Ufisadi unaota mizizi Wizara ya Ulinzi!

The Fixer

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
1,365
593
Ndugu zangu Wana JF!

Ufisadi ndio unayoifanya hii Tanzania isiwe nchi ya Asali na Maziwa kama ambavyo tumekuwa tukiahidiwa kuifika na wanasiasa wetu Uchwara wa Tanzania, Nisema hivyo kwasababu uwezo wa kuifanya hili litamalaki upo ndani ya Rais wetu na viongozi katika nyanja mbalimbali lakini hawataki kuwa Wasafi!

Nikitoa mifano kidogo tu ya Wizara ya Ulinzi na Vikosi vyake kwa ujumla ndiko kulikojaa rushwa utadhani ni haramu kutokula hiyo rushwa;

Zabuni; Hiki ni kitengo ambacho kimejaa Ufisadi mi nadhani kuliko hata huko BOT ama inawazidi hao wa EPA pia, Wanatoa vibali kwa Wazabuni ya ana yoyote ili kwenda kutoa huduma mbalimbali za kijamii hasa kwenye makambi yetu ndio wanaangusha heshima ya jeshi, Yule ambaye hatoi rushwa mbele hapati kibali ila yule ambaye anatoa rushwa ndio anabebwa na Askari maafisa pale makao makuu na hata Wizarani,

Tenda ya kufungua maduka (Army Shops) katika majeshi wamepewa Wahindi, Huyu Mhindi anaitwa Mr Sadru huyu ndiye Tajiri anayeendesha na ile Supermarket pale Mwl Nyerer Int. Aiport. Huyu mzee anayo fedha ya kuhonga ya kutosha sana hawa Wanajeshi wetu na sisi kama watanzania hatukatai wawekezaji ila sasa kwahuyu Mzee anawaleta Wahindi wenzake kufanya hata kazi za Store ambazo watanzania wanaweza kuzifanya na Mbaya zaidi namna anavyowaingiza hapa nchini ni ndio kuna harufu mbaya kabisa kwani huyu Mhindi amewanunua Maafisa wa Uhamiaji kiasi kwamba inatia shaka sana na wanaingia nchini kwa visa ya matembezi lakini ndio inakuwa imetoka hiyo (Alafu wakati wa sikukuu za X- MASS huwa wanafungiwa zawadi kidede) na Halafu mfumo wa kazi katika zile Army supermarket za ajira sio nzuri ni wakibaguzi sana na hata malipo yake hayaridhishi kwa hasa Wazawa!

Malalamiko kama haya yamewahi kupelekwa makao makuu ya jeshi lakini wahusika wakija pale Dukani na wakionekana wana harufu yoyote ya kufanya uchunguzi wowote hufungashiwa mambo kibao kwani hadi Cement mtu mmoja anapewa hadi mifuku 50 Free of charge na Walipokuja kipindi flani pale Jeshini (Twalipo camp) mkabala na Saba saba Ground Trade fair ndio lilipo Duka hili pale utamkuta Mhindi mmoja anaitwa Mr Rafik, Huyu jamaa anatukana hadi Askari wa vyeo vya chini na Askari wakipeleka malalamiko ngazi za juu wanakuta Maafisa wao wameshanunuliwa siku nyingi kwa Fenicha hadi Magodoro na Friji za kichina ili kuwa nyamazisha.

Kila kitu kina mikataba ila sasa Jamaa wakitaka kusaini mikataba mipya mwanzoni hadi Askari utawasikia tu wanawasubiri kunako mkataba mpya utakapo sainiwa ila wakati ukifika.....Thubutu....Jamaa wanapitishwa kama kawaida na baada ya hapo haitapita hata week utaona Jamaa wanakuja na gari la jeshi na kupigiwa shopping ya nguvu kuanzia Vyakula hadi Bulb (Energy saver)

Sisi kilio chetu ni kwa hawa Mawaziri wetu wapya waliopewa Wizara hii , Haya niliyoyaainisha hapo juu ni kwa upande mmoja tu wa Maduka ila kama Nikijaaliwa nafasi tena, Ntakuja kuwapa katika upande mwingine wa shilingi hasa manunuzi kamili ya Jeshini !

Kama Mwinyi (Waziri) ataweza kuyadhibiti haya mambo tunamuombea heri sana manake hali ni mbaya kuliko maelezo!
 

Wasio pajua pale Mgulani ( Twalipo camp )waende tu wasiogope
kuna bidhaa za bei nzuri tu hadi redio ila zimeandikwa Made in China !
 
Mhhh Mheshimiwa kwani maduka hayo yalianzishwa Mwaka gani, na nani alikuwa Waziri mkuu na nani alikuwa waziri wa ulinzi, pia ni vizuri kujua tenda kubwa za jeshi kama hiyo hupitishwa na Wanabodi kina nani na kwa mtiririko upi. labda tuanzie hapo kwanza
 
Mhhh Mheshimiwa kwani maduka hayo yalianzishwa Mwaka gani, na nani alikuwa Waziri mkuu na nani alikuwa waziri wa ulinzi, pia ni vizuri kujua tenda kubwa za jeshi kama hiyo hupitishwa na Wanabodi kina nani na kwa mtiririko upi. labda tuanzie hapo kwanza
....

waziri wa ulinzi alikuwa kinana chini ya muheshimiwa rais mwinyi..enzi hizo..
 
Nimewahi kulia sana na madukani ya airport mkasema najifanya napanda sana ndege. Kuna watu haya kiswahili hawajui eti ndiyo wanauza pale. Nikashangaa kwa nini. Kuja hapa mkasema maneno kibao haya mengine hayo.
 
Huseni Mwinyi...jamaa mbona kimya sana yule?

Anajaribu kujifanya 'wa Busara' ili badaye propaganda za CCM zimpe Sura ya baba apate Urais.

But, anyhow. Jeshi sasa hivi linaachiwa makusudi ikiwa kama rushwa toka serikalini. Wanyamaze wasiwasumbue wakuu wa nchi.

Je, wajua hata terminal benefits zao sasa hivi zimewekwa sawa sawa? Na hivi karibuni Rais aliongeza muda wa kustaafu kwa kila rank ya kijeshi, eti zawadi yake kwa jeshi?
 
Back
Top Bottom