Ufisadi umetuweka pagumu Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi umetuweka pagumu Pinda

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pdidy, May 13, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,414
  Likes Received: 5,684
  Trophy Points: 280
  wanahabari kwangu mie hii ni vibweka.source habari leo

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kwamba kuibuliwa kwa masuala ya rushwa kwa viongozi wa serikali kulikofanywa na vyombo vya habari, kumeiweka serikali mahali pagumu, na kwamba sasa watendaji wake inabidi wawe makini zaidi.

  Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Dar es Salaam jana, Waziri Mkuu alisema kuibuliwa kwa masuala hayo ya rushwa kwa viongozi na kulazimisha wengine kujiuzulu, ni changamoto kubwa na sasa inabidi mawaziri wawe makini na waangalifu zaidi.

  “Hapa mlipotufikisha sasa ni pagumu,” alisema Pinda na kuongeza kuwa ingawa masuala mengi ya vitendo vya rushwa yalifanyika katika awamu zilizopita, lakini ni changamoto kwa serikali ya sasa kujitahidi kuhakikisha haiangukii katika mtego wa wengine kutuhumiwa kushiriki vitendo hivyo.

  “Hii imetufanya tuwe makini zaidi, (wanahabari) mmesukuma sana mambo. Mmefanya kazi nzuri na mnapaswa kuendelea kufanya kazi hiyo na ni juu yetu sisi kuhakikisha hatuingii katika mtego. Awamu hii inatakiwa tuwe waadilifu sana, ili hata kama itakapomalizika miaka mitatu minne, isije ikasemwa tena Mzee Pinda nawe ulichukua,” alisema Waziri Mkuu.

  Alivipongeza vyombo vya habari kwa kazi nzuri ya kufichua ufisadi, akisema yeye anaunga mkono kazi hiyo na kwamba muhimu ni kuhakikisha vyombo hivyo vinaandika habari za kweli bila kupotosha na pia kujali maslahi ya Taifa.

  Akijibu maswali ya wahariri hao kuhusu masuala mbalimbali, Waziri Mkuu alirudia kauli yake aliyoitoa bungeni mwezi uliopita kuwa wahusika wa kashfa ya Richmond watachukuliwa hatua kama ambavyo wamependekeza wabunge, lakini hilo litakwenda hatua kwa hatua.

  Mojawapo ya hatua hizo ni suala la uingiaji wa mikataba ambalo alisema linaonyesha Watanzania hawana ujuzi nalo, na akapendekeza katika mchakato wa kusaini mikataba, kuwe na kamati huru ya wataalamu binafsi itakayopitia na kutoa mapendekezo kabla ya mikataba kusainiwa.

  Alipinga wazo la mikataba hiyo kupelekwa kwanza bungeni, akisema chombo hicho cha kutunga sheria kitapoteza jukumu lake la msingi na kujiingiza katika matatizo. “Hatujalala, ila hatuwezi kukamata watu; kuwaweka ndani na kuchukua mali zao kama baadhi ya watu wanavyopendekeza.

  Hakuna anayetaka kukumbatia uovu, lakini zaidi tufuate taratibu,” alisema Pinda.
  Alikiri kuwa mkataba wa Kitengo cha Kuhudumia Makontena Bandari (TICTS) ulikuwa na walakini na kwamba serikali inafanya taratibu za kuhakikisha mkataba huo unapitiwa upya na kusema; “Nadhani la TICTS tutalimaliza.”

  Kuhusu wanasiasa wanaotuhumiwa kwa rushwa na ufisadi kupokewa kwa sherehe kubwa wanaporudi maeneo wanayotoka, Waziri Mkuu alisema hilo ni la mtazamo wa watu zaidi hasa wale wanaompokea.

  Kuhusu kauli yake ya kutaka mafisadi hao watenganishwe na vyama, alisisitiza kwamba si vyema wakahusishwa na chama au serikali kwa sababu siyo sera ya chama wala serikali kuhusu rushwa na ufisadi, bali matatizo hayo yanatokana na hulka na tamaa ya mtu binafsi. “Chonde, chonde, ufisadi siyo sera ya chama wala serikali; chama na serikali vinakemea hili.

  Mtu mmoja kwa sababu ya ulafi wake, tamaa zake, tukimpata jukumu ni moja; kumfuatilia achunguzwe na kisha sheria za nchi zichukue utaratibu wake,” alisema Waziri Mkuu. Alipoulizwa anajisikiaje kuhusu madai kwamba wapo baadhi ya watu waliokamatwa kwa kumzomea Rais mstaafu Benjamin Mkapa kwa madai ya kuhujumu uchumi, Waziri Mkuu alijibu;

  “Ninachoogopa ni kuanza kuhukumu watu, siyo nzuri, si sahihi. Kuchukua sheria mkononi si sahihi.” “Mimi siafiki hata angekuwa mtu mwingine yeyote. Huyu ana heshima yake, ni binadamu. Ana haki yake kama Mtanzania, ana mahali pake apelekwe huko. Zipo taratibu za kufuatwa, lakini siyo kuzomea,” alisema Waziri Mkuu katika mkutano huo uliodumu kwa zaidi ya saa mbili.

  Alipoulizwa kuhusu mikakati inayochukuliwa kupunguza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mkoani Mara, Waziri Mkuu alikiri kuwa Mkoa wa Mara una matatizo yanayotokana na utamaduni na hulka za wenyeji wa mkoa huo, lakini akapendekeza kuwa wataalamu wa sosholojia wapelekwe kufanya utafiti na kubaini jinsi serikali inaweza kutatua matatizo hayo
   
 2. r

  rushaka Member

  #2
  May 16, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama serikali ya awamu ya nne ina nia tahabiti ya kuhakikisha kweli haiangukii katika mtego wa wengine haina sababu ya kuendelea kuwakumbatia mafisadi katika utawala wake. Kama samaki wachache wameoza kapuni wataambukiza wenzao.
   
 3. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Pinda anajaribu kuelimisha jamii kuwa siyo wote wameusika, sijui tutaamini vipi hizo kauli zao
   
 4. m

  mpakakieleweke Member

  #4
  May 19, 2008
  Joined: Apr 14, 2008
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna kitu bado natafakari sikielewi vizuri. Toka lini mtu akamsifia mtu mwingine aliyemweka mahali pabaya na anamsifu aendee unautaratibu wa kumweka pabaya.
  Mhhhhhhh......?
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  sasa PInda anasema wamewekwa pabaya inamaana kuna mtu hapa Tanzania yupo juu ya sheria??kwa hiyo ugumu upo kuwakamata hawa mafisadi au??Bado hajaeleweka vizuri aonyeshe matendo tu mungwana ni vitendo.
   
 6. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Huyu mpaka kieleweke mwingine kasajiliwa vipi kwa jina langu? ama ndio wamekwisha kwiba password yangu jama ....
   
Loading...