Ufisadi mwingine huu ndani ya serikali yetu ya tanzania

Watanzania vilaza kwenye kila kitu, someni majarida na magazeti yenye kuongeza knowledge na sio magazeti ya ngono.
Wapi ulisoma kazi ya waziri mkuu au waziri yoyote wa serikali ni kufungua seminars?????? Na jingine semina ufanye wewe halafu akulipie nani??????
Shame on you people, fyi hizi ni taratibu za kawaida nchi sote na sio hata rais.
Nina wasiwasi mkubwa na exposure yako mkuu... zingatia ushauri wa warea, wabongo wengi mjifungia hapo ndani na ku-assume mnajua kila kitu... ni kwenye nchi maskini tena za kiafrika ndio unakuta viongozi wake wanalipwa mara mbili kufanya kazi moja!!! Waziri au mkurugenzi yuko dar.... masaki na ofisi ya wizara iko pamba road posta, anaitwa kwenye ufunguzi wa semina ya mamlaka iliyochini ya wizara yake inayofanyika karimjee, muda wa kazi, anatumia gari la ofisi.... analipwa perdiem kama amesafiri kwenda sumbawanga.... its not fair na nchi haitopiga hatua kwa style hii!!!
 
Tatizo liko kwenye warsha serikalini, NGO na hata vyuoni kwenyewe wanakosomea watendanji wengi wa serikalini, vyama vya siasa, NGO nk. Kwenye secta binafsi sio tatizo sana.

Kuna wakati PM Pinda alipiga marufuku hili tatizo la warsha za kugawana pesa, lakini moto wake umeshapooooa kabisa. labda tumkumbushe auwashe tena. Ila naomba atafute ushauri wa kitaalamu zaidi kuliko wa kisiasa.

Tatizo hasa linasababishwa na mishahara midogo. Sasa Afisa wa serikali analipwa laki tatu kwa mwezi! akienda sokoni bei ziko juu. hiyo laki 3 anaambulia mpunga tu wa watoto nyumbani. Hela ya kulipa ada itatoka wapi? Kijijini wanambeep ili awapigie simu na watumie chochote, atatoa wapi? Msiba, harusi, kinywaji, nauli au mafuta ya gari atayatoa wapi? Sasa akitokea kuna mwanya wa kuwa na warsha na fungu lipo ataacha kuandaa ili ajilipe kihalali?

Serikali badilikeni. Huwezi kumlipa mtumishi wa mjini mshahara wa laki 2 ukategemea atafanya miujiza ya kuishi. Labda wa kijijini, naye pia ataishia shambani kwake ili kunusuru maisha yake.
 
Watanzania vilaza kwenye kila kitu, someni majarida na magazeti yenye kuongeza knowledge na sio magazeti ya ngono.
Wapi ulisoma kazi ya waziri mkuu au waziri yoyote wa serikali ni kufungua seminars?????? Na jingine semina ufanye wewe halafu akulipie nani??????
Shame on you people, fyi hizi ni taratibu za kawaida nchi sote na sio hata rais.

Nawe huwa unazikata nini mbona umejihami. Ni uwizi mtupu wala usihalalisha.
 
Vandugu leo nimefurahishwa sana na mada yenye maana inayotazama tuliko na tunakoenda. Hiyo mimi imekua ikinikera sana na mbaya zaidi kiukweli nilipo ndiyo naandika speech ukiipeleka kwa wengi wasio wajibika anakurudishia eti imekaa vyema ispokua kwenye salamu badili hivi mara vile ikimaanisha hajaisoma kabisa kaiangalia tu. Pamoja na hayo yote kwa kwa sababu ya protocol mimi ninapewa mihela kumkabidhi mheshimiwa kwa ujumla ni mshahara wangu wa mwezi kabla sijakatwa makato dahh tunaumia, sikuingine walimkabidhi secretary akachomoa robo tatu nzima msaidizi wa waziri akapiga simu eti mmetuwekea bei gani kwenye bahasha hela mbuzi hivi kumuuliza akasema walichokuta kuchunguza lilikua panga nikasema safi sana. Kuna bwana mmoja ambaye nitamheshimu sana anaitwa Juma V. Mwapachu wa EAC nilimwandikia speech lakini jamaa akairudisha kwa email kuwa kwanini unisemee badala ya mimi kusema???? Asubuhi alitoa bonge la speech acha kabisa na hakupewa hata dala (shilingi tano). Nawaasa vijana tunaopenda mapesa ya haraka bila jasho, tuwajibike kikamilifu sina tatizo kama hela unachukua speech umeandika mwenyewe na mkutano utautumia kwa manufaa ya nchi.
 
Watanzania vilaza kwenye kila kitu, someni majarida na magazeti yenye kuongeza knowledge na sio magazeti ya ngono.
Wapi ulisoma kazi ya waziri mkuu au waziri yoyote wa serikali ni kufungua seminars?????? Na jingine semina ufanye wewe halafu akulipie nani??????
Shame on you people, fyi hizi ni taratibu za kawaida nchi sote na sio hata rais.

Bangi za kujificha hizi
 
Kinachosikitisha zaidi na kule serikalini anatoka na posho yake so anapata posho mara mbili...? Huu ni unyonyaji wa hali ya juu bila hata huruma ya kodi ya walalahoi wanaoumia usiku na mchana kutafuta mlo mmoja tu..!

Mbaya zaidi huko nako wanakompokea huyo kiongozi anayekwena kufungua warsha, kongamano, n.k. nao wanatumia mwanya huo kulamba hela ya umma.
 
Jamani hivi mnajua kua ukimwalika Mkuu wa mkoa, Waziri, Mkuu wa wilaya au kiongozi yeyote serikalini aje kufungua Mkutano, warsha, semina au mafunzo Unamlipa hela.
1. unamlipa full perdiem kama vile ameenda kikazi nje ya kituo chake cha kazi,
2. unamlipa hela ya kufungulia mkutano au hiyo shughuli uliyoiandaa
3. unamlipa hela ya mafuta ya gari alilotumia kuja nalo
4. unamlipa na dereva wake
5. Hotuba anayokuja kuisoma wakati wa kufungua hiyo semina unaiandaa wewe uliyemualika
Sasa kinachotokea akifika hapo anaisoma hiyo hotuba akimaliza kuisoma anawatakieni semina njema then anachukua hela zake anarudi Ofisin kwake kuendelea na shughuli zake zingine
Hii ndo hali halisi tunayokutana nayo
Kama hata hotuba anaandaliwa sasa huu ni upumbavu
 
Vandugu leo nimefurahishwa sana na mada yenye maana inayotazama tuliko na tunakoenda. Hiyo mimi imekua ikinikera sana na mbaya zaidi kiukweli nilipo ndiyo naandika speech ukiipeleka kwa wengi wasio wajibika anakurudishia eti imekaa vyema ispokua kwenye salamu badili hivi mara vile ikimaanisha hajaisoma kabisa kaiangalia tu. Pamoja na hayo yote kwa kwa sababu ya protocol mimi ninapewa mihela kumkabidhi mheshimiwa kwa ujumla ni mshahara wangu wa mwezi kabla sijakatwa makato dahh tunaumia, sikuingine walimkabidhi secretary akachomoa robo tatu nzima msaidizi wa waziri akapiga simu eti mmetuwekea bei gani kwenye bahasha hela mbuzi hivi kumuuliza akasema walichokuta kuchunguza lilikua panga nikasema safi sana. Kuna bwana mmoja ambaye nitamheshimu sana anaitwa Juma V. Mwapachu wa EAC nilimwandikia speech lakini jamaa akairudisha kwa email kuwa kwanini unisemee badala ya mimi kusema???? Asubuhi alitoa bonge la speech acha kabisa na hakupewa hata dala (shilingi tano). Nawaasa vijana tunaopenda mapesa ya haraka bila jasho, tuwajibike kikamilifu sina tatizo kama hela unachukua speech umeandika mwenyewe na mkutano utautumia kwa manufaa ya nchi.

Ndo maana hotuba za mkulu za kusoma cku hizi zinakuwa pumba tupu,kumbe mwandishi mwenyewe ndo ww-sasa kama hata kuwasilisha ujumbe wenye kueleweka kwa wana jf huwezi,vipi utaweza kuandaa ujumbe wenye kueleweka kwa taifa zima? Huyo mwapachu alikurudishia hyo speech yako kwa kuwa ilikuwa shallow,kaulize watu wa EAC kama huwa haandikiwi speech, na hakuchuku hilo dala lako ni kwa kuwa alikunja dola zake kabla hajaja hapo-Wote ni ndege wa kundi moja tu hawa! Jifunze kufikiri japo 10% ya wenye kufikiri wanachofikiri-
 
Back
Top Bottom