Ufisadi si kuchukua pesa tu

Sir

Member
Aug 4, 2009
12
0
Kumekuwepo na tabia ambazo hazifai katika jamii ya watanzania na wengi tunaangalia tu bila hata kujiuliza ni kwa nini.

Kwanini mtu ajifikirie yeye ni muhimu kuliko mtu mwingine hasa katika kupata huduma ambazo ni muhimu kwa kila mtu?
Mara zote nikienda kwenye ATM naona watu wamekuwa wastaarabu kwa kufuata utaratibu either umewekwa mioyoni mwao au katika mazingira waliyopo.Utaratibu wenyewe ni kupanga mistari na kumsubiri aliyeko mbele amalize na kuondoka (hapo natoa hongera)

Lakini suala tofauti linakuja barabarani hasa kwenye foleni zetu, mtu bila aibu anakuta mmejipanga kusubiri kuruhusiwa cha kushangaza mtu huyo huyo anapita vinjia vya pembeni na kwenda mbele alafu anataka aruhusiwe kuingia barabarani, hapo ndio inashangaza akili inayotumika, kwamba una haraka zaidi? huyo mbele yako hana akili ya kupita pembeni? wewe ni muhimu zaidi? au ni kujipendelea kuliko watumiaji wengine wa barabarani

Hii nimeihusisha na ufisadi kwa nini? Mtu anayejiona anahitaji kumiliki mali nyingi kwa njia za udanganyifu na bila ya kumhurumia mtanzania mwenzake tena bila aibu hana tofauti na huyu jamaa wa barabarani ambaye hajali kuonwa na wenzake akifanya utaratibu ambao siyo.

Ukianza kujiona wewe unahitaji zaidi ya wenzako au kuliko uwezo wako popote ulipo unakaribisha ufisadi iwe ofisini, barabarani hata kwenye huduma nyingine kama benki, tanesco,n.k

Charity begins at home, tukishindwa kurekebisha vitu vidogodogo tukaviona vya kawaida ipo siku mtu aliyefanya ufisadi mkubwa tukamraki kwa mbwembwe na vifijo kwa jambo alilofanya au kwa kilatini tunasema IN CAUDA VENENUM (In the tail (is) the poison) Sumu ya nyoka ipo mkiani
 
Daah!! hii kaka umeiweka shwafii sana, Mazoea haya sasa yamekuwa tabia,hapo nyuma kidogo kabla sijapata Mkoko wangu nilifikili tabia hii wanayo wandesha daradara tuu kumbe bwana hata watu wa humu humu kwenye hili javi la JF wamo!
ukiwauliza kulikoni? utawasikia," eeh eeh Mafuta na foleni Mkuu".
Eebo!
 
Daah!! hii kaka umeiweka shwafii sana, Mazoea haya sasa yamekuwa tabia,hapo nyuma kidogo kabla sijapata Mkoko wangu nilifikili tabia hii wanayo wandesha daradara tuu kumbe bwana hata watu wa humu humu kwenye hili javi la JF wamo!
ukiwauliza kulikoni? utawasikia," eeh eeh Mafuta na foleni Mkuu".
Eebo!
Ulichoongea ni kweli lakini hivi una muda gani toka utoke majuu/mamtoni maana hata daladala huwezi kuitamka!
 
Back
Top Bottom