Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,668
- 40,916
Kwakweli hali ilikua mbaya sana ilipofikia. Kila mtu aliyelipenda hili Taifa, alitaka apatikane kiongozi atakayeiondoa nchi kwenye uoza wa ufisadi uliopindukia, kukubalika na jamii na kufanywa kuwa mfumo halali wa maisha ya watanzania.
Sio mimi peke yangu niliyekua nikisubiri hilo kufanyika, bali kuna wengine wengi ambao watakubaliana na mimi kuwa kulikuwa na umuhimu wa hatua stahiki kuchukuliwa ili kulimaliza tatizo.
Unakuta kijana anamaliza chuo, anaajiriwa kwenye taasisi ya serikali, baada ya mwaka, anakuwa na nyumba kadhaa, magari kadhaa, biashara kadhaa na mabibi kadhaa, lakini kwa uhalisia wa mshahara wake hakukuwa na uwezekano wa hayo yote kufanyika kwa muda mfupi sana. Ulihitajika muda.
Utaratibu halali wa maisha ya binadamu, mambo hufanyika kwa hatua na sio kwa mkupuo na kasi ya aina yake kama mfano nilioutaja hapo juu.
Ukifuatilia kiini cha fedha anazotumia kijana niliyemtaja hapo juu katika mfano nilioutoa, utakuta ni fedha za serikali ambazo zilikua ziende kwenye miradi ya maendeleo , ila zimekua diverted kwenye mifuko ya wachache.
Mfumo wa matumizi na wizi wa fedha za serikali, ulirasimishwa na kua halali, kiasi kwamba jamii ilimshangaa kabisa mtu mwenye ajira serikalini na kushindwa kupata maendeleo kwa kasi.
Baada ya awamu ya tano kuja na kuziba mianya yote ya ufujaji, kwa namna yoyote ile beneficiaries wa hiyo mirija iliyozibwa lazima wayasikie maumivu. Kwa kua fedha hizo zilikua rasmi na zilikuwa zikiingizwa kwenye mzunguko wa fedha, hakuna ubishi kwamba uchumi uliotegemea fedha hizo kwa namna moja ama nyingine utaathirika.
Baada ya uchumi uliotegemea ufisadi uliorasimishwa kutolewa upepo, uliobaki ni uchumi halisi na ndio uwezo wetu halisi wa kifedha.
Kama tunalengo la kujenga Taifa letu, tunaweza kutengeneza mifumo bora ya utafutaji wa kipato na kujenga Taifa lenye kufuata utaratibu kwa raia wake katika kufikia malengo ya kila mmoja kimaendeleo.
Tunayo nafasi ya kufanya hivyo, na tunaweza kufanikiwa kama tukitaka.