Ufisadi: Nani msafi kati ya Lowassa na Dr Magufuli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi: Nani msafi kati ya Lowassa na Dr Magufuli?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mge, Sep 5, 2015.

 1. m

  mge JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2015
  Joined: Dec 19, 2013
  Messages: 549
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Rais wetu pamoja na sifa zingine lakini sifa ya msingi ni lazima awe msafi asiwe na mali zisizo na maelezo. Yupi kati ya hao ataweza kupambana na ufisadi?
   
 2. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2015
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,571
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Sasa katika hali hii, nikiangalia wagombea wawili wa urais, yaani Magufuli na Lowassa, naona kuwa tafsiri ya kauli za Dr. Slaa ni kuwa UKAWA wamemtoa Lowassa chooni, lakini Magufuli ameng'ang'ania kubaki chooni. Ningekuwa mpiga kura, kura yangu ningempa huyu Lowassa aliyelopolewa kutoka chooni kuliko huyu Magufuli ambaye amepania kufia humo chooni.
   
 3. m

  marcusgarvey JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2015
  Joined: Aug 16, 2015
  Messages: 891
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Acheni uvivu,Kasomeni report ya prof Assad ndo mtamjua vema huyo jpm
   
 4. M

  Mnasihi JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2015
  Joined: Oct 9, 2013
  Messages: 4,030
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Msafi ni EL kwani mali zake ni ng'ombe wa urithi. Huyo mwingine hatowea kupambana na kuuundia mahakama mfumo uliomlea na kumuweka madarakani. Anadanganya mchana kweupe akishirikiana na Slaa.
  Tatizo la ccm ni lile la kutudharau, kututukana na kutuibia rasilimali zetu. Wanafikiri wapiga kura wa 2010 ndio hawa wa sasa. Tumewachoka mno, hata Slaa mliyemtuma kuwasemea kakiri. Fanyeni yoote ila Lowasa ndio rais wenu.
   
 5. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2015
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,571
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Hapa nimeweka Kashfa za Magufuli naomba na wewe weka za Lowasa tusiishie kuropoka tu.

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/711820-serikali-yashindwa-kesi-na-wachina-walioshtakiwa-kwa-uvuvi-haramu.html

  [​IMG] Dr. Slaa: Nikiwa Rais nitamtia Magufuli ndani kwa kuuza nyumba za Serikali

  Dr. Slaa akihojiwa na Radio five ya Arusha jioni hii nini maoni yake kuhusu uteuzi wa Magufuli kuwania Urais.

  Ameongelea mengi lakini amesema iwapo UKAWA wakimpa nafasi na Watanzania wakampa kura za kutosha kushinda Urais atamtia Magufuri ndani ili kujibu tuhuma za uuzwaji wa Nyumba kwa bei ya kutupa.

  Chanzo: Radio five, Arusha  • Monday, May 25, 2015

   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI WA FEDHA ZA SERIKALI 2013/2014 TANZANIA   [​IMG]


   Mohamedi Mtoi Kanyawana


   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI WA FEDHA ZA SERIKALI 2013/2014

   · Upotevu wa shilingi trilioni 1.151 Serikali kuu pekee hauvumiliki.

   · Makusanyo yote yaliyotokana na kuongezeka kwa kodi 2013/14 yameyeyuka.

   Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ufisadi wa kutisha uliofanyika kwenye matumizi ya fedha za umma kama ilivyobainishwa
   kwenye ripoti za ukaguzi wa fedha kwa mwaka 2013/2014 zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

   Wakati chama kinaendelea kuzifanyia uchambuzi wa kina ripoti zote tano ili kuweka hadharani ubadhirifu mkubwa ambao mwingi hujificha kwenye maelezo ya kitaalam, tunapenda kutoa taarifa ya awali kama ifuatavyo;

   · Wizara tatu , Trilioni 1.151 zimepotea

   Katika uchambuzi wetu wa awali tumebaini kuwa kwa upande wa serikali kuu pekee zaidi ya shilingi trilioni 1.151zimepotea au kuliwa na wajanja walioko serikalini , kiwangio hiki ni sawa naasilimia 5.231 ya bajeti yote ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha 2015/16 inayoendelea kujadiliwa huko Bungeni Dodoma.

   Ripoti ya CAG iliyotolewa jana inaonyesha kuwa katika Serikali Kuu, Wizara tatu tu ambazo tumezifanyia Uchambuzi mpaka sasa zimepotea kiasi cha shilingi 1.151 Trilioni , wizara hizo ni;

   i. Wizara ya Fedha (TRA) , Fedha zilizopotea kutokana na bidhaa ambazo zilipaswa kuuzwa nje ya Nchi ila kutokana na uzembe zikauzwa ndani ya nchi bila kulipiwa kodi zilikuwa jumla ya shilingi 836 Bilioni.

   ii. Ofisi ya Waziri Mkuu , kitengo kimoja cha maafa zilipotea jumla ya shilingi 163 Bilioni.

   iii. Wizara ya Ujenzi , ziliibwa jumla ya shilingi 252 Bilioni.   · Bajeti ya mwaka 2013/14 Mapato yote ya ongezeko la kodi yameyeyuka:

   Mwaka 2013/14 yalifanyika maboresho ya sheria mbalimbali za kodi wakati wa Bunge la bajeti kodi ambazo kimsingi zilimwongezea mwananchi mzigo mzito wa kulipia kodi hizo kwa ajili ya kuongeza mapato ya Serikali na ili kuiwezesha serikali kuwahudumia wananchi wake .

   Pamoja na ongezeko hilo la kodi ,ukweli mchungu ni kuwa fedha yote iliyokusanywa kutokana na ongezeko la kodi mbalimbali katika mwaka wa fedha 2013/14 imepotea yote katika wizara tatu tu za serikali kutokana na vitendo vya kifisadi, na hii ni kwa mujibu wa taarifa CAG .

   Kodi zilizorekebishwa na mapato yake ni kama ifuatavyo;

   a. Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148; kilipatikana kiasi cha sh.48.977bilioni

   b. Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332;kilipatikana kiasi shilingi 131.686 bilioni

   c. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147; kilipatikana kiasi cha shilingi510.017 bilioni

   d. Sheria ya Ushuru wa Mafuta, SURA, 220; kilipatikana kiasi cha shilingi155.893bilioni

   e. Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82 ;kilipatikana kiasi cha shilingi 28.213 bilioni

   f. Sheria ya Usalama Barabarani, SURA, 168; kilipatikana kiasi cha shilingi 19.710 bilioni

   g. Sheria ya Petroli (Petroleum Act) SURA, 392;kilipatikana kiasi cha shilingi123.725 bilioni   Hali hiyo ilifanya marekebisho yote ya sheria za Kodi zilizofanywa katika mwaka huo wa fedha kuiwezesha serikali kukusanya jumla ya shilingi 1.018 Trilioni katika mwaka wa Fedha 2013/2014 na hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Hansard ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

   Hali hii haikubaliki na haivumiliki hata kidogo. Hapa tumezungumzia Wizara tatu tu za serikali kuu bado wizara 30 na idara mbalimbali za Serikali ikiwa ni pamoja na Halmashauri na Taasisi na Mashirika ya Umma.

   Ripoti hizi zimezidi kudhihirisha kwa mara nyingine kuwa matatizo yanayowakabili Watanzania ikiwa ni pamoja na umaskini, maradhi, ujinga yanaendelea kudumu kwa sababu watawala wa Serikali ya CCM wameamua yaendelee kuwepo kwa kukumbatia adui wa nne ambaye ni ufisadi.

   Ripoti hizo za CAG ambazo zimeanika ufisadi katika maeneo yaliyokaguliwa ikiwemo Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, mashirika ya umma na miradi ya maendeleo, kwa mara nyingine zimedhihirisha wazi kile ambacho CHADEMA kimekuwa kikisema kwa muda mrefu kwamba ufisadi huu unaoendelea kulitafuna taifa na kuwafanya Watanzania wazidi kuwa maskini ni matokeo ya kushindwa kwa sera, mikakati na mipango ya CCM.

   Wakati kasi ya ufisadi inaongezeka kutoka mwaka hadi mwaka kwenye Serikali ya Rais Jakaya Kikwete chini ya usimamizi wa CCM, ndivyo serikali hiyo hiyo inaongeza kasi ya kushindwa kusimamia UWAJIBIKAJI ambayo ndiyo moja ya nguzo muhimu katika kuhakikisha matumizi ya fedha za umma yanaonekana katika kuboresha maisha ya wananchi hususan kuweka fursa za kujitafutia maendeleo ya mtu mmoja mmoja na hatimaye ustawi wa jamii nzima.

   Ufisadi huu hauvumiliki tena. Watanzania wasikubali kuendelea kubeba mizigo ya watawala walioshindwa kutekeleza wajibu wao. Hali ya siasa inazingirwa na sintofahamu kubwa. Uchumi unazidi kuyumba. Kijamii, maisha yazidi kuwa magumu na walioko madarakani wamelewa madaraka. Msamiati wa UWAJIBIKAJI haumo vichwani mwao tena.

   Ni mwaka wa Watanzania kuamua kuachana na ufisadi huu.

   Imetolewa leo Jumatano, 20 Mei, 2015
  Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

  Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
  -Apuuza maonyo ya wataalamu
  -Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani


  ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

  Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

  Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

  Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

  Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

  Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

  “Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

  Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

  “Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

  Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

  Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

  Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

  Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

  Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

  Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

  Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

  Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

  Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

  Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

  Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

  Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

  Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

  Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

  “Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

  Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

  Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

  Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.


   
 6. m

  mkezwag JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2015
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 3,245
  Likes Received: 499
  Trophy Points: 180
  Mkuu ni kweli Tanzania na watanzania ni watu wa ajabu Kabisa.yaani Karne hii watu bado wanategemea mtu badala ya system?wananchi Hawa wa ajabu wa Tanzania walitaka kuondokana na huu utamaduni wa kutegemea watu kwa kutengeneza system kupitia rasmu ya pili ya tume ya mabadiriko ya katiba,ccm chini ya uenyekiti wa six na samia wakaufutilia mbali.
   
 7. m

  mkezwag JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2015
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 3,245
  Likes Received: 499
  Trophy Points: 180
  hii ndiyo ccm yaani choo kwa mujibu wa slaa
   
 8. Dr. Ngwazi

  Dr. Ngwazi JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2015
  Joined: Jul 30, 2015
  Messages: 708
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60

  mvivu ni wewe unayekimbilia tafiti za wenzako. swali ni rahisi tu, halihitaji huo utafiti wa huyo prof wako maana hata wale wapiga kura wa kule kwetu ngopyolo huyo prof hawamjui
   
 9. m

  marcusgarvey JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2015
  Joined: Aug 16, 2015
  Messages: 891
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dawa imekuingia
   
 10. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2017
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,983
  Likes Received: 3,521
  Trophy Points: 280
  Bongo Dar es Salaam!
   
 11. Azarel

  Azarel JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2017
  Joined: Aug 25, 2016
  Messages: 11,351
  Likes Received: 11,787
  Trophy Points: 280
  Mimi sijui ila nachojua E.N. Lowassa ni msafi na alisingiziwa mengi.
   
 12. B

  Bazilio JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2017
  Joined: Apr 1, 2017
  Messages: 632
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 80
  Ndoto ya mchana kumg'amua lowasa kama walomsema miaka 9 kaweza kuwatia mfukoni sembuse zumbukuku wengine
   
 13. barafuyamoto

  barafuyamoto JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2017
  Joined: Jul 26, 2014
  Messages: 23,612
  Likes Received: 15,712
  Trophy Points: 280
  Alisingiziwa na nani??
   
Loading...