Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 5,321
- 11,410
Ni hadithi ya wazazi ambao walikuwa wanalala na watoto wao wadogo wawili katika kitanda kimoja.
Ilipokuwa inafika usiku na wazazi wakiamini watoto wamelala wakawa wanafanya tendo la ndoa. Bahati mbaya katika kufurahia jambo lao wakamwangusha yule mdogo chini.
Akalia...akabembelezwa na kurudi kulala. Kaka yake aliumizWa sana na kitendo hicho. Wazazi wakasubiria baada ya dk chache wakaamini watoto wamelala.
Wakaanza tena kufanya tendo la ndoa kwa fujo za raha zao.ndipo mkubwa akapiga kelele akimwambia mdogo"Juma jishikilie vizuri wameanza tena"
Hizi gharama za matengenezo ya hii nyumba angekuwepo marehemu Dr. John P.Magufuli kweli zingekuwa hivi?
Watanzania tunapaswa kujishikilia vizuri wezi wameanza tena. Hii nyumba kweli ya mili 500+? Kweli ndugu zanguni?
Hii nyumba kuna hesabu za kekundu keuzi zimefanyika kipindi hiki ambacho hakuna wa Kukemea kuna watu wanaongeza hesabu juu kwa juu. Angekuwepo Magufuli wasingefikisha hiyo pesa. Kuna uwezekano baada ya mwezi amefariki watu wakakaa wakaandika upya gharama na kugawa cha juu.
Sikuwahi kuwa fan wa Magufuli na mnaweza angalia threads zangu za kale. Ila huwa napenda kusimamia ukweli na ninachokiamini. Mama Samia usiruhusu Ufisadi urudi tena.tunakuomba. hawa wanakujaribu. Wakiona unacheka nao wananchi tutakuja juta.