna malalamiko ya kimaadili yaliyoripotiwa na wakazi wa Iowa kwamba Kampuni hiyo ya AgriSol inapata faida kwa kuwanyang'anya kinguvu ardhi wakimbizi hao, ambao wengi wao ni wakulima wadogo wadogo, na kukodishwa ardhi hiyo na serikali ya Tanzania kwa senti 25 kwa heka moja, ardhi yote hiyo bila kulipa kodi ya aina yoyote ile.
Mradi huo unaweza ukaipatia kampuni hiyo, ambayo imeanzishwa na Bruce Rastetter, dola milioni 300 kwa mwaka.
Akielezea masikitiko yake, aliyekuwa mfugaji mmoja wa nguruwe kutoka mjini Rhodes, Larry Ginter, amesema amesikitishwa na uonevu huo unaofanywa dhidi ya wakulima hao nchini Tanzania.
Ginter anaongeza kusema kwamba mchezo huo unaofanywa na Agrisol umeanza siku nyingi na anavyoona yeye huo ni ukoloni wa kisasa, ambao ameuita ni wizi wa hali ya juu.
Hata hivyo, msemaji wa AgriSol nchini Tanzania amekanusha tuhuma hizo na kudai kuwa ni serikali ya Tanzania yenyewe ndio iliyoasisi makubaliano hayo ya kuwaondoa wakimbizi hao zaidi ya laki moja na sitini.
Akitoa utetezi huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano nchini Tanzania, Henry Akona, amesema si sahihi kuinyooshea kidole Kampuni ya Agrisol katika sakata hilo.
Katika tovuti ya kampuni hiyo, kuna taarifa inayodai kwamba mradi huo umechelewa kuanza huko Katumba na Mishamo kutokana na malalamiko hayo. Na mradi huo utaendelea tu pale madai hayo yatakapotafutiwa ufumbuzi.
Jinsi Tanzania inavyohusika
Mradi wa AgriSol uliungwa mkono na serikali ya Tanzania ili kwenda sambamba na Kilimo Kwanza, mkakati uliozinduliwa mwaka 2009 na Baraza la Kitaifa la Biashara TNBC, ukiwa na lengo la kuimarisha maendeleo ya kilimo kupitia ushirikiano na sekta ya umma na binafsi.
Katika ushirikiano huo, ArgiSol itasaidiwa katika kupewa ardhi ya kilimo cha kibishara kitakachohusisha mazao ya chakula kama vile mahindi na soya pamoja na ufugaji wa kuku.
Ili kutekeleza hilo, kampuni hiyo ya Kimarekani imejiandaa kuzindua uwekezaji wenye thamani ya dola milioni 100 nchini Tanzania katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Lengo kuu la AgriSol linasemekana ni kusaidia kuimarisha ugavi wa chakula cha ndani ya nchi, kutoa fursa za ajira na uchumi kwa wananchi wa Tanzania na hivyo kuchochea uwekezaji katika kuimarisha miundombinu ya nchi hiyo.
Kwa upande wake Anuradha Mittal, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Oakland, ambaye amefanya utafiti nchini Tanzania, amesema sera hizo zinazuia biashara ya ndani kwani wenyeji hao wameambiwa kuwa hawataanzisha biashara mpya. Mittal ameongeza kusema kwamba wakimbizi hao hawana chao isipokuwa kuhama makazi hayo.
Kwa mujibu wa hati ya makubaliano iliyoandikwa na Iddi Simba kwa niaba ya AgriSol, serikali ya Tanzania iliionyesha kampuni hiyo maeneo matatu ya ardhi magharibi mwa nchi hiyo, ambayo awali yalikuwa ni makambi ya wakimbizi ambayo yalitakiwa kufungwa katika siku za usoni.
Hata hivyo, Simba hakuwa serikalini wakati wa kuandikwa kwa makubaliano hayo. Alilazimishwa kujiuzulu mwaka 2001 katika ngazi ya uwaziri wa biashara, baada ya kugundulika kuwa alitoa vibali haramu vya kuingiza sukari nchini Tanzania.
Na Kampuni ya AgriSol imetamka wazi kuwa imeachana na mpamgo wa kuwekeza katika maeneo ya Katumba na Mishamo. Kwa sasa, inalenga kuwekeza katika miji ya Kigoma, Lugufu na Basanza.
Mwandishi: Ndovie, Pendo Paul\IPS
Mhariri: Josephat Charo
 
kilimo kwanza? hivi kilimo kwanza ni kwa ajili ya wawekezaji wageni au ni kwa ajili ya kuwaendeleza wakulima wadogo wadogo? au ni ka-mradi kengine ka kuwawezesha wanene na wafadhili wao wa nje kuchukua mikopo na kujigawia ardhi kwa mgongo wa kilimo kwanza?

tusubiri tuone huko mbele............
 
Idd Simba ni tapeli la kimataifa kutokea Burundi angalia kwenye uwaziri likapiga dili la vibali,UDA likauza shirika bila watu kujua,Pride watu wanalia kwa riba kubwa kwenye salama condom wanasema zinapitisha ukimwi huyu angekuwa uarabuni angekuwa ashanyongwa
 
US firm faces Tanzania land grab accusations
Sunday, 15 July 2012 11:22

A peasant tends her crop in Tanzania. A major US energy company, AgriSol Energy, is accused of engaging in land grabs in Tanzania. photo | FILE
Washington, Saturday. A major US energy company, AgriSol Energy, is accused of engaging in land grabs in Tanzania that would displace more than 160,000 Burundian refugees who have lived there for decades, according to a report by the Oakland Institute, an organisation focused on environmental issues.

An ethics complaint from the Iowa Citizens for Community Improvement (CCI) states that AgriSol is benefiting from the forcible eviction of the refugees, many of whom are subsistence farmers, and leasing the land -- as much as 800,000 acres -- from the Tanzanian government for 25 cents per acre. "All duty and tax free," the Iowa CCI adds. The project could net AgriSol, led by co-founder Bruce Rastetter, as much as $300 million a year, according to the Iowa Ethics and Campaign Disclosure Board.

Larry Ginter, a retired hog farmer from Rhodes and a member of Iowa CCI, said in a telephone conference that he was "outraged at the exploitation of the farmers there (in Tanzania)."

"This is an old pattern that has been going on for years," he adds about AgriSol. "This is a classic case of colonialism, and is theft of the highest order."
A spokesperson for AgriSol Tanzania denies those allegations and claims that the government had been the one that had instigated the movement of refugees. "We did not evict them," Henry Akona, director of communications for AgriSol Tanzania, told IPS.

"Perhaps it has been mishandled," he said, regarding the movement of refugees. "But it's unfair for the Oakland Institute to mix AgriSol into it."
The company's website states that the project is delayed at the settlements of Katumba and Mishamo "until the situation is resolved".

The AgriSol project was supported by the Tanzanian government under an initiative called Kilimo Kwanza -- meaning "Agriculture First" -- that was launched in 2009 by the Tanzania National Business Council to "promote agricultural development through public-private partnerships".

The "public-private" partnership would, currently and in the future, aid AgriSol in three different types of production: large-scale crop cultivation, such as food grains, beef and poultry production, and soy and maize production. AgriSol was set to launch a $100-million investment in Tanzania over the next 10 years. The stated aim of the programme, according to AgriSol was to, "help stabilise local food supplies, create jobs and economic opportunity for local populations, (and) spur investment in local infrastructure improvements."

The demands that ArgiSol made included such lopsided conditions that AgriSol would effectively "pay less for land in Tanzania than for a Starbucks coffee in the United States," according to Anuradha Mittal, executive director of the Oakland Institute.

Mittal, who conducted field research in Tanzania, said these policies have been supplemented by aggressive moves to stymie local businesses.
"The people on the ground have been told they can't build new businesses," she said. "They have no other option left but to move."

This partnership, according to the report, was also contingent on several other factors including that the Tanzanian government grant AgriSol a preferential "strategic investor status" and relocate the 162,000 people currently living in Katumba and Mishamo.(Agencies)
 
Inawezekana watu wamesamehe; lakini pia wamesahau au wanaamini sote tumesahau? You can't compromise beyond a compromise! When a compromise is no longer a compromise, it becomes a capitulation! I mean a categorical capitulation!
 
Back
Top Bottom