UFISADI TFF: Malinzi mwogope Mungu, Fedha za TBL dola 425,000 umezichota kutoka akaunti hizi

Malinzi ameharibu mchezo wa mpira kabisa.wadhamini wanakimbia kutokana na ubabaishaji
 
Habari wanaJF

Ndugu zangu wanaJF na Watanzania Malinzi aache kupotosha umaa kuwa Ufisadi ulitosemwa hapa JamiiForums ni kwasababu ya mwaka wa uchaguzi, Mimi nadhani waandishi waliopata nafasi ya kuongea nae hawakua na maswali ya msingi ya kumuuliza, naomba ajibu maswali haya Malinzi kama kweli anavyodai Ufisadi wa TFF ni kauli za kuelekea kwenye uchaguzi mwaka huu 2017.

NB: Ukiacha fedha hizo za TBL zilizochotwa bila maelezo, FIFA wamegoma kuleta fedha zingine TFF tangu Septemba 2016 mwaka jana mpaka query (maswali ya ukaguzi wa kifedha) kuhusu matumizi ya dola za kimarekani milioni 1.5 kukosa maelezo/viambatanisho juu ya zilivyotumika.

Wewe naona unaleta porojo tu hapa na sijui lengo lako ni nini? TAKUKURU inasema wanafanya uchunguzi wewe unasema wanachelewa sana kufungulia mashtaka yaani wewe unajifanya ni Hakimu, wazee wa baraza na mnyongaji all rolled in one!!! Wewe unajuaje kwamba hizo fedha hawajazitolea maelezo ya kuridhisha kwa TAKUKURU, mtu ukisoma tu maelezo yako yanaonekana wazi wazi unasukumwa na chuki binafsi, huko obsessed na Malinzi na Mwesiga basi, sio kwamba nawatetea lakini usianze kuhukumu watu kwa kutumia hisia tu.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
"Taarifa za ndani ni kuwa wiki iliyopita Mwesigwa alikwenda Dodoma kuonana na Waziri Mkuu, Mh Kassim Majaliwa kuomba awalinde kwani Takukuru wamezidi kuwaandama kila kukicha na hii inaonekana kuwaogopesha Takukuru kuwapanidisha kizimbani ukizingatia uchunguzi wote walishakamilisha."

Hii para ina utata. Ina maana huyo mkuu huko Dodoma ana mamlaka hayo??? NASHANGAA TU KWA SAUTI KUBWA
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Habari wanaJF

Ndugu zangu wanaJF na Watanzania Malinzi aache kupotosha umaa kuwa Ufisadi ulitosemwa hapa JamiiForums ni kwasababu ya mwaka wa uchaguzi, Mimi nadhani waandishi waliopata nafasi ya kuongea nae hawakua na maswali ya msingi ya kumuuliza, naomba ajibu maswali haya Malinzi kama kweli anavyodai Ufisadi wa TFF ni kauli za kuelekea kwenye uchaguzi mwaka huu 2017.

1. Ni kweli Malinzi uliitwa kuhojiwa na TAKUKURU juu ya ufisadi huo?

2. Edgar Masoud alikuwa Mkurugenzi wa Fedha TFF? na alienda likizo kipindi gani? na alifukuzwa kazi kipindi gani?

3. Je ni kweli Nsia aliletwa na kupewa madaraka ya ukurugenzi wa Fedha, ikiwa Daniel Msangi mzoefu akiwepo ofisini akikaimu Edgar kwenda likizo?

4. Kipindi cha Julai 2016 - Fedha zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya dola TBL (Wadhamini wa timu ya Taifa Stars) kwenda kwenye akaunti za kawaida?

4. Aliyehusika na kuweka sahihi kuhamisha hundi hizo alikua Edgar Masoud, Daniel Msangi au Nsia?

6. Ajira za wakuu wa Idara za TFF huthibitishwa na Kamati ya Utendaji, Je, ajira ya Nsia ilipitishwa na kamati ya Utendaji?

7. Kilichofanya Malinzi ampiganie Mwesigwa kuongezwa mkataba kwa kuwapigia magoti wajumbe wa kamati ya utendaji ni kuendelea kulinda madudu yao ya fedha walizokwapua.

Leo naweka wazi akaunti zilizotumika kuhamisha fedha hizo na kisha kutokomea kusikojulikana.

TBL walilipa fedha za udhamini kwa awamu mbili yaani (quater) za Novemba - Janauri 2016, Februari - May 2016 zilizoingizwa benk Julaai 2016.

Fedha hizo ziliwekwa na TBL katika akaunti ya ya TFF ya dola za kimarekani namba Acc 9120000312647, kiasi cha dola laki 425,000 Stanbic tawi la Kinondoni (Ubalozi wa Marekani) na kuhamishwa kwenda akaunti ya kawaida TZS Acc 508320, Acc 139368 na Acc 139384 bila karatasi za maelezo (supporting documents).

Kumbuka fedha za TBL hutumika kwa ajili ya maandalizi ya Taifa Stars ikiwa safari, kambi, posho za wachezaji,makocha na viongozi wanaoambatana na timu kama inavyoonesha kwenye mkataba.

Aliyeweka sahihi kuzitoa fedha hizo kutoka akaunti moja kwenda nyingine kabla ya kuzitoa zote kabisa ni Mwesigwa Selestine (Katibu Mkuu TFF) na Nsia (aliyeajiriwa ndani ya wiki mbili na kutambulishwa benki hiyo kama Mhasibu wa malipo yote ya TFF).

PCCB wameshawahoji wahusika wote juu ya uhamishwaji wa fedha hizo, lakini tunaona mpaka sasa wamekua waoga kumpandisha kizimbani Malinzi pamoja wasaidizi wake waliohusika akiwemo Mwesigwa na Nsia/

Taarifa za ndani ni kuwa wiki iliyopita Mwesigwa alikwenda Dodoma kuonana na Waziri Mkuu, Mh Kassim Majaliwa kuomba awalinde kwani Takukuru wamezidi kuwaandama kila kukicha na hii inaonekana kuwaogopesha Takukuru kuwapanidisha kizimbani ukizingatia uchunguzi wote walishakamilisha.

REJEA UZI HUU: UFISADI TFF: Bil 1.1 zachotwa ndani ya wiki 1, PCCB washikwa na kigugumizi kumpeleka Malinzi Kortini

NB: Ukiacha fedha hizo za TBL zilizochotwa bila maelezo, FIFA wamegoma kuleta fedha zingine TFF tangu Septemba 2016 mwaka jana mpaka query (maswali ya ukaguzi wa kifedha) kuhusu matumizi ya dola za kimarekani milioni 1.5 kukosa maelezo/viambatanisho juu ya zilivyotumika.

YAMETIMIA!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Wewe naona unaleta porojo tu hapa na sijui lengo lako ni nini? TAKUKURU inasema wanafanya uchunguzi wewe unasema wanachelewa sana kufungulia mashtaka yaani wewe unajifanya ni Hakimu, wazee wa baraza na mnyongaji all rolled in one!!! Wewe unajuaje kwamba hizo fedha hawajazitolea maelezo ya kuridhisha kwa TAKUKURU, mtu ukisoma tu maelezo yako yanaonekana wazi wazi unasukumwa na chuki binafsi, huko obsessed na Malinzi na Mwesiga basi, sio kwamba nawatetea lakini usianze kuhukumu watu kwa kutumia hisia tu.
Bado msimamo wako ni ule ule kua mleta mada ana chuki Binafsi na Malinzi na mwenzie Mwesiga??
 
H aha aha aha aha aaaaaa Yule si Nsia Swai.
_20170629_142742.JPG

Nsia ndo huyo mama hapo mbele?
 
YAMETIMIA!

Wewe naona unaleta porojo tu hapa na sijui lengo lako ni nini? TAKUKURU inasema wanafanya uchunguzi wewe unasema wanachelewa sana kufungulia mashtaka yaani wewe unajifanya ni Hakimu, wazee wa baraza na mnyongaji all rolled in one!!! Wewe unajuaje kwamba hizo fedha hawajazitolea maelezo ya kuridhisha kwa TAKUKURU, mtu ukisoma tu maelezo yako yanaonekana wazi wazi unasukumwa na chuki binafsi, huko obsessed na Malinzi na Mwesiga basi, sio kwamba nawatetea lakini usianze kuhukumu watu kwa kutumia hisia tu.
 
Hapa naenda mbali na kuwaza kwa sauti juu ya fedha za Rugamarila wa ESCROW zaidi ya Tzs 306 Bn. Hawa jamaa hatari sana
 
Hili jamaa kumbe jambazi kabisa?! Aise mafisadi na UFISADI kila kona, mbona hii nchi ilioza!
 
Tunahamasishwa tuichangie Serengeti Boys kumbe watu wanabunya tu hela za FIFA na TBL kiulaini
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom