Ufisadi Sekta ya Afya umechangia matatizo yanayojitokeza hivi sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi Sekta ya Afya umechangia matatizo yanayojitokeza hivi sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 11, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  Mgomo wa pili wa madaktari uliotangazwa na kutekelezwa Jumatano wiki hii, na kuwasababishia usumbufu mkubwa wagonjwa hospitalini, sasa umesitishwa rasmi na madaktari hao kwa kile walichoeleza ni kuheshimu ahadi ya Rais Jakaya Kikwete kuwa wampe muda afanyie kazi madai yao.
  Hizi ni habari njema kwa Watanzania na wale wote wenye mapenzi mema na uhai wa Taifa letu, ijapokuwa migomo hii tayari imewaathiri watu wengi na hasa wagonjwa wanaowategemea kuwaokoa. Hatujui ni namna gani watawaomba radhi walioteswa na migomo hii.
  Ni mgomo ambao kwa hakika umewaacha midomo wazi Watanzania wengi, hasa ikizingatiwa kwamba walishakubaliana na serikali kuhusu madai yao na kilichokuwa kinasubiriwa ni utekelezaji. Hata watu wengi waliohojiwa walionyesha kupingana na madaktari kwamba haikuwa haki kutesa wagonjwa.
  Baada ya mgomo wa kwanza uliotikisa kwa takriban wiki tatu, madaktari na serikali walikaa pamoja na kusikiliza madai husika na serikali kupitia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyekaa nao akakubali madai yote nane ikiwa ni pamoja na kuwajibishwa Katibu Mkuu wizara ya Afya, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa serikali, Dk. Deo Mtasiwa, nyongeza ya mishahara, vifaa vya kazi, nyumba na mikopo ya magari. Madai yote ya madaktari hawa yalikubaliwa na kilichokuwa kinasubiriwa sasa ni utaratibu wa kuanza kuyashughulikia kulingana na uwezo uliopo kwani mengine itabidi yasubiri bajeti ya serikali Juni mwaka huu.
  Hata Rais Jakaya Kikwete wakati akizungumza kwenye hotuba ya mwisho wa mwezi uliopita, alisisitiza; “Nathamini sana mchango wanaoutoa madaktari wetu katika kudumisha afya za wananchi. Aidha narudia kutoa pole za dhati kwa wananchi na hasa wagonjwa waliokuwa mahospitalini wakachukuliwa kwa mateso waliyopata kwa mgomo huo. Ni matumaini yangu kuwa hali kama ile haitajirudia tena”.
  Wiki moja tu baada ya Rais kutoa rai hii, madaktari wakatangaza mgomo huu wa pili na kusema utakuwa wa kihistoria. Ni mgomo uliokuwa ukifanyika wakati hata ule wa kwanza, machungu yake yalikuwa hayajatoweka akilini mwa Watanzania kutokana na jinsi ulivyoitetemesha nchi na kuumiza wengi vikiwemo vifo.
  Madaktari hawa wakaja na shinikizo la kufukuzwa au kujiuzulu kwa Waziri wa Afya Dk.Haji Mponda na naibu wake, Dk. Lucy Nkya. Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwaambia kuwa kumlazimisha Rais afanye hivyo haikubaliki. Swali ni je, hivi viongozi hawa wawili ndio waliosababisha matatizo katika sekta ya afya? Mbona matatizo ya sekta hiyo ni ya muda mrefu?
  Kama kweli madaktari wetu wametangaza kurejea kazini kuanzia leo, hali hiyo idhihirike kwa kuonekana wakichapa kazi na siyo kufanya usanii wa kuripoti kisha wanaweka mikono mifukoni. Tangu kuanza kwa mgomo wa kwanza na kisha huu wa pili, serikali imeonyesha jitihada kubwa kujaribu kufikia makubaliano.
  Kwa hili tunaipongeza sana. Na kusema ukweli kilichokuwa kinasuburiwa ni namna ya kuyafanyia kazi madai yale, hivyo haikuwa busara tena kwa mgomo mwingine kujitokeza, tena muda mfupi baada ya makubaliano yale kufikiwa huku majadiliano yakiendelea.
  Na hii ndiyo inayoleta shaka kwamba labda lilikuwepo jambo la ziada nyuma ya mgomo huo ambalo serikali hailifahamu. Madai yale ni ya msingi na hakuna anayepingana nayo.
  Lakini pia madaktari wetu wangewatizama zaidi wananchi wanaowategemea katika kuokoa maisha yao na kuwahurumia kwa mujibu wa kiapo na maadili ya kazi yao. Ni muhimu sana kwa taaluma zetu nyeti kama hii ya madaktari zitizamwe kwa macho mawili na kuangalia changamoto zilizopo, matatizo yaliyopo na kutafuta majawabu kabla ya madhara kujitokeza.
  Sekta ya afya imegubikwa pia na ufisadi. Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali, katika mwaka wa fedha unaoishia Juni, 2010 aligundua kiasi cha sh 1,895,253,371 kililipwa kwa wazabuni kabla ya kupokea vifaa. Na ukaguzi uliofanyika katika idara za Wizara umebaini vifaa vya thamani ya sh.1,648,407,271 vilikuwa havijafika.
  Kanuni 198 ya sheria ya fedha za umma ya mwaka 2001 inasema kwamba vifaa vyote vilivyonunuliwa lazima viandikwe kwenye daftari la vifaa. Kinyume na kanuni hii Wizara haikuandika kwenye daftari vifaa vya thamani ya sh 148,293,950. Kwa mantiki hiyo, matatizo mengi yamekuwepo siku nyingi katika sekta hiyo siyo kwamba yamesababishwa na Dk. Mponda na Nkya hivyo waondoke ndipo hali iwe ahueni.
  Huku ni kuwaonea kabisa kwani hata wao wameyakuta. Hata wakati Rais JK anaingia madarakani, alikuta matatizo na hadi sasa yapo aliyoweza kuyapatia ufumbuzi na mengine anaendelea nayo.
  Hivyo madaktari wetu wavute subira wakati serikali ikijipanga kushughulikia dai moja hadi lingine kulingana na uwezo uliopo. Serikali nayo ipambane na ufisadi wizarani humo kwani ni sehemu ya chanzo cha matatizo yanayochipua migomo hii.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  kuna kijana namjua kafanya kazi wizara ya afya 3yrs only kama muhasibu sasa kaacha kazi ana pesa za kubeba kwa magunia
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  nani aliyewaambia serikali kupitia pinda ilikaa na madaktari baada ya mgomo wa kwanza?
  Kwa hiyo hawa mawaziri walipoteuliwa walitegemea kukuta wizara ya afya ikiwa safi bila matatizo?
  Huyu mwandishi anaposema matatizo ya madaktari yanashughulikiwa ana ushahidi wa hilo?kuna mpango kazi wowote wa kushughulikia suala hili?
  Nadhani hatujaisoma taarifa ya madaktari na kuielewa,kwa ufupi mgomo haujaisha kwani serikali haijashughulikia suala lolote katika madai ya madaktari.hata kusimamishwa kwa nyoni na mtasiwa kulitokana na ufisadi na sio shinikizo la madaktari.kuhusu kupandishwa call allowance,kukopeshwa magari,green cards na chanjo ya hepatitis ...yote haya hayajatolewa waraka wa utekelezaji.waraka wa kupandishwa kwa call allowance umepelekwa wizara ya afya kitoka utumishi lakini mpaka leo haujawafikia ma RMO au ma DMO ambao kimsingi ndio watekelezaji,nani ameukalia kama sio hawa mawaziri.ndio maana madaktari hawawataki hawa wawili kwani hata makubaliano yakifikiwa mawaziri hawa hawatatekeleza.
  Naamini bado kuna mgomo mkubwa unakuja iwapo jk atawakumbatia mawaziri walioshindwa.
   
Loading...