Ufisadi wa CIS (zaidi ya Bilioni 180) kuibuliwa upya... Kikaango kwa Vigogo wa zamani (Wabunge, Mawaziri, n.k) chaja!

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,037
9,953
Kweli nchi hii ina wezi, kuna watu walipiga hazina fedha za commodity import support yaani CIS wameambiwa wazirejeshe ndani ya siku 30. Wengine wanadaiwa tangu 1978 yaani tuko vitani jamaa wanapiga hela hazina. Hawa naona ngosha atazaa nao kabisa sio kulala nao mbele tu. Mwenye majina yao hebu atutajie machache.

=======

TANGAZO KWA WADAIWA SUGU WA MADENI YA “COMMODITY IMPORT SUPPORT” (CIS)

Katika miaka ya 1980 hadi 2000 Wahisani walitoa fedha za kigeni kwa Serikali ya Tanzania kwa mpango maalum uliofahamika kama “Commodity Import Support (CIS)” kwa lengo la kuipa Serikali uwezo wa kuimarisha uchumi kwa kuzipatia Taasisi, Makampuni, Viwanda na wafanyabiashara uwezo wa kuagiza bidhaa na malighafi kutoka nje ya nchi, kwa kuwa wakati ule nchi ilikuwa na upungufu mkubwa wa fedha za kigeni.

Fedha za msaada za CIS zilitolewa kama mkopo wenye masharti nafuu kwa wanufaika, ambapo wakopaji walitakiwa kulipa deni bila kutozwa riba katika kipindi cha miezi 18.

Kwa mujibu wa sheria ya CIS {The Commodity Import Support Regulation Act, CAP 261 R.E. 2002 (S. 8 (1) (b)}, mkopaji akichelewa kulipa katika kipindi cha miezi 18 tangu kupatiwa mkopo, atapaswa kulipa riba ya asilimia sawa na kiwango kinachotozwa na Benki Kuu ya Tanzania inapoikopesha Serikali (discount rate) katika kipindi husika.

Zaidi ya makampuni 980 yalikopeshwa chini ya utaratibu huu. Pamoja na juhudi kubwa iliyofanywa na Serikali ya kuwataka wakopaji wote kurejesha mkopo huo, ikiwa ni pamoja na tangazo la tarehe 30 Desemba, 2015, bado urejeshaji wa mikopo hiyo umekuwa sio wa kuridhisha.

Ili kuhakikisha wadaiwa wote wanalipa mikopo yao, Serikali imeunda Kikosi Kazi ambacho kinajukumu la kufuatilia na kukusanya madeni toka kwa wadaiwa wote ili fedha hizo ziweze kutumika kwa miradi ya maendeleo.

Serikali inawataka wadaiwa wote kulipa madeni hayo ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kutolewa kwa tangazo hili. Kwa wote ambao hawatarejesha mikopo hiyo katika kipindi cha siku 30, majina yao yatatangazwa katika vyombo vya habari na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Kikosi Kazi, Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es Salaam, chumba Na. 352, Simu Na. +255 739 40 30 25.

KATIBU MKUU
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

Hii si mara ya kwanza kuambiwa wajisalimishe. Mwaka 2008 baadhi ya makampuni yaliyokopa kwenye mfuko wa Commodity Import Support (CIS), walipewa siku saba wajitokeze kueleza namna watakavyolipa madeni yao kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria, wamiliki wa makampuni zaidi ya 150, yakiwemo yanayomilikiwa na vigogo, walijisalimisha kwa wakala aliyepewa kazi ya kukusanya madeni hayo.

Habari zaidi, soma=>Vigogo wajisalimisha kwa Rais Magufuli. Ni wa makampuni yaliyochota Sh bil 300 za CIS

Kampuni 25 zilizochota CIS kufilisiwa

Vigogo waliokopa CIS wajisalimisha

TUHUMA:Vigogo, wakalia mabilioni ya CIS

CIS 180bn scam: Tanzania Govt to act
 
Ndo maana yule mgonjwa wa ubelgiji alikuwa anakomaa serikali ina njaa kumbe ndio janja yao!
 
Wakuu,

Huu ni mmojawapo kati ya “michongo” iliyopigwa enzi zile na tukapiga kelele sana humu JF tukaitwa majina yote!

Sasa, naona LEO serikali imeibuka ghafla na kutoa notisi ya siku 30 tu wawe wamejisalimisha. Patatosha?

Back
Top Bottom