Ufisadi TAA: Mhindi wa Flamingo apewa Tenda aliyonyimwa Mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi TAA: Mhindi wa Flamingo apewa Tenda aliyonyimwa Mtanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Aug 6, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Ndugu wapendwa ,...mmmh haka kakidudu cha ufisadi naona akaishi kabisa...sasa dawa yake naona si maneno tuamue kufanya na vitendo...hivi karibuni afisa mmoja wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa tanzania BW TESHA....,alifanya vituko vya ajabu...kwa wale wanaoujua uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere..ukiwa unaingia kuna open space iko upande wa kulia...hiyo sehemu ilitangazwa wanaongeza uwanja kwa ajili ya parking...gafla wakaambiana chinichini kuna sehemu imebaki tunwezatengeneza hotel...ikatangazwa wazi....mtanzania mmoja akaenda kuomba wakiwepo baadhi ya watu...gafla ile tenda ikawa dili.....,yule ofisa akatangaza wamesitisha hawana mpango wa kujenga tena ile sehemu....
  Baada ya muda kama mmefika karibuni kuna ujenzi ulikuwa unakamalika ..kabla ya mmoja wa waliomba tenda akaambiwa wamesitisha mpaka alipoingia hivi karibuni na kukuta ujenzi unamalizika ...walipoulizia akaambiwa amepewa yule yule muhindi wa flamingo...ambae ndie huyo amepewa lounge.amepewa supermarket..amepewa dutyfree shop.......amebakiza kupewa uwanja wa kutulia ndege......
  Ndugu watanzania inafika wakati lazima tuwathamini watanzania wenzettu...kwamba wanauwezo wa kufanya chochote...alipokuwa akiulizia aliambiwa amepewa kwa sababu wanaitaji mtu anaeweza kuitengeneza ikaonekana ati sehemu ya kimataifa...tobaaa ilala,,,,mi nafikir kuna umuhimu mkubwa wa kuwachunguza sana hawa mabwana ambao wako TAA miaka na miaka...BWA MSANGI NA BWANA TESHA....HAPO HIYO COMBINATION YA MCHAGA NA MPARE...INATUREJESHA KWENYE UTUMWA KABISA...WANA DHARAU SANA ...HATA IKITOKEA UKIPINGANA NA HUYO MUHINDI AKIKUFIKISHA KWAO UMEKWISHA BILA HATA YA KUJIELEZA....
  UFISADI UTAISHA LINI JAMANI???????????????
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Tunavyoongea hivi sasa kesi iko mahakamani.....wamesitisha ujenzi ule
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ile AIRPORT kwa kweli hadi inatia Kinyaa. Sehemu zote za ndani wamekaa Wahindi. Maduka yote yamejaa Wahindi na ndani hata bidhaa za Tanzania ni za kuhesabu. Hii hali kweli ilinitibua sana. Nilikuwa na hamu niiandike ila nikawa nagwaya.

  Nafikiri inabidi hili lipigiwe kelele na hawa watu waulizwe, imekaaje Wahindi ndiyo washike yale maduka yote? Yaani hakuna Mpingo hata mmoja anaweza kuendesha ile biashara ya maduka pale DIA?
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  hiyo cha mtoto wakamuulize msangi ile kesi waliokuwa nayo kwa waziri wa miundombinu ati kuna kampuni ya ndege iliomba kurent office 4 pale JNIA...KILICHOFANYIKA akaambiwa atengeneze ofisi saba then wakatane...yule bwana akaona ujinga akaenda mbele ya safari....kesi iko kwa waziri..je ni haki swala la vibanda/ofiisi za taa apelekewe waziri sababu ya hawa mafisadi wawili tesha na msang?????oooooooooooooooh no giv m a break
  kwa nini wasiamishwe....imagine ndugu wapendwa pale duty free office mtanzania unahesabu na baya zaidi post kama za accountant,nk zile muhimu wamepewa wafilipino...kama if hakuna watanzania jamani.....loh....mi nilishasema sitonunua kitu pale..wanadai duty free ukinunua bei haina tofaut na sehemu nyingine jamani?????

  KAWAMBWA ONDOA HIZI PRESSURE......
   
 5. M

  MC JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hii kweli inahitaji kufanyiwa kazi,

  Kwa ufupi huo uwanja unatia Kinyaa kwa kila kitu, nafikiri watu wanaendekeza pesa kuliko kazi, creativeness = 0.

  Hepu fikiria, sehem ya Passport Check kwa wanaowasili, Mnapanga mstari na Vyoo viko pembeni yenu kushoto na unasikia harufu....

  Shame on them,
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Yaani afadhali wangekuwa wanavitunza vizuri vile vyoo
   
 7. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Hiyo combination ni hatari, kama ya D. Yona na Mramba, eh!!
   
 8. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Halafu mnashangaa kuwa Nchi yenu iko katika nyanja za mabingwa wa madawa ya kulevya na bidhaa haramu!
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Zile ngazi za umeme zote zimekufa milele. Hizo lift ni kutengeneza tu Motor zake ambazo nafikiri Tanzania wanaweza kuzishughulikia. Joto la ndani hadi linatisha. Labda siku hizi kama wamebadilisha. TV zote zimekufa na matangazo wanaandika kwa chalk kwenye ubao.
  Ndiyo matatizo ya kujengewa kila kitu. Kikiharibika, huwezi hata kukitengeneza.
  Kila kitu Muungwana atakuambia "tunasubiri wafadhili". Hata kujenga vyoo na kuleta maji Airport na kuweka matanki ya maji machafu, nalo twasubiri Wafadhili....

  Ile DIA tangu wajenge mashemeji zetu (wafaransa wakaowa na dada yetu mtoto wa Kawawa) hadi leo ukiacha barabara za ndege, majengo yako vilevile na sanasana yamepunguzwa. Ukifika pale basi unapata kithibitisho hasa kuwa tumelogwa.
   
 10. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Duh inaelekea formation zao zinaendana!!

  Hapa TZ ni ajabu sana na sijui ni lini tutabadilika. Ni muhimu sana kuwasaidia wazalendo hasa pale inapokuwa si lazima kupata hiyo huduma au bidhaa toka kwa mgeni.

  Hata sheria yetu ya manunuzi inasema wazi kuwa wanaruhusiwa kufanya upendeleo kwa watu wa ndani "local preference' ila nadra kuipata. mi huwa nakosa tender kwa kushindana na watu wa nje naumia sana. hiyo hela ningeitumia hapa na bidhaa zangu unakuta ni za ubora unaokubalika. hiyo hela ningeitumia hapa na si ajabu ningeajiri zaidi na unakuta niko juu kidogo kiasi kwamba nikiitwa niko tayari kuwa sawa na lowest sometimes. Najiuliza hivi nikienda Ujerumani au India nikomba tender nikawa lowest kwa specification sawa na wengine nitapewa???? haiwezekani!! sijui sisi tutabadilika lini?

  Wanatushangaa hata hao wageni tunaowapapatikia. We really need changes from bottom to the top top top level
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii ndo anasema Rev.Kishoka tumeuza uhuru wetu sie wenyewe na miwaziri ipo ipo tu inaangalia kama mibogus na isitoshe inapitia hapo hapo sijui inapewa 10%?
   
 12. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Hapa tatizo nini jamani?
  maanake sielewi elewi!
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Habari za wajinga wa kihindi nimesha isema sana sana .Mie ni mtumiaji mzuri wa uwanja huu lakini hata Duty Free shop eti ni wahindi hata wageni hutushangaa .Wahindi wenyewe hakuna hata mmoja anaongea kiswahili , kama mnabisha siku ukiwa kule jaribu utaona mambo ya ajabu .Pare zauzwa bidhaa za nje kwa wingi na sisi bidhaa zetu sijui tuna uzia wapi .Hivi JK huwa hapiti uko akaona ?
   
 14. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Nchi ilishauzwa hii,watu wake na kila kilichomo ndani.Yaani nchi ya Tanzania na watanzania wenyewe na ndiyo maana kila kitu kinaenda kwa hao mnaowakataa kushika vitega uchumi vya Tz.Viongozi waliopo ndiyo wasimamizi wa kuhakikisha mambo yanaenda kama wanavyotaka mabwana wakubwa.
  Kwa maana nyingine wanaofanya upuuzi huo wanaitwa vumilia vumbi;kwasababu mabwana wakubwa wanawagaragaza wanavyotaka na hakuna anayebisha.
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mhindi hawezi kuwa mtanzania?

  Amandla........
   
 16. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #16
  Aug 6, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Sema FM,

  Watanzania ni wabaguzi sana. Mie kwa mfano niliona maji yametengenezwa nje ya Tanzania na nilipodadisi wakajibu kuwa bidhaa zote zile hata kama zimeandikwa made in India, ukweli ni kuwa wanafanya hivyo ili kuongeza UJIKO ila ukweli ni kwamba zote ni MADE IN TANZANIA na wanafanya kubadilisha label tu.

  Nilipotaka kujua kwa nini wote wanaonekana ni Wahindi, akasema ni macho yangu tu na hiyo inaongeza sana ujiko kwa watu kama Wahaya ambao huwa wanajiona kama Wazungu vile. AKasema wengi wao ni MIPINGO kabisaa ila wanavaa tu ngozi za kihindi na kujifanya hawajui Kiswahili ili kupandisha hadhi ya DUKA.

  Hivyo Wana JF, zile bidhaa zote mle ni za KITANZANIA, na wale wahindi wote ni Watanzania. Msilalamike kabisaa.
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Nakumbuka ile makala yako. Ila sikuchangia siku zile kwa kukosa muda.

  Wale Wahindi bwana. Mshikaji wangu mmoja nilitaka kumuuliza hii imekaa kaaje na nyie kuweka Wahindi hapa. Ila nilipoangalia cheo chake na wapi yupo Tesha, nikajua huyu jamaa hapa ni Kisamaki kidogo sana. Sikutaka kumpa hard time jamaa yangu, nikajikalia kimya.
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ujiko kwa nani? Tangu lini kitu Made in India kimekuwa na ujiko? Hata kwenye pharmacy zetu wanajua hilo! Mpelekee mkeo kanga ya India wakati amekuagiza ya Urafiki uone kama atafurahia.

  Kutokujua kiswahili sasa kumekuwa ishara ya kutokuwa mtanzania?

  Mnapunguza nguvu za hoja yenu kwa kuingiza ubaguzi. Kama tatizo ni mtu kunyang'anywa haki yake, tuko pamoja. Hata kama aliyemnyang'anya ni mdogo wake wa kuzaliwa baba na mama. Kama tatizo ni huyo unayemuita mhindi kufanya biashara kwenye uwanja huo wa ndege, basi huko siko. Naona wengine wameishawaingiza wapare na wachaga katika rada yao! Mtakuja kumalizana mkiendekeza upuuzi huu!

  Amandla......
   
  Last edited: Aug 6, 2009
 19. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #19
  Aug 6, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hiyo India ilikuwa mfano tu na siwezi kuandika nchi hasa.

  Sasa ubaguzi wa nini wakati jamaa ni Watanzania?

  Tuwape nchi yote Wahindi hawa maana Tanzania ni yao na wao ni Watanzania. Wapeni Airport, Mabenki, Polisi, Jeshi, Bunge, Mahakama, ATCL, mbuga za wanyama nk nk. Vinginevyo kukiuka amri hiyo ya kutokuwapa basi itakuwa ni UBAGUZI.

  Kila la kheri.
   
 20. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #20
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wewe hutamalizwa? Au umehama nchi?

  Kikwete nae anaongea hivyo hivyo; alipofungua mkondo wa Fiber Optics, anasema mkongo huu unatoka Tanzania, unaenda Rwanda, Uganda, Burundi, hivyo shughuli zao zitapita hapa kwetu, na sisi kibiashara tutapata kidogo, msipofanya hivyo "hampati." Kina nani hawapati? Nyinyi, wewe Fundi Mchundo na Kikwete sio Watanzania?

  Kama kuna wafanyabiashara wa makabila na rangi zote nchini, lakini opportunity fulani wanapata watu wa rangi na asili moja tu, hapo kuna tatizo. Hilo tu linaweza kuzua machukizo yanayoweza kupelekea machafuko. Wawe wamepata hizo biashara kihalali au kiharamu mwisho wa siku ukijaza Wahindi tu sehemu si busara, si fair. Akitokea right wing nativist mmoja akawa-sensitize watu watamsikiliza, kama Ujerumani ya Hitler na Wayahudi .

  Ni sisi ndio tutakaomalizana, wewe Fundi Mchundo labda hautakuwepo, tutakaomalizwa tuko concerned.
   
  Last edited: Aug 6, 2009
Loading...