Ufisadi mwingine Kilimo Kwanza!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi mwingine Kilimo Kwanza!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 7, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,480
  Likes Received: 81,771
  Trophy Points: 280
  Manji akiri kukosa 'dili' la Kilimo KwanzaImeandikwa na Mwandishi Wetu;
  7th October 2009

  Habari Leo

  MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yusuf Manji, amekiri kushindwa katika mchakato wa zabuni ya kusambaza matrekta yenye thamani ya Sh bilioni 50.

  Mmiliki huyo wa kampuni ya Quality Group, amesema, mchakato huo ulifanywa kwa kuzingatia haki hivyo hana kinyongo. Manji ametoa msimamo huo leo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

  Kwa mujibu wa Manji, kwa kuzingatia mchakato huo, mfanyabaiashara mwenzake, Jayanthkumar Chandrubhai Patel 'Jeetu Patel' ana haki ya kushinda zabuni hiyo.

  Katika taarifa hiyo, Manji amekiri kuwa ni kweli kampuni yake iliomba zabuni hiyo na imeshindwa.

  Hata hivyo mfanyabiashara huyo amekanusha kutishia kuanika uovu wa kampuni iliyoshinda zabuni hiyo, gazeti la Tanzania Daima lilidai hivyo.

  Katika gazeti hilo, ilidaiwa kuwa Manji hakufurahishwa na namna mchakato ulivyoendeshwa, na kuwa alikuwa anajiandaa kuanika uovu wa kampuni ya Jeetu Patel.

  "Napenda kusema kinagaubaga, kuwa kampuni zilizo chini ya usimamizi wangu zinafuata maadili, zinazingatia kanuni za kibiashara kwa kiwango cha juu kitaaluma.

  "Hii si mara ya kwanza tunashiriki katika kuwania zabuni za Serikali na si mara ya kwanza pia tunashindwa kuzipata, tunaelewa kuwa zipo taratibu za kisheria za kufuata kama mtu hakuridhika na mchakato mzima... katika hili hatuna ushahidi wa uhakika kuonesha kuwa hatukutendewa haki, hivyo tumeridhika," amesema Manji katika taarifa hiyo.

  Serikali ilitangaza zabuni ya kusambaza matrekta hayo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wake wa Kilimo Kwanza kutokana na makubaliano ya mkopo usio na riba kutoka India wa zaidi ya Sh bilioni 50.

  Makubaliano hayo yaliyofikiwa katika ziara ya Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein, nchini humo mapema mwaka huu
  .
   
 2. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hivi vyombo vyetu vya kiutendaji vitajifunza lini katika kufanya maamuzi yenye faida kwa Taifa lao mimi naona kama vile ufisadi huu hauwezi kwisha kama hata wale ambao wana kesi za ufisadi mahakamani wanaendelea kupewa zabuni za kuendeleza mikakati ya kufufua uchumi wetu kwa mfano hili la KILIMO KWANZA. Hii ni aibu na fedheha kwa wale wote walioshughulikia zabuni hii na kwa serikali nzima kama wanaamini wanaweza kukuza uchumi kwa kuwatumia mafisadi na kampuni zao.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,480
  Likes Received: 81,771
  Trophy Points: 280
  Yaani! Nimechoka kabisa! Huyu ni mtuhumiwa wa ufisadi halafu wanaenda kumpa deal nyingine tena kubwa sana! Sijui hata hiyo zabuni ilitangazwa lini na ni nani waliokuwa waamuzi wa nani anayestahili kupewa zabuni hiyo! Uongozi wa nchi yetu yaani umeoza kabisa!
   
 4. K

  Koba JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Kweli sielewi jinsi serikali yetu inavyofanya kazi,hivi kuna mtu anaamini kweli hayo matrekta yatawafikia wakulima kwa huo utaratibu? hii ni michezo tuu na hizo billions zitaishia tuu kama umeme wa Richmond!
   
 5. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 779
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 80
  Ni kweli unayosema lakini kwa sababu kuna uchaguzi mwakani na kikwete ili asionekane hajafanya kitu hayo matrekta mzee yatakuja na utayaona amini usiamini! ni kama zawadi za khanga na pilau kwenye chaguzi
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,480
  Likes Received: 81,771
  Trophy Points: 280
  Manji, Jeetu wagombea matrekta

  • Homa ya Kilimo Kwanza

  na Mwandishi Wetu
  Tamzani Daima


  WAFANYABIASHARA wawili maarufu hapa nchini wenye asili ya Kiasia, Yusuf Manji na Jayantkumar Chandubhai Patel, maarufu kwa jina la Jeetu Patel, wanadaiwa kuingia katika mzozo mkubwa wa kibiashara wakati wakigombea kupata zabuni ya mradi wa kuingiza nchini na kusambaza matrekta, wenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 50.

  Habari ambazo Tanzania Daima Jumatano limezipata kutoka vyanzo vyake vya habari vya kuaminika zimeeleza kuwa, Manji na Patel ambao wanadaiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kuomba zabuni hiyo, sasa wanawindana huku wakitishana kumalizana kibiashara.

  Baadhi ya watu wa karibu na wafanyabiashara hao mabilionea waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti katika siku za karibuni walieleza kuwa, kumekuwa na jitihada za chini kwa chini zinazofanywa na wapambe wao kuvujisha katika vyombo vya habari mbinu zao wanazotumia kupata zabuni kubwa za serikali.

  Mfanyabiashara mmoja maarufu ambaye yuko karibu na wafanyabiashara hao, alilieleza gazeti hili kuwa, mabilionea hao sasa wamekuwa mahasimu baada ya kuzidiana ujanja katika zabuni hiyo ambapo kila mmoja anatishia kutoa siri za kibiashara za mwenzake.

  “Sasa wanatishana, kila mmoja anatishia kutoa siri za mwenzake kibiashara. Wote wanapata tenda kubwa kutoka serikalini, wanavyozipata wanajua wao. Kinachotushangaza kila mmoja anasema atamuanika mwenzake,” alisema mfanyabiashara huyo aliyeomba jina lake lisitajwe.

  Taarifa za ndani kutoka kwa watu walio karibu na Manji, zinadai kuwa mfanyabiashara huyo hakufurahishwa na jinsi mchakato wa upatikanaji zabuni hiyo ulivyoendeshwa, na sasa anakusudia kuvujisha katika vyombo vya habari taratibu zilizokiukwa katika mchakato wa utoaji wa zabuni hiyo.

  Zinadai kuwa, Manji anajiandaa kuweka wazi jinsi sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004 ilivyokiukwa wakati wa mchakato wa utoaji zabuni hiyo.

  Katika mradi huo, Jeetu ambaye anatajwa kuwa mwakilishi wa Kampuni ya Escort hapa nchini, yenye makao makuu yake nchini India, ambayo imeshinda zabuni hiyo, anadaiwa kuwashawishi maofisa wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambalo limekabidhiwa jukumu la kuutekeleza mradi huo na serikali, kuipatia kampuni hiyo.

  Habari hizo zimedai kuwa, Jeetu alifanikisha mpango huo baada ya kuwaunganisha maofisa kadhaa wa ngazi za juu wa JKT na watendaji wakuu wa Escort walioko India, ambao baada ya kuhakikishiwa kupewa zabuni hiyo, waliwaalika maofisa kadhaa wa JKT kwenda nchini humo kwa ajili ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa kazi ya kusambaza matrekta hapa nchini.

  Taarifa zaidi zilidai kuwa, tayari baadhi ya viongozi wa juu wa JKT wamekwisha safiri hadi India kusaini mkataba huo.

  Hata hivyo, inadaiwa kuwa, Manji anapinga hatua ya viongozi wa JKT kwenda kusaini mkataba huo nchini India, ikizingatiwa kuwa baadhi ya watendaji wa serikali wamekwishalalamikiwa kwa kusaini mikataba inayohusu miradi ya kitaifa nje ya nchi.

  Aidha, inadaiwa kuwa, baadhi ya habari zinazotarajiwa kusambazwa zitakuwa zinahoji ukiukwaji wa taratibu kwa kutoa zabuni hiyo pasipo kuitangaza kama sheria ya manunuzi ya umma inavyoelekeza, licha ya Baraza la Mawaziri kuujadili mradi huo na kutoa baraka kwa JKT kuutekeleza.

  Kwa upande wa Jeetu, taarifa zinadai kuwa, anajiandaa kujibu tuhuma za aina yoyote zitakazotolewa katika vyombo vya habari, zikiwa na lengo la kuichafua Kampuni ya Escort au zinazohusu upatikanaji wa zabuni hiyo.

  Baadhi ya maofisa wa serikali waliozungumza na Tanzania Daima Jumatano kuhusu suala hilo walieleza kuwa, serikali ina taarifa kuhusu jambo hilo na inalifuatilia kwa karibu ili kuhahakisha hakuna taratibu zinazokiukwa katika utekelezaji wa mradi huo.

  Mmoja wa maofisa wa ngazi za juu serikalini aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake alieleza kuwa, anafahamu kuwa Serikali ya India ilitoa mkopo usiokuwa na riba, wa zaidi ya sh bilioni 50 kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kununulia matrekta, wakati Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, alipofanya ziara nchini humo mapema mwaka huu, kwa sharti la kulipwa katika kipindi cha miaka 10.

  Alisema sharti jingine lililotolewa katika kutoa mkopo huo, linaitaka Serikali ya Tanzania kuhakikisha inanunua matrekta hayo kutoka kampuni za India na si vinginevyo.

  Ofisa huyo alisema, serikali iliamua kuikabidhi JKT jukumu la kusimamia utekelezaji wa mradi huo ili kuondoa mazingira yoyote ya kutokea udanganyifu katika kuutekeleza.

  Hata hivyo, alieleza wasiwasi wake iwapo kuna taarifa za baadhi ya maofisa wa JKT waliokabidhiwa jukumu la kusimamia utekelezaji huo, kuzungumza na mwakilishi wa Kampuni ya Escort hapa nchini (Jeetu), kisha wakaipa kampuni anayoiwakilisha zabuni hiyo bila kufuata taratibu.

  “Hili jambo linaweza kuharibu kabisa sifa ya JKT kama litakuwa kweli, kwa sababu itakuwa ni kashfa kubwa kwa jeshi kukiuka taratibu za manunuzi ya umma. Ingawa kuna imani kuwa si rahisi mambo ya kijeshi kuchunguzwa, lakini hili liko wazi mno kwa sababu ni zabuni iliyo wazi iliyokuwa ikifuatiliwa na wafanyabiashara wengi, hivyo hao hao wanaweza kuwa wametoa siri za taratibu kukiukwa,” alisema ofisa huyo.

  Waziri mmoja aliyezungumza na gazeti hili hivi karibuni, alisema suala hilo lilizungumzwa katika Baraza la Mawaziri na kupatiwa baraka zote za kulitekeleza. Aliongeza kuwa, anaamini hakuna taratibu zilizokiukwa.

  Hata hivyo, alionya kuwa Baraza la Mawaziri linazo taarifa za mfanyabiashara mmoja maarufu kufanya mpango wa kutoa taarifa za uongo kuhusu mchakato wa upatikanaji zabuni hiyo kwa sababu ya kisasi cha kukosa zabuni hiyo.

  Tanzania Daima Jumatano lilipowasiliana na Ofisa Habari wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Nadhifa Omary, ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema jambo hilo linaweza kuzungumziwa na waziri tu kwa sababu ya unyeti wake.

  Alieleza zaidi kuwa, hawezi kulizungumzia kwa sababu yuko nje ya ofisi kwa mapumziko, hivyo hana maelezo ya kina ya kulitolea ufafanuzi.

  Alipoulizwa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga, Dk. Hussein Mwinyi, alisema analifahamu vizuri suala hilo na alilihakikishia gazeti hili kuwa, hakuna utata wowote katika utekelezaji wa mradi huo, isipokuwa linaweza kufanywa ajenda ya kuchafuana na watu ambao wana malengo binafsi na mradi huo. “Ninalijua vizuri jambo hilo, tenda zilitangazwa na zikafunguliwa, nakuhakikishia. Mimi mwenyewe niliona kampuni kama 11 hivi zilizoomba zabuni hiyo, sasa kama kuna mtu anasema kulikuwa na kasoro, ni mambo ya wafanyabiashara kutaka kuchafuana tu kwa malengo binafsi waliyonayo katika mradi huo,” alisema.

  Naye Manji alipotafutwa kupitia simu yake ya kiganjani ili kuzungumzia suala hilo, kwa mara kadhaa ilikuwa ikipokelewa na wasaidizi wake na kueleza ameweka utaratibu wa kutoongea na waandishi wa habari mpaka inapobidi.
   
 7. M

  Mchili JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi sheria ya manunuzi ya 2004 haina kipengele kinachokataza makampuni yanayotuhumiwa kwa rushwa kupitishwa kwenye tender za serikali? Kama kipo kipengele hicho basi kampuni ya Jeetu ilitakiwa kuwa disqualified hata kama ina viwango vingine vyote vinavyotakiwa. Kama hicho kipengele hakipo basi hii kanuni ya manunuzi ina upungufu mkubwa.
   
 8. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwani tumelogwa na nani? Hivbi kweli serikali hii hii inathubutu tena kumpa tenda huyo jeetu patel? Inaniuma sana kwa kuwa nalipa kodi kila mwezi, inaniuma sana hata sijui nifanyeje.
  Unajua wakati mwingine naona yule jamaa aliyeamua kujipunguzia stress na kuongeza siku zake za kuishi kwa kutosikia habari kama hizi ana point. This is unbeliavable, kwani hao wahindi ndo wana serikali huku tanzania? afadhali Idd amini alivyowatimua uganda, i hate them, na zaidi hawa wake zao huko serikalini,am sick of this. Oh Lord, i think i need air!
   
 9. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2009
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Baada ya uchaguzi mkuu 2010 mdudu anayeitwa "KILIMO KWANZA" atakuwa amefika ukomo na hatasikika kamwe. The so called Kilimo Kwanza ni njia tu ya kutafuta fedha kwa ajili ya kununua kura kwenye uchaguzi wa 2010.
   
 10. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2009
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Duh inakula tena kwetu. Anyway, tumeshzoea kula bila kunawa. Ila tupo na brain tumours watanzania until we have our own "jerry rawlings". Naapa tumeliwa wima
   
 11. M

  Magezi JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Jitu ni tapeli na lina kesi ya EPA still miwaziri yetu ilivyo na mtindio wa ubongo inampa tender kubwa kama hiyo??

  Hivi kikwete una mawaziri kweli??? au na wewe ni mwizi tu???? Kwa nini unang'ang'ania hawa majizi wa kihindi wanaotudharau kila siku???

  ah..... unakera!!!!!!!!!!!!!
   
 12. N

  Nanu JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndugu wana JF na Watanzania hapa nimefuta machozi tu na kuanza kuandika.

  Nina uchungu sana na vitu viwili, kwanza kampuni yoyote yenye uhusiano na Jeetu Patel (hata familia yake au ndugu zake) isingepewa consideration yoyote katika hiyo tender. Mtandao wote wa huyu mtu uko corrupt pamoja na familiya yake yote. Regardless of the price, he shouldn't have been considered at all. Tender kama hizi serikali inatakiwa itoe kwa vikundi vya wajasiriamali wazalendo, vyama vya ushirika na ingetoa katika lots ili waweze kuafford. Hata hawa wezi hawatoi fedha zao wanapata fedha za benki tu na gurantee ni hiyo tender au agreement ya serikali tu.

  Pili sikufurahia kabisa jambo hili kupitia jeshini kwana hapa ni direct kuwa JK na CCM wanatafuta fedha za kampeni. Wote tunajua mambo ya meremeta wanasema ni jeshi hivyo hairuhusiwi kuhoji nini kilitokea, swali hili la matrekta, kwanini lipelekwe jeshini? Jibu ni wazi wanataka kumeremeta tena na hivyo wanataka kupitia mgongo wa jeshi. Jeshi tunalihudumia kwa kazi zetu, vipi liwe tena kwenye biashara? Je wizara ya kilimo haipo? Kwanini hili lipelekwe wizara ya ulinzi? Kama hatuwaamini watu wa wizara ya kilimo au hata biashara, kwani zisivunjwe na kufukuza watu wote na kuunda upya? Hili linatuachia maswali mengi sisi watanzania.

  Sasa nimegundua kuwa kuna utamaduni/culture ya wizi katika serikali zote.
   
 13. N

  Nanu JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Magezi, mwenyekiti wa cabinet ni JK. Maamuzi yote makubwa ya serikali yanapitia cabinet. Basi kama kuna utindio wa ubongo hata rais atakuwa nao......is part of the game though his outlook shows he is innocent but....we are experiencing the opposite from what we see from JK and his Govt. Piga ua hii Kilimo Kwanza ni wimbo wa JK na CCM yake wa kutokea 2010.
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  huyu jeetu (jitu???) si alisafishwa last week hapa?kumbe ndio haya yaja!!!
   
 15. M

  Mchili JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Au ni jinsi ya kupata hela ya uchaguzi..
   
 16. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kuna mtu kati yenu ametenda akanyimwa au mnalalamika kama kawida yenu ...jeetu ametenda akashinda wewe huna hata kampuni hujatenda sasa serikali unataka ije iweke matangazo barabarani kuhusu tender..guys acheni kulalamika kama wakatoliki wasio isha kulalamika na hawashibi na dunia!!!!!
   
 17. M

  Masatu JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sheria ya manunuzi haimkatazi mtu mwenye kesi mahakamani kuomba tender serikali. Jitu kashinda tenda kihalali, u just have to get over it na chuki zenu za kibaguzi.

  Shame on you!
   
 18. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hii ni dhahiri shahiri kuwa mafisadi papa wametushinda na ni dalili mbaya kwa ukombozi wa mnyonge.
   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mambo mengine ni ujinga na udhaifu wetu tu , si kila kitu ni njama za mafisadi
   
 20. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #20
  Oct 8, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Nitasema ukweli daima, uongo kwangu mwiko....

  Simfahamu Jeetu Patel, wala sina 'beef' naye.

  Lakini, hebu tujiulize. Ingekuwa mimi au wewe - Mmatumbi mwenzangu - ndio tumeshinda hiyo zabuni, fair and square, lakini TUNA KESI MAHAKAMANI, je, tungekubaliwa?

  Ninachojua mimi, katika ethics, mtu yeyote ambaye anatuhumiwa -- hata ukiwa kazini -- anasimamishwa kwanza, mpaka kesi yake iishe. Iweje leo, Jeetu Patel, na wenzake, wana KESI MAHAKAMANI, tena ya EPA, kisha kampuni yake ndiyo ishinde zabuni hiyo?

  Tunakwenda wapi?

  ./Mwana wa Haki
   
Loading...