Ufisadi Stendi ya Mabasi Dodoma, Rais Magufuli fuatilia hili

kamanda mbigi

JF-Expert Member
Feb 8, 2017
1,241
1,546
Siku chache zimepita kituo cha mabasi ya mikoani Dodoma kilianza kufanyiwa ukarabati kwa kujenga jengo la maofisi na kuzungusha uzio ili mamlaka zikusanye ushuru vizuri.

Wiki hii uzio huo umewekewa maandishi "BOMOA" na "X" kubwa tu. Sasa inakuaje mamlaka tofauti za serikali moja kubomoleshana majengo kana kwamba hawana mawasiliano baina yao.

NOTE:
Eneo ambapo kituo cha mabasi kipo ni mali ya shirika la reli. Sasa kwanini manispaa wametumia gharama kubwa kumlipa mkandarasi na wakati wakijua wanajenga kwenye eneo ambalo sio lao.

Kama sio kichaka cha kupigia pesa hapo ni nini.

45275165e423820a3b849888daeda43f.jpg
688bc8ba666666a3474bdfafed9685d0.jpg
9cf7fc69188d25accb813c268dfb9207.jpg
 
Back
Top Bottom