Ufisadi Ngono kwenye mashindano ya Miss Tanzania

Je, Mashindano ya Miss Tanzania yafutwe?


  • Total voters
    28
  • Poll closed .

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
Waungwana,

Kuna mtu fulani aliniambia yafuatayo kuhusu mashindano ya ulimbwende ya Miss Tanzania.

1) Mashindano haya yanapokaribia kufikia hatua za mwisho yaani kabla ya kuingia Kambi Kuu, picha za walimbwende hao ambazo huwa zimepigwa katika hatua mbali mbali, hukusanywa na kuwekwa kwenye kitabu (catalogue) ambacho hutumwa kwa njia ya mtandao (Internet) kwa wateja ambao wako nje ya nchi.

2) Wateja hawa, kwa kiwango kikubwa, ni wazungu wenye uchu wa kuja kustarehe na hawa dada zetu, kwa malipo ya bei mbaya, ambayo huwa yanalipwa kabla ya wateja hawa kuingia nchini, wakiwa tayari wamekwishafanya "booking" ya kuchagua walimbwende watakaostarehe nao, wakati wakiwa "kambini" hoteli ya White Sands (ila mwaka jana, kama sikosei, kambi ilikuwa Paradise Resort ya Bagamoyo... ile iliyoungua/iliyounguzwa/iliyochomwa moto.....)

3) Wengi wa walimbwende ambao hulazimishwa (na hapa tunazungumzia suala la human trafficking au sexual slavery) kufanya vitendo vya ngono na wateja hawa kutoka ughaibuni pasi na wao kujipatia hata senti moja. Kila mshiriki anayeingia kwenye hatua hii ya mwisho hula kiapo cha kutotoa siri ya nini kinachotokea wakiwa "kambini", huku wakitishwa kama, iwapo watatoa siri, madhara makubwa yanaweza kuwafikia. Jambo hili limefanya ushahidi wa kina kuhusu ufisadi ngono huu kutopatikana, kwa kuwa, mpaka leo, hakuna mlimbwende hata mmoja aliyeweza kupata ujasiri wa kujitokeza na kuelezea yanayotokea.

Mimi ninauliza,

1) Kama haya ni kweli, je, kuna faida gani ya dada zetu kushiriki kwenye mashindano haya ambayo yanaonekana kuwa kichocheo cha maambukizi ya UKIMWI pamoja na magonjwa mengine ya zinaa?

2) Kama haya ni kweli, ile Sheria ya Sexual Offences Special Provisions Act (SOSPA) ya mwaka 2002, inafanya nini, isiwabane hao wanaoendesha ufisadi ngono huu?

Mtu aliyenieleza taarifa hizi (ni msiri, kwa kanuni ya uandishi wa habari siwezi kumtaja na sitamtaja... hata nikipelekwa jela) aliniambia kwamba, mawakala wa ngazi ya mikoa na kanda huwa wanashirikishwa kuendesha "minada ya siri" ambapo watu wanaotaka dada zetu hawa waweze kufikishwa "kambi kuu" huwa wanaendesha mnada huo kwa njia ya SMS, ambapo huwa wanawapigia kura washiriki wanaowataka "washinde" na kufikia ngazi ya "kumi bora", ili wakifika kwenye kambi kuu waweze kupatikana kwa ajili ya wateja hao kutoka ughaibuni. Kimsingi, biashara hii chafu inatambulika kwa jina la "sex tourism" lakini jina halali kabisa ni "sex slavery" au "human trafficking".

Wana JF, nawaombeni mchango wenu:

1) Nini kifanyike?

2) Nani abanwe?

3) Hatua gani za kisheria zifanyike?

Lakini kabla hamjafikia uamuzi wowote, jaribuni kufanya tathmini iwapo mashindano haya (zaidi ya "kuwaharibu" dada zetu kama akina Irene Uwoya na Wema Sepetu, kwa mfano.... najua hapa nitaulizwa "wameharibiwa" kwa namna gani... jibu mnalo!) yameleta mchango wa aina gani kwenye jamii ya Watanzania. Binafsi, mchango mkubwa ninaouona ni kwamba yamechangia kwa kiwango kikubwa katika kuporomoka kwa maadili ya Kitanzania. Hapo awali, kabla ya Miss Tanzania kuanza kuendeshwa, ilikuwa nadra sana kuweza kuyaona mapaja au sehemu kubwa ya miili/maungo ya akina dada zetu hawa, zikiwa wazi bila kufunikwa. Kile kipengele cha "vazi la ufukweni" (Je, ni msichana gani wa Kitanzania huwa anavaa mavazi kama yale akiwa "ufukweni"?) kimekuwa kisingizio cha kuwatembeza nusu uchi akina dada zetu.

Nadhani imetosha sasa. Natoa hoja: MISS TANZANIA IFUTWE! TOO MUCH DAMAGE HAS BEEN DONE.

Wenye kuunga mkono waseme NDIO na wasiounga mkono waseme HAPANA.

./Mwana wa Haki
 
1. Udaku tu!!!

2. Ni watu wazima..hawalazimishwi chochote!

3. TV, internet pia huonyesha picha mbaya..je vipigwa marufuku Tz kama Saudia?

4. Kwa nini tu bango kwa Miss Tz???

5. Wengine wenye tabia nzuri..hata wameolewa: angalia Mke wa Lazaro Nyalandu!

6. Uhuni/umalaya ni tabia tu ya mtu!
 
Hakuna anaye walazimisha kuingia kwenye mashindano. Hakuna anaye walazimisha kugawa ngono. Hakuna kinacho wazuia kuondoka waki lazimishwa kitu ambacho hawakati kufanya. If you feel it's too much simply work away.
 
Hakuna anaye walazimisha kuingia kwenye mashindano. Hakuna anaye walazimisha kugawa ngono. Hakuna kinacho wazuia kuondoka waki lazimishwa kitu ambacho hawakati kufanya. If you feel it's too much simply work away.

Mkuu, wengu hawapendi ila mazingira yanawalazimisha, mfano umasikini na ule uwezekano wa kuwa 'tajiri' kwa kushinda miss tanzania!
 
Mkuu, wengu hawapendi ila mazingira yanawalazimisha, mfano umasikini na ule uwezekano wa kuwa 'tajiri' kwa kushinda miss tanzania!

Nakubali mkuu but they still have a choice. Wangapi maskini na hawauzi utu wala heshima yao? Ukweli una baki pale pale kwamba wameingia wenyewe kwa matakwa yao na wanaweza kutoka. Pia kuna mamiss wangapi tunawaona wana toka kwenye famili zinazo jiweza tu lakini bado wana fanya umalaya?
 
MwanaHaki
Umepiga pentagon
Mashindano haya yanadhalilisha sana dada zetu. Majaji na baadhi ya waratibu wa mashindano haya ndiyo agents wa ufisadi huu ndo maana inasadikika kwamba wengi wa wanaoshinda taji huwa washatembelewa vya kutosha na mapedeshee hasa wanaotoka makampuni yanayotoa ufadhili. Kuna walimbwende waliwahi kunimegea siri hii kwamba wanalazimika kuuvua utu wao ili wapate mradi. na kama ujuavyo dada zetu tamaa zinawaponza....

Ila hilo la kwenye intanet sina uhakika wala ushahidi nalo.
 
Shalom,

Hapa ntaongea kitu kimoja ambacho nadhani ni cha msingi sana ckabla hatujaingia ndani sana na mjadala huu na jinsi ambavyo hawa walimbwende wanadhalilishwa kama inavyodaiwa. Kabla ya kusema lolote inabidi tuangalie uhasilia wa tabia za wahusika wa mashindano kabla ya kujiingiza katika mashindano ya Umiss na mienendo ya tabia zao baada ya Mashindano.

Nimekuwa mdau wa mashindano haya ya ulimbwende, na hapa siongelei mashindano ya Miss Tanzania tu na katika miaka hiyo kitu ambacho nimekuja fahamu ni kwamba wengi wa Mabinti wa Kitanzania wanaojiingiza katika haya mashindano ni wale ambao wanatafuta urahisi wa maisha. Si kwamba hakuna ambao ni 'well to do' ambao wanaingia katika haya mashindano bali ni katika kusaka urahisi wa maisha, kusaka njia za mkato katika kufanikiwa katika maisha haya na majina ya haraka jamiini.

Tukisema wanalazimishwa ni kwamba tunakosea sana ila haya yote ambayo wanayafanya ni machaguzi ambayo wanakuwa nayo mara baada ya mashindano na baada ya ile dakika yao moja ya umaarufu kuyoyoma. Ukitembelea Hotel za Kitalii leo na maeneo mengine ya starehe utakutana nao wengi wakihangaika kujaribu kupata mabwana wenye pesa na hadhi, tena siku hizi limeibuka wimbi la wengi wa mabinti hawa kutafuta mabwana wa kizungu na sidhani kama kuna watu katika kamati hizo za mashindano ambao huwa wanahusika katika kuwatafutia. Asilimia kubwa ya mabinti hawa Ufuska na Kuuza Ngono ni jadi yao.

Sema tatizo kubwa lingine lililopo ambalo hapo moja kwa moja linahusiana na hizi kamati ni katika kutafuta udhamini. Hapa, kama ilivyo katika soko la ajira, rushwa ya ngono inatembezwa sana kwa hao mabosi wa makampuni ambayo yanajitolea kudhamini hayo mashindano ili kuhakikisha kwamba wafadhili hao hawapokonyoki. Hapa nadhani ndipo hizi Kamati za Mashindano ya Ulimbwende zinacheza kama viungo machachari kuhakikisha kwamba wanafanikisha malengo yao... Its so sad lakini ndio hali halisi. Wadhamini ni wadau wa kwanza katika kununua hao mabinti kupitia miadi ya kuhakikisha continuing support wa hizo events.
 
Mimi najua warembo wanagawiwa kwa mapeded'zhee wa hapa hapa bongo! Hilo nina uhakika nalo;
Mfano mzuri ni yule aliekuwa miss Mara kafanywa nyumba ndogo na Papaa Msofe Dar ilhali kwao Musoma kawaambia anasoma chuo kikuu!!! kahongwa ka RAV4 hivi short chesis.....
Wakiwa kambini hata wewe unaweza kuenda kujichagulia, ila unaweza kuambiwa huyu tayari kafanyiwa booking na Ridhwan, au fulani!
 
unajua uhuni ni hulka ya mtu,pili vishawishi navyo vinaweza kumfanya mtu akaacha tabia yake ya asili na kufuata mkumbo kwa hapa kwetu nafikiri tamaa ndizo zinazosababisha haya kwzewea walimbwende wetu ni hatari kwa fani, hawajui mambo mazuri hayataki haraka,mashindano yaendelee ila kanuni ziongezewe makali
 
Rushwa ya mapenzi kwa Tanzania ni kitu cha kawaida kila mahali , Hapa kwenye umiss inaonekana zaidi kwa sababu masikio,mawazo na macho ya watu walio wengi huwa inaelekezwa zaidi kwao kwani ni mabinti wenye kupendeza na kuvutia ki ngono,

Nenda kwenye Halmashauri/Munispal au kwenye makampuni binafsi na sehemu zingine zenye kutoa ajira, Ngono inafanyika zaidi hata kuliko ktk vipindi vya mashindano ya Umiss Tanzania.

Naliongelea hili kwasababu nina uhakika nalo.. Tunaweza kukemea endapo tutaweza kubadiri tabia zetu sisi wenyewe.

Baadhi ya wabunge, Mawaziri wengi pia hujihusisha na matendo machafu, Fuatilia wakati Bunge likiwa limekaa Dodoma,Utashangaa kuona Hotel zote mjini zimejazwa na mabinti wadogo na Mashangingi..Je nini wanafuata kule wakati wa kipindi cha Bunge ????
Inafika mahala tukubali kuridhika na mpenzi / Mke au mume mmoja. Haipendezi mbele ya jamii. Maumbile yetu hayakuwekwa kwa ajili ya kustareheshana..!!

Waziri wa Habari,michezo na tamaduni..PIGIA kelele wabunge na Mawaziri wenzio wawe mfano mzuri mbele ya wale wanao waongoza...!

WATANZANIA TUPUNGUZENI KULIWEKA TENDO LA NDOA MBELE KWANI LINATURUDISHA NYUMA KIMAENDELEO KWA NJIA MOJA AU NYINGINE.....!!
 
Consensual sex between adults, carry on.

Is it? How do u define consensual? How do you justify the presence of money exchange? Is that still consensual? Furthermore...Doesn't it become prostitution?(which is also illegal)
 
Mimi najua warembo wanagawiwa kwa mapeded'zhee wa hapa hapa bongo! Hilo nina uhakika nalo;
Mfano mzuri ni yule aliekuwa miss Mara kafanywa nyumba ndogo na Papaa Msofe Dar ilhali kwao Musoma kawaambia anasoma chuo kikuu!!! kahongwa ka RAV4 hivi short chesis.....
Wakiwa kambini hata wewe unaweza kuenda kujichagulia, ila unaweza kuambiwa huyu tayari kafanyiwa booking na Ridhwan, au fulani!
Jamani, jamani, jamani! Tutapona kweli? Eh Mola tunusuru!
 
Back
Top Bottom