Ufisadi wa kampuni ya Lugumi enterprises ilikuwa kete tosha ya kuiangusha CCM

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
604
1,000
CHADEMA hawakuzichanga vizuri kete zao mapema, wamekomalia ishu ndogo sana ya uwanja wa ndege Chato, japokuwa kwa machoni inaonekana ina muksheli namna ulivyojengwa hasa mkandarasi aliyepewa hiyo kazi kuonekana ana ukaribu na mkuu wa dola.

Wamesahau kuwa huyu mkuu wa kaya anajinasibu kuwa anapiga vita ufisadi na katika vita hivi vya ufisadi watu wengi wameenda magerezani na wengi wamefilisiwa mali zao. Mfano ni wakili msomi na mwanasheria nguli Dk Ringo Tenga.

Kama akina Tenga na wenzake wamekaa magerezani na kisha wamekuja kulipa fedha mbona Lugumi na wenzake Magufuli hajawachukulia hatua?

Serikali kupitia waziri wake wa mambo ya ndani wakati huo Kangi Lugola alikiri kuwa Lugumi alitapeli jeshi la polisi bil 49 za kitanzania ili afunge mitambo ya kuchukua alama za vidole vituo vya polisi vya wilaya Tanzania nzima.

Lakini waziri huyo alikuja kufanya mazungumzo na Lugumi huku hakuna hatua zozote za kisheria zikichukuliwa dhidi ya Lugumi na wenzake.

CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani ilitakiwa wambane Rais Magufuli, kwa nini anawamamata baadhi ya wahujumu uchumi kama Dk Tenga, lakini Lugumi na wenzake wanaachwa?

Kwa hiyo mapambano ya ufisadi hapa Tanzania ni kwa ajili ya watu fulani, lakini wengine hawakamatwi wala kuguswa! Kwangu mimi naona CHADEMA hii ilikuwa kete nzuri ya kuwanyoosha hawa CCM.
 

pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
11,597
2,000
Lugumi ni nani?
Hii kampuni ilikuwa na 'mikono' ya akina nani?
Walikamatwa ktk uhujumu uchumi? kwanini hawakukamatwa?
Ukipata majibu sahihi ya maswali haya kila kitu kipo vizuri
 

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
604
1,000
Lugumi ni nani?
Hii kampuni ilikuwa na 'mikono' ya akina nani?
Walikamatwa ktk uhujumu uchumi? kwanini hawakukamatwa?
Ukipata majibu sahihi ya maswali haya kila kitu kipo vizuri
Hapa ndio pa kushikilia,na kwa nini wengine wakamatwe kwa ufusadi? Wengine wanaachwa? Kama JPM yupo serious.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom