Ufisadi serikalini, (cag, polisi, ikulu, takukuru) mahakamani na bungeni; nini kitatokea?

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Mihimili yote mitatu ya dola imetuhumiwa na Imani ya wanachi imekwisha.

A) SERIKALINI
-CAG ndo mkaguzi wa mahesabu ya Serikali. Ndo anayekagua kila kila idara na halmashauri zotte. Sasa naye ameguswa na Ufisadi kwa mujibu wa kamati ya Jairo.
-Polisi ndo walinzi wa watanzania, lakini kwa mujibu wa taarifa ya LHRC idadi ya watanzania waliokufa ktk mikono ya polisi vifo vyenye utata (polisi ambao wanapaswa kuwa walinzi wao) kwa mwaka 2010 ni zaidi 100 ( nimesahau kiasi kamili).
Pili Arusha na kwingineko polisi wanadaiwa kuwabeba ccm- Hawaaminiki.
-Ikulu ndo kichwa cha nchi, Nyerere alisema ni mahali ‘patakatifu’ lakini katibu mkuu kiongozi ambaye ndo katibu wa Mwenye ikulu, katibu wa Rais wa nchi, naye analinda mafisadi – nao ( yeye na Rais) hawaaminiki.
-Takukuru ni taasisi ya kupambana na Rushwa, Kamati ya Mwakyembe ikatuambia ilisaficha Rushwa ya Richmond. Hosea bado yupo = haiaminiki.

B) Makama ndo inategemewa kuwa waamuzi wa haki. Lakini Jaji mkuu mstaafu wa Tanzania ( Agustino Ramadhan) akiwa na majaji wenzake 6 walishindwa kuwatendea haki watz kwa kutoa hukumu ya kuzuia mgombea binafsi. Mahakama nayo inaendeshwa kwa shinikizo la Serikali iliyokwishaoza.
Maamuzi ya mahakama kuzima mgomo wa walimu kwa njia tata miaka kadhaa nyuma nayo ni kizungumkuti kingine. Imani ya wananchi imepungua.

C) Bunge ndo linaendeshwa kama Halmashauri kuu ya ccm. Ndo limepitisha mswada wa mabadililiko ya katiba ambao ndg Ulimwengu aliuita mswada wa kuchekesha. Mswada uliopingwa na wasomi, wanaharakati na wapinzani. Serikali na ccm wakaupitisha. Imani ya wananchi imepungua. Imebaki kwa Chadema ambao idadi yao ni ndogo hawawezi kuzuia maamuzi ya msingi.

Baada ya kuona hayo huko mbele tutarajie nini?
Je, watz wameshakosa imani ktk mihimili yote ya dola nini kitatokea mbeleni? Au watz wafanye nini?
Wasomi, wanaharakati na wapinzani tufanye nini ili kuikoa nchi yetu isiende ktk balaa hii linalonyemelea nchi yetu?
Katiba ni jibu la yote. Tutarejesheje mchakato wa katiba mpya ktk mstari sahihi? Tufanye nini ili kuepusha vurugu? Tupateje katibu mpya ambayo ndo suluhisho kwa amani?

Mimi najiuliza maswali haya, naamini nanyi mnajiuliza maswali kama haya.
 
Back
Top Bottom