Ufisadi ndio unaozungumziwa sana duniani


L

Leornado

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
1,534
Likes
20
Points
0
L

Leornado

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
1,534 20 0
Kura ya maoni ya kimataifa iliyofanywa na BBC imeashiria kuwa ufisadi miongoni mwa maafisa wa serikali ni mojawepo wa matatizo yanayozungumziwa sana duniani.
Uchunguzi huo umebaini kuwa hongo, ufisadi na ulafi miongoni mwa maafisa wa serikali ulijadiliwa sana miongoni mwa marafiki na watu wa familia moja kuliko swala la mabadiliko ya hali ya anga, umaskini, ukosefu wa ajira na hata ongezeko la bei ya vyakula na kawi.
Kura hiyo ya maoni ya BBC iliwahusisha watu alfu 13,000 kutoka mataifa 26. Asilimia 21-takriban mtu mmoja kati ya watano waliohojiwa- walisema wamejadili maswala kuhusu ufisadi na ulafi na marafiki au watu wa jamii yao katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
091209105220_unjukrasa106_60.jpg
Maadhimisho ya siku ya ufisadi duniani mjini Jarkata, Indonesia.


Hali hiyo imefanya ufisadi kuwa tatizo la dunia linalozungumziwa sana. Swali tofauti lililoulizwa na BBC liliwataka watu kukadiria ni maswala gani waliozingatia kuwa yenye umuhimu mkubwa yanayopaswa kushughulikiwa kwa dharura.
Ufisadi ulishika nafasi ya pili kama mada yenye umuhimu mkubwa baada ya umaskini.
Wale waliohojiwa nchini Brazil, Misri, Colombia, Ufilipino na Kenya walizingatia zaidi ufisadi kuwa ndio tatizo kubwa duniani.
Barani Ulaya, raia wa Italia ndio waliolezea zaidi wasiwasi wao kuhusu ulaji rushwa.
Uchapishaji wa matokeo ya utafiti huo wa BBC unasadifiana na maadhimisho ya siku ya ufisadi duniani inayoongoozwa na Umoja wa Mataifa leo Alhamisi.
 
L

Leornado

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
1,534
Likes
20
Points
0
L

Leornado

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
1,534 20 0
Mafisadi mpoo, kazi kwenu
 
Rungu

Rungu

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2007
Messages
3,905
Likes
1,049
Points
280
Age
68
Rungu

Rungu

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2007
3,905 1,049 280
Tupoo, mwanawane!
 

Forum statistics

Threads 1,205,604
Members 457,997
Posts 28,199,503