Ufisadi wa Kufa mtu TANAPA: Hebu angalia Mkakati ulivyokaa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa Kufa mtu TANAPA: Hebu angalia Mkakati ulivyokaa!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ndyoko, Dec 28, 2011.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Kama ulidhani ufisadi umekwisha ktk sekta ya maliasili na utalii, fikiria upya. Haijulikani hili lilipangwa bila kujua au la, lakini ukiliangalia kwa jicho la tatu utagundua kuwa 'dili' za ufisadi bado zinaendelea kuchezwa tena kwa ustadi mkubwa.

  Kwa kuzitumia benki za EXIM na CRDB wizi mkubwa umeendelea kufanywa kupitia sekta ya utalii. Hebu tujiulize inaingiaje akilini kwa nchi masikini kama TZ kuendelea kuzikarimu benki tajwa hapo juu kuchukua dola 5 kwa kila dola 30 zinazolipwa na watalii wanaotembelea mbuga zetu za Taifa? Hili limefanyika kwa maslahi ya watanzania au ndo mtindo ule ule wa 10% tulouzoea? Haiingii akili kwani kwa style hii ni wazi benki husika zinavuna kiasi kikubwa cha hela bila kuzifanyia kazi.

  Habari za awali zinaonyesha kuwa huu ni mkakati maalumu uliopangwa na 'wakuu' ili kufanikisha wizi wa rasilimali za nchi kutoka maliasili zetu kwani ilionekana ni ngumu sana kufanya ufisadi kupitia uwindaji au usafirishaji wa wanyama hai kwa kuwa huko wananchi walizinduka zamani. Inaelezwa kwamba kati ya hizo dola 5 kwa kila kichwa kinachoingia mbugani, ni kiasi kidogo sana kinachoingia kama mapato ya benki kwa kuingia kwao mkataba na serikali. Sehemu kubwa ya hizo dola 5 (kati ya dola 3.5 na 4), zinaingia mifukoni mwa wakubwa 'mafisadi' wanaoendelea kuitafuna nchi hii na mfumo mzima wanaoutumia.

  Ama kweli 'haka kanchi katamu kama ukikapatia', mweeeeh!
   
 2. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2011
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kweli hii?

  Source? authority?
   
 3. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  crdb bank ilihusika katika wizi wa mipesa ya EPA
  ila siku nyingine jaribu kutuwekea kaushahidi japo kadogo,hii bado tetesi
   
 4. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Yaani wewe bado uko gizani sana, hujui kama kila mtu Tz ni fisadi. Tofauti tu ni kwamba mafisadi wengine wameshajulikana na wengine hawajajulikana.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  this deserves jail penalty.. Poor and damading contracts.
   
 6. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kama ni kweli, basi waungwana MAJIZI yana mambinu
   
 7. sakapal

  sakapal JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,824
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza nani kakwambia benki inapitisha pesa tu achukue mwingine hiki ni chombo cha pesa kinachoaminiwa na wananchi na si kufanyia ufisadi mimi ni mtumishi wa benki kwa miaka mingi sana sisi tunatafuta pesa kwa wingi na ndomana tunalipwa mishahara minono ukiambiwa lete ushahidi hapa jamvini kwa ulichoropoka unao au unahisi tuu
  ulaji unafanyika epa na si benki binafsi nenda kakague pesa zinazopita bot na kutoka ndo utajua ufisadi usichafue benki zetu tafadhali
   
 8. r

  rwazi JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huwezi kusema kila mtu ni fisadi,labdawewe jitaje kuwa ni fisadi
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona unanena kwa kinywa kipana? Sina hakika na analolosema mtoa mada lakini kumbukumbu zangu zinaonyesha kwamba pesa za EPA zilipitia kwenye commercial banks na CRDB ikiwa ni mdau mkubwa! Una maana huko benki hakuna mishemishe mkuu? Najua mishemishe kibao mnapeana mapande halafu bahati nzuri huwa hamshitakiani kwa kuogopa kuharibu public image!
   
 10. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  We kenge kweli kwani umesikia hapa ni mahali pa kujidai eti una mishahara mikubwa. Nenda kwa geti lolote la TANAPA uulizie ndo utapata majibu ya hii maneno. Kanchi kanaisha haka
   
 11. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Wewe acha uongo! CRDB ni wezi sana! kuna mdogo wangu aliweka fixed term mwaka 2000, akasafiri kwenda US kusoma. amerudi akakuta pesa zimeliwa na kijana namhifadhi jina tawi la Holland House ! tulifuatilia mpaka leo hakuna kitu! kijana alifukuzwa kazi na pesa mpaka leo haijarudi! eti ikimature wanaweka kwenye sundries ! sijui banking ya aina gani hii imekaa kifisadifisadi! kwa kawaida pesa ikimature inatakiwa irudi kwenye account ya mteja ya savings ai current lakini cha ajabu eti zilipelekwa sundries zilipomature na watu WALAMBA SANA KWENYE SUNDRIES! sasa wewe usitake kuitetea hii benki! ni wezi tena mafisadi! mie na ndugu yangu TUMESHITAKI KWA MUNGU na atalipa tu ! maana tumecungushwa kama pear mpaka tulichoka tukaamua kukaa kitako!

  NA hizo dola 5 kwani banking si ni debit credit! zilipelekwa kwenye account ambayo inaweza kutolewa kupelekwa kwenye account nyingine halafu irushqwe kwa mafisadi kwani haiwezekani! labda uwaongopee ambao hawajui banking ! CRDB ni dhulumati wakubwa!
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  mkuu nadhani jamaa hafanyi kazi benki manake amesema kitu ambacho hakipo. Labda benki binafsi haina maana ya commercial bank. Hajui kiwa commercial banks ndio zinatumika kama conduits za kutakasa pesa chafu! Hajui kuwa huwa wanapitisha debit entry kwenye account za wateja wakubwa na kuzipeleka kwa wahindi na baada ya mwezi wanapitisha credit entry kurudisha pesa baada ya kuwa wamepata riba isiyo na.jasho toka kwa wahindi! Hajui kuwa kitu inaitwa debit na credit inaweza tumika kuchezesha pesa kutoka account moja kwenda nyingine hadi ikafika kwa fisadi ikawa vigumu kutrace!

  Mkuu mwambie mdogo wako akatafute haki yake hata ikiwa ni kwa Kimei aende kama inashindikana aende Bank Kuu kitengo cha Bank Supervision hienda akapata msaada. TUSISEME KUMEJAA RUSHWA. NENDENI MKAJARIBU NAJUA KUNA WATANZANIA AMBAO WANACHUKIA RUSHWA NA.BADO.WANAISHI
   
 13. Catagena

  Catagena Member

  #13
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is a stupid arrogance...Who cares about your big salary? We all know that you guys collude with all those who embezzle the government money.

  Remember, JF is used as a tool to disentangle all the evil deeds...coming up with pay arrogance is a sign of immaturity...and you dare call yourself a great thinker? That's next to impossible...A bank teller can never be a great thinker..no no no no. You can tell a ripe corn by its look (Chinua Achebe)
   
 14. A

  Ame JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  CRDB ni wezi kwa njia nyingi sana kwani hata kwa riba wanazotoza katika mikopo yao ni utata mtupu. Hawaiweki information vizuri ya jinsi wanavyotoza micro credits zao matokeo yake wanawaibia walala hoi zaidi kuliko wafanya biashara wakubwa. Ukichukua mkopo mdogo CRDB riba kwa mwaka ni zaidi ya 40% huku kwenye ki-leaflet wanakwambia riba ni 18% bila ku-specify ni kwa muda gani hiyo riba siyo per annum bali per month ambapo ukifanya compunding ina aggregate kwenye zaidi ya 60% kwenye payback period ama life time ya mkopo zaidi ya kile ulichochukua kwenye mkopo. Information ni moja ya kitu muhimu katika decision making kwasababu kila mwandamu ni rational lakini wao wameamua kwa makusudi kutoelimisha wateja ili wawaibie tofauti na mabenki mengine kama Azania etc ambayo in aggregate riba yao haizidi 20%.
   
 15. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Mkuu jitazame upya inawezekana hujijui kuwa akili yako haina tofauti na ya mwendawazimu aokotaye makopo. Siamini kuwa wale tulowaona wakiathiriwa na mafuriko maeneo ya jangwani, tabata na kigogo nao ni mafisadi. Nenda muhimbili pale kuna dk mmoja anaitwa Dr Nyandindi akakupatie tiba ya kichaa
   
 16. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  akili hii inakusaidia peke yako mkuu!
   
 17. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Wakuu kama ukipata nafasi tembelea mageti ya TANAPA kama mtalii wa ndani au vyovyote vile, mtajionea ukweli wa hili jambo. Suala la kujiuliza ni hizo dola tano kwa kila mtalii kwenda benki mazima ni pesa nyingi kwa kazi ambayo haiendani na uhalisia.
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu Ndyoko, utatusaidia sana kama utatufafanulia hasa kwa nini hizo benki zinapata hizo dola tano.
  Ninachohisi ni kuwa: Umeanzishwa utaratibu wa watalii kulipa kwa kutumia kadi wanapotaka kuingia kwenye vivutio vya utalii. Nadhani hizo benki mbili zinehusika wka namna fulani katika kutengeneza huo mfumo wa malipo na ndio maana wanapata hizo dola kama commission yao. lakini kama una taarifa nyingine tafadhali tujulishe.
   
 19. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kama hili lina ukweli kazi ipo.Nimekuwa nikitumia CRDB TANAPA card kwa muda sasa,mara nyingi network imekuwa tatizo.
  Kweli nchi hii inaliwa na wenye meno na si wenye maneno.
   
 20. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  kwa uchambuzi wa haraka umeonyesha upeo mdogo sana wa uelewa. \na hapa kuna mawili, 1. inawezekana wewe ni teller tu kama kweli wafanya kazi benki au, 2. kama ni kiongozi then hiyo benki imekula hasara maana huna mchango wa maana huko benki, 3. inawezekana pia huo 'mshahara mkubwa' unaodai unaupata benki basi ni baada ya 'kupromotiwa kimwili'.
   
Loading...