Ufisadi ulijengwa na Mwinyi, Mkapa akaubariki na Kikwete Kauvalia Kibwebwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi ulijengwa na Mwinyi, Mkapa akaubariki na Kikwete Kauvalia Kibwebwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Aug 29, 2012.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Nionavyo mimi ile misingi ya maadili ya viongozi na wananchi kwa jumla ilipobomolewa na Ally H. Mwinyi pale Zanzibar mwaka 1990. Kuanzia hapo Mwinyi akaanza kuuza mali zetu kwa waarabu. Akauza Loliondo, mwandishi wa gazeti la "Mfanyakazi" nd. Katabalo aliyekuwa mstari wa mbele kuandika juu ya ufisadi huo akafariki kwa kifo tatanishi. (hapa uelewe kuwa mbinu za kuuwa watu watetezi wa umma ziko za aina nyingi mfano, kukolimbism, za kimabwepande, nyereretype n.k)

  Nd. Mkapa akasonga mbele zaidi; ubinafsishaji (kujirundikia na kujichotea mashirika ya umma kwa bei mbovu). uchimbaji wa madini yetu kiuwizi wizi kuanzia kwenye mikataba hadi migodini kwenyewe. Vyombo vya dola kuwa sehemu za ugaidi wa kiuchumi na biashara haramu kama "human trafficking"; magenge ya ujambzai yayomilikiwa na makamanda; uwi na uporaji wa magari na mabenki.

  Nd. Kikwete katika utawala wake kuna fununu nyingi za ufisadi kwenye vitalu vya gesi na mafuta. Uporaji aridhi, uuzwaji wa aridhi kwa wamarekani na waarabu. Kuuza wanyama wetu ambao Mungu alitupatia kama zawadi yetu watanzania. nk.

  Woote hawa ni magamba chama cha kimabwepande policy. Tuchukue hatua. Tuwakatae kuanzia leo. Nashauri tukutane mtandaoni tupeane mikakati ya kusimamia demokrasia ya kweli. JAMAA HAWA WANG'OLEWE. Tuonane kwenye Facebook, Tweeter, JF. Tukikutana hadharani watatu-"arushisha" ama watatu"morogoresha" kama ilivyo kawaida yao.
   
 2. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,176
  Likes Received: 1,257
  Trophy Points: 280
  Rama Ighondu yuko njiani kukutafuta!! lakini wote tukae tayari maake sasa wameamua kulinda ujambazi kwa mtutu wa bunduki na mambo mengine!
   
 3. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uhuni katika Tanzania
   
Loading...