Ufisadi ushuru wa forodha siri nzito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi ushuru wa forodha siri nzito

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 9, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  *Wahusika watajwa, ni Waarabu
  *Waporomosha maghorofa Kariakoo
  *Washirikiana na vigogo, maofisa wa TRA


  Na Waandishi wetu, Raia Mwema

  TAARIFA zimekuwa zikimiminika chumba cha habari cha Raia Mwema kuelezea zaidi mtandao wa wizi wa mapato yatokanayo na ushuru katika bandari ya Dar es Salaam ya kuwa ni mpana zaidi na unawahusisha wafanyabiashara wakubwa na wanasiasa vigogo.

  Taarifa hizo ni za maelezo ya ziada juu ya habari kuu ya gazeti hili ya wiki iliyopita iliyoandikwa chini ya kichwa: Ripoti Maalumu; Ufisadi wa kutisha Ushuru wa Forodha.

  Familia ya wafanyabiashara vijana wenye asili ya Kiarabu, imeelezwa kujilimbikizia mali kwa ufisadi huo katika ukwepaji kodi na sasa wamekuwa wakijenga majumba makubwa katika maeneo ya Kariakoo na pembezoni mwa Dar es Salaam.

  Wakiongozwa na kaka yao, vijana hao wa Kiarabu wapatao watatu kwa sasa wanaelezwa kuingiza faida ya zaidi ya Shilingi bilioni tatu kwa wiki.

  Katika baadhi ya taarifa hizo, Raia Mwema limetajiwa wafanyabiashara na wanasiasa wakubwa, wa zamani na wa sasa, ambao ni washiriki katika mtandao huo lakini kwa sababu za wazi, na hasa kwa kuwa hawakuweza kupatikana, majina yao hayatatajwa kwa sasa.

  “ Tunasubiri kuona kama mtaandika tena. Msije nanyi mkapewa (Sh.) milioni 50 au 100 mkaacha. Wizi huu una mtandao mpana na unahusisha wafanyabiashara wakubwa na vigogo. Mnaweza nanyi mkapewa fedha mkanyamaza, au wakakunyamazisheni kwa mbinu nyingine, ” alisema msomaji mmoja katika ujumbe wake kwa Raia Mwema wiki iliyopita akijitaja kuwa ni mfanyabiashara wa Dar es Salaam aliyekerwa na kuathiriwa na mtandao huo.

  Alisema mwingine: “ Kama ni kuchangia Chama cha Mapinduzi (CCM) sisi tumekuwa tukichanga hata katika wakati ambao hawa (anataja jina la kampuni) hawakuwapo na chama hakikuwa na wachangiaji wengi.

  “Nakuambieni mlichoandika ni jambo linalofahamika wazi pale TRA (Mamlaka ya Mapato). Ni kilio cha wateja na wafanyabiashara wote wanaohusika na uingizaji na utoaji mizigo bandarini. Hata huyo Kamishina Kitilya (Harry Kitilya, Kamishina Mkuu wa TRA) anajua kinachoendelea, katika majibu kwenu amejibaraguza tu.

  “Nina ndugu yangu amekuwa akisumbuliwa kwa miezi sasa ili kutoa mizigo yake, mara barua, mara bima, mara sijui nukta gani kwenye barua, basi ili mradi asumbuke mpaka apitie kampuni yao.”

  Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, baadhi ya wafanyabiashara waliokwisha kukerwa na usumbufu huo bandarini Dar es Salaam na katika ofisi za TRA na Tiscan, wamekuwa wakipitisha mizigo yao katika bandari za Beira, Msumbiji na Mombasa, Kenya.

  “Sasa tazama, Serikali kila mara inalia kwamba mapato hayatoshi, lakini hayatoshi vipi wakati inaruhusu wizi katika moja ya vyanzo vikubwa na muhimu vya mapato? Fikiria hawa wanaokwenda kupitisha mizigo Beira na Mombasa ni Watanzania, tena wengi wao wakazi wa Dar es Salaam. Wanakubali kuingia shida ya kwenda mbali lakini wafanye kazi nzuri ambayo sasa inaingiza mapato Kenya na Msumbiji,” anasema mfanyabishara huyo kwa masharti kwamba jina lake lisitajwe.

  “Kwenu waandishi wa Raia Mwema, kwanza sina budi kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya kwa kutupatia habari za uhakika na bila kuonea mtu. Leo (wiki iliyopita) najitokeza kuliunga mkono gazeti lenu katika jitihada za kufichua ufisadi ambao kila kukicha Serikali imekuwa inaupigia kelele,” ndivyo alivyoanza msomaji mwingine ambaye kwa sababu za wazi naye hatutamtaja jina.

  Aliongeza: “Habari yenu ya ukurasa wa mbele toleo namba 136 ni ya kweli. Vijana hawa wako watatu (anataja majina) wana asili ya Saudia japo ni Watanzania.

  “Ni kweli walianzia uwakala Tanga na Holili. Walihama baada ya ofisa mmoja wa forodha, namkumbuka kwa jina la Banny, aliyehamishiwa huko, kuwabana sana.

  “Wanashirikiana na viongozi wa juu wa TRA na wamejenga mtandao kuanzia bandarini, na ICD zote. Wanafanya wanavyotaka saa yoyote na wakati wowote kama vile hakuna Serikali. Ofisa yeyote atakayebisha kufanya wanavyotaka huhamishwa kituo mara moja.

  “Wamesababisha maofisa kadhaa kufukuzwa kazi. Nawakumbuka baadhi ya maofisa waliofukuzwa kazi pale Longroom; DICD na Container Terminal na wengine wamehamishwa vituo.

  “Kwa kawaida kampuni zote hufuata taratibu za kiforodha lakini kampuni zao hupita njia za mkato kwa kuandika barua ya kuomba provisional clearance na nyingi za barua hizo zinalenga kukwepa kodi.

  “Hizo barua za provisional clearance mara nyingi huandikwa Longroom kwa maelekezo ya vigogo wa TRA na zinakuwa zinaruhusiwa kutoa mizigo bila ukomo wa idadi na muda kwa bidhaa ambazo hazina sifa za kupewa provision.

  “Bidhaa zenye sifa ni kama malighafi za viwandani,vyakula na bidhaa za Serikali na za balozi. Si nguo, vitenge, kanga, saruji na nondo kama inavyofanywa sasa. Tafadhali pokeeni nakala za baadhi ya barua za aina hii za karibuni zaidi kwa uthibitisho wa mambo yanavyofanywa na wakubwa TRA kwa kushirikiana na mtandao huu.”

  Taarifa zilizotufikia wakati tukienda mitamboni jana Jumanne, zilisema kwamba ukaguzi mkali wa ndani umekuwa ukifanyika TRA kutaka kubaini nini ambacho kimekuwa kikendelea kuhusiana na ukwepaji ushuru.

  Wiki iliyopita, gazeti hili likikariri malalamiko miongoni mwa wafanyabiashara na wateja wapitishao mizigo yao katika bandari ya Dar es Salaam lileleza ya kuwa wakati Bajeti ya Serikali inasuasua kutokana na uhaba wa fedha za ndani, familia moja ya Dar es Salaam inayomiliki kampuni inayojihusisha na bishara ya bidhaa za nyumbani imejiingiza katika uwakala wa forodha kwa staili ya aina yake ikiwa ni pamoja na kujikita katika kuwasaidia wengine kukwepa kodi katika mtandao unaohusisha wanasiasa.

  Biashara hiyo ya aina yake ya uwakala wa ukwepaji kodi, imedaiwa imekuwa inaipotezea Serikali mabilioni ya shilingi ambazo zilistahili kukusanywa kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali wanaoingiza bidhaa mbalimbali kutoka China na Dubai.

  “Sasa ni vigumu sana, na kwa kweli hakuna wakala mwigine anayethubutu kutoa bandarini bidhaa za nguo kwa kuwa nyaraka za kampuni nyingine zifikapo Tiscan au Longroom huwekewa bei za juu ambazo hazilipiki ili kuwakatisha tamaa waagizaji ambao kwa sasa wamechoshwa na huduma za vijana hawa zilizojaa kiburi na dharau.

  “Hali hiyo imewafanya waagizaji kukosa pa kwenda bali kwa vijana hao na wakabaki wakisikitika jinsi vyombo vya dola vinavyowekwa mfukoni kwa hasara ya jumla ya Taifa. Waagizaji wanalalamika kwamba hawana tena uhuru kwa kuwa wanalazimika kutumia kampuni moja tu ambayo bei zake hazina majadiliano. Ukienda kubembeleza unaambiwa katafute wakala mwingine ambaye hata hivyo huwezi kumpata kwa kuwa hawa wamehodhi kila kitu,” alieeleza mtoa habari Raia Mwema aliyeko ndani ya sekta ya kodi.

  Mfanyabiashara mwingine alisema kwa hali halisi iliyopo kwenye mfumo wa ukusanyaji kodi, ni vugumu kukwepa ushuru kwa kudanganya kiasi (idadi) cha mali kilichomo kwenye kontena (false declaration) au kuweka bei ndogo au ya chini ya ile bei halisi (under invoicing), lakini kwa kampuni hii hilo linawezekana kwa kuwa mfumo mzima tangu serikalini, Tiscan na TRA umekuwa nyuma yao kutokana na nguvu kubwa ya kifedha waliyonayo.

  Imeelezwa kwmaba kwenye kampeni za mwaka 2005 kampuni hiyo ilichangia chama tawala Sh. Milioni 200 na kwamba katika mwaka huu wameahidi kuchangia milioni 500.

  Ili kufahamu kiasi cha mapato ya Serikali yanayopotea angalia hesabu hizi:

  Kontena la nguo za kawaida lenye urefu wa futi 20 laweza kuwa na thamani ya Dola za Marekani 60,000.00 hadi Dola za Marekani 80,000.00 kutegemeana na aina, ubora na idadi ya nguo zenyewe. Ushuru wa jumla ni 48% ya thamani halisi (cif value). Kwa hiyo kama thamani ni Dola za Marekani 60,000.00 x 48% = Dola za Marekani 28,000. Kwa thamani ya Dola 1 ya Marekani = Sh.1400, ushuru kwa kontena hili katika shilingi ni 40,320,000.

  Kama kontena ni la thamani ya Dola za Marekani 80,000, ushuru ni 80,000.00 x 48% ambazo ni sawa na Dola za Marekani 38,000.00 na kwa Sh ni 53,760,000.

  Kwa mujibu wa habari za ndani ya TRA, kampuni hii hukadiria gharama zote kwa meta za ujazo kutoka China hadi Dar es Salaam, na hivyo kontena la futi 20 ambalo lina meta za ujazo 36, ina maana gharama zote zitakuwa ni Dola za Marekani 450 x 36 = Dola za Marekani 16,200 ambazo ni sawa na Sh. milioni 22.68.

  Ikiwa utaondoa gharama halisi za kusafirisha kontena hadi Dar es Salaam ambazo ni Dola za Marekani 2,500, basi kinachobaki ni Dola za Marekani 16,200 – 2500 = Dola za Marekani 13,700.00 au Sh. 19,180,000.

  Uchunguzi wa Raia Mwema umeonyesha kwamba sehemu kubwa ya fedha hutumika katika kulipia ushuru kidogo, rushwa kwa maofisa sehemu mbalimbali husika, gharama za bandari na usafiri wa bandarini kwenda kwenye maghala yao.

  “Kwa uzoefu wangu kampuni hii kwa kontena la nguo la futi 20 hawalipi zaidi ya Sh. milioni 10. Hii ina maana ya kuwa badala ya kulipia gharama halisi ya zaidi ya Sh. milioni 40 wao wanalipa milioni 10 tu. Kwa hiyo, kwa mfano mmoja tu, Serikali hupoteza Sh. milioni 30 kwa kila kontena la nguo la futi 20 linalotoka bandarini. Ikiwa makontena 100 yanaweza kutoka bandarini kwa wiki moja, ina maana Serikali hupoteza milioni 30 x 100 = bilioni 3 kwa wiki. Kwa mwaka mmoja hii ni sawa na shilingi bilioni 156,” alieleza mtaalamu wa kodi ambaye kwa sasa ni mstaafu.


   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ukweli ndio huo nchi hii ni ya waarabu wahindi wasomali,hapo ndipo utakapoona jinsi ambavyo hakuna uwiano kati ya wananchi bado kidogo tuu wachina wakolea na watai watakuja juu kama kifuu cha moto,lakini yote yanamwisho amini usiamini ,watajuta na kusaga meno siku moja na hao watu wa TRA ni wakukata vichwa na kutupa mto Rufiji wabaya sana hawa watu hawana uzalendo hata kidogo sijui wanadhani wenye watakapo taka vitu vyao wao wataponea wapi ,majizi,majambazi makubwa TRA
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hawa jamaa walisimama sasa hivi wameanza tena naambiwa.?
  Kipindi flani walikuwa ndo wenyewe unawapa doc. tu ww unaletewa zigo mlangoni.
   
 4. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  La kawaida tu labda huwa hupati matolea mengine! kipi kipya hapo tofauti na la wiki iliyopita?

  page ya mbele ipo hapo juu a

  Page ya 2. Ufisadi ushuru wa forodha siri nzito
  page 3. Pengo amjibu askofu Kilaini, ewura yatangaza kushuka bei
  page4. Serkali yavurugana na wanunuzi wa pamba
  page 5. ewura na usanii wa bei za mafuta
  page 6. ewura inaendelea
  page 7. Rai ya Jenerali- wawakilishi kama wafadhili. kosa
  page8. Maoni- kulikoni Tendwa na CCJ, Bodi ya uhariri, tangazo TCRA-usajiri wa simu
  page 9. Tanroad: tatizo siyo ephraim mrema , tatizo ni ikulu
  page10. Wazee wasikwepewajibu, nchi inawalilia
  11. mbwambo- ya jaubary makamba na ridhiwani kikwete, walipata kunena haya
  12 na 13 , ziwa victoria hatarini, lakini laweza okolewa
  14 dfakika 90 tu, bilioni tatu za kuileta brazil zimekwenda, BBC shirika namba moja la utangazaji duniani
  15 Zanzibar kwa tanzania kama eritrea kwa ethiopia (2)
  16Tunavyoenenda na kisa cha mfuga mbwa
  17Harambee za chama si maslahi ya taifa
  18 wamejiandikisha wapate kitambulisho si wapige kura
  19uchaguzi 2010: somo kutoka "Serengeti symphony"!
  20 Muendelezowa habari kutoka page 11, 9 na 15
  21 Tangazo toka TBS
  22, 23, and 24 michezo
  15.
   
 5. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Unataka kusemaje hapa MS. Nilidhani umeanza kupona kumbe malaria bado inasumbua....
   
 6. W

  WaMzizima Senior Member

  #6
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ufisadi upo kila mahali hapa duniani tofauti ni jinsi nchi mbalimbali zinavyo deal na hili swala kujaribu kuzuia ushawishi wa ufisadi na vilevile hatua zinazochukuliwa iwapo unakuwa fisadi.
  Hivyo basi ni wazi kuwa hata Tz ufisadi ulikuwepo tangu enzi hizo za ukoloni tofauti kuu na sasa ni kuwa angalua tuna uwazi kuhusu haya masuala. Enzi za JKN isingewezekana kwa dr Slaa kusimama na kutangaza list yake ya mafisadi maana;
  • Kwanza hakukuwa na vyama vya upinzani
  • Uhuru wa habari haukuwepo
  • Tolerance ya kukosolewa haikuwepo vilevile
  Hivyo ni wazi kuwa Serikali za Mkapa na Kikwete kwa kweli zimejitahidi kwa kiasi fulani kuruhusu uhuru wa habari na vilevile tolerance ya upinzani inaongezeka hapa nchini kulinganisha na miaka iliyopita. Na kwa hilo ni budi kuwapongeza viongozi wetu...
   
 7. C

  Calipso JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nilikua nakuamini saana M/kijiji lkn leo umeniangusha.. umeonesha wazi ubaguzi na udini,yaani umeonesha wazi kufurahia ubaguzi,hilo gazeti ni la wa-Kristo na lengo lao kuuchafua Uislam,kwani wanaona mafisadi wengi ni kutoka huko upande wenu,sasa wanaamua kuzusha ya kuzusha,na vile vile wanaona walojenga wengi hapo kariakoo ni waznz,sasa wanaamua kuwachafua.. Yapo mengi yanakuja lkn yoote ni uzushi...
   
 8. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  HUu ni wehu sasa!
   
 9. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poor you!
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Athari za Madrasa ni kubwa sana kuliko unavyoweza kufikiri!
   
 11. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...AAARRRGGHHH!! Hivi kila kitu lazima tuingize hoja feki za Waisilamu Kuonewa hata kama hazipo, jamani??? Grow Up!
   
 12. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Si lazima uchangie kama una "prejudices" zako. Wapi kuna udini kwenye hii post?, je nani amekwambia uarabu ni uislam?, hakuna watu mafir-aun kama hao unaowatetea. Unless na wewe ni one of them, hawa watu wanashirikiana maafisa wa TRA- Je na TRA nayo ni ya waislam?, Harry Litilya kamishna mkuu wa TRA ni muislam?, Maana maafisa wote wa TRA wanamuwakilisha Harry na harry naye anamuwakilisha rais. Mtu yeyote anayetumia njia za panya kunyonya watanzania huyo ni lazima aangaliwe kwa kurunzi zito bila kujali dini, kabila wala rangi yake.

  Hebu tujadili mada hapa tuache kulialia, Twaha Ulimwengu aka Jenerali Ulimwengu(one of Raia mwema founders) ni mtu ambaye yupo neutral na hata kujua dini yake ipi ni mpaka ukutane nae kwenye ibada, sasa iweje Raia mwema liwe la kikikristo?. Sometimes malalamiko mengine huwa yanatufanya tuonekana kuwa ni watu wa kulialia tu hata panapokuwa na genuine claim sababu ya watu kama ninyi.

  Haya Tujadili mada ya raia mwema si kuleta usisi na u-wao hapa. Kama umetumwa kuleta destruction kajipange upya hii itakuwa ime-backfire
   
 13. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Wakuu tuanikieni na majina yao kabsaaaaaaaa..
  naskia hakipiti kitu bila wao sa sijui ndo TRA No 2 au 1?..
  Hivi ni kweli Kitilya hafahamu au anajitoa fahamu maksudi..
  Na Ole wao iko siku...haya maviongozi yetu
   
 14. C

  Calipso JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Lengo si kutetea mafisadi,kila kabila kuna ufisadi ktk nchi hii,mbona wachaga wamejaa wengi tu mafisadi,na karamagi na Lowassa ni waarabu,bali ninachoogelea,kwanza gazeti silo,la pili ni kumuona m/kijiji akionesha wazi kabisa kufurahia kuona neno la uarabu tofauti na kawaida yake anavoleta mada au anavojadili mada,sio lazma mimi niwe mwarabu bali natetea mtu kuchukia kabila flani,lete maada kwa njia nzuri tujadili,sio kwa kufurahisha nafsi yako.... lkn samahanini wakuu. labda shule yangu ndogo ndio inanisumbua
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Calipso.. yaani kuanzisha mada nimekuwa mdini? Hivi nimetoa maoni yoyote hapa kuhusu kilichomo kwenye hilo gazeti wakati hata kulisoma sijalisoma!! Au nikiona habari ina jina la mtu anayedhaniwa ni muislamu niikimbie..?
   
 16. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hivi kwa busara zako unaamini kuwa uhuru ni kitu cha ruhusa au haki yako ya msingi kama binadamu?Na hizo kauli za kina Salva kwa Mwanahalisi,Mwananchi,nk zinatolewa na Ikulu ya Msumbiji au hiyo ya JK unayoisifia?

  Halafu lazima uelewe mazingira tuliyokuwa nayo miaka ya Nyerere na sasa ina tofauti.Wakati enzi hizo vyanzo pekee vilikuwa Radio Tanzania na Uhuru au Mzalendo,sasa tuna teknolojia ya mtandao ambapo japo TBC,Habari Leo,Uhuru na Mzalendo wanaweza kubana habari lakini zikaibukia Jamii Forums au kwenye blogs.Kadhalika,BBC wanaweza kudakwishwa breaking news kwa email au sms hivyo kufanya udhibiti wa kupashana habari kuwa mgumu.

  Unyonge wa kufikiri kuwa haki yako ya msingi ni ridhaa ya mtu au taasisi flani ni hatari kuliko utumwa.
   
 17. R

  Ronaldinho Member

  #17
  Jun 10, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Msameheni Calipso yawezekana uwezo wake wa kujadili mambo ni mdogo au katumwa pasi kupewa maelezo ya kutosha......
   
 18. GY

  GY JF-Expert Member

  #18
  Jun 10, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133

  Sasa Mwanakijiji kama hata kulisoma hujalisoma bado umejuaje ni moto?

  Au ndo kama nilivohisi awali, kuwa umeendelea kumkaribisha Jenerali kwa kupromote gazeti lake/lao/lenu
   
 19. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hadi watu flani wafe labda ndiyo serikali iamke. Suala kama hili lilizuka mwishoni mwa miaka ya 1990 pale ambapo ndugu watatu wa jamii ya Kihindi (waliokuwa wakimiliki kampuni moja ya Clearing and Forwarding -- Dewlo Brothers) walipowaua wafanyakazi wao wawili wa Kiafrika (na baadaye kuwachoma moto) ili kuwaziba midomo wasije wakatoa kwa vyombo husika habari za ufisadi wao wa ukwepaji kodi -- kama huu huu wa hawa jamaa wa Kiarabu.

  Ingawa Wahindi wao walikamatwa, na kufunguliwa kesi ya mauaji, walikuja shinda kesi baada ya kukaa takriban miaka 5 rumande. Kushinda kwao kesi bila shaka kulitokana na nguvu za pesa walizokuwa nazo walizotoa kwa waendesha mashitaka ambao waliivurunda kesi hadi yule Jaji aliyewaachia kutamka kwamba charge sheet na ushahidi uliowasilishwa na waendesha mashitaka ulikuwa ni aibu tupu!

  Nadhani twaiona sasa historia ikijirudia, na nahofia huenda kuna watu watakufa.
   
 20. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mhhhh !Mie najiuliza hivi: Hivi baada tu ya gazeti hilo -- Raia Mwema -- kuingia mitaani na bila shaka wakubwa (akiwemo JK, Mkulo, Hosea nk) kulisoma (JK kupitia kwa Salva of course), hakuna yeyote kati ya hawa aliyeinua simu na kumpigia simi Kitilya kumuuliza iwapo jambo hilo ni kweli au la? JK,kwa mfano angemtaka Kitilya kumpatia ripoti kamili in 6 hours -- na angeipatatu -- bcoz President's word is God's word).

  Lakini inaonekana JK hana ubavu wa kukabiliana na uchafu wa namna hii unaolishwa Watanzania, isipokuwa yuko tayari mara moja kumshabikia Kaka na Drogba katika kutafuta cheap popularity. Mambo haya hayawezi kuyashughulikia bcoz aliingia Ikulu siyo katika kutatua kero kama hizi.
   
Loading...