sijulikani
Member
- May 15, 2014
- 52
- 89
Ajira za walimu zilitangazwa kwamba zitaanza April 01, 2014. Kweli ikawa hivyo, wengi wakaenda Halmashauri na hata wakaripoti mashuleni. Utaratibu unawataka kupeleka cheque number ambayo ikifika halmashauri basi ndiyo itakayotumika kutumia mishahara.
Baadhi wakapeleka cheque number lakini wachache tu wakapata mshahara wa April 2014. Wengi wakakosa. Ikadhaniwa kwamba tatizo la cheque namba likiisha kama walivyoelekezwa na kama walivyopewa wenzao wachache, basi mshahara wa April 2014 yaani mwezi unaoisha sasa watapa mishahara yao bila kikwazo.
Lakini ajabu ni kwamba juzi zimeanza kusambaa meseji kwenye simu kwamba walimu wanatakiwa kupeleka Halmashauri barua zao za kuomba mshahara wa mwezi huu yaani May 2014! Hakuna barua yoyote ya kufafanua au kuwaita kwa hilo bali ni hizi meseji zinazosambaa tu. Huu ndiyo utaratiibu
Hivyo ndivyo hali halisi Mwanza, wilaya ya Nyamagana. Lakini wakiulizwa walimu wa jirani yaani wa wilaya ya Ilemela, hawana tatizo hili. Wamepata mishara yao tangu mwezi walipoajiriwa April 2014.
Hiki ndicho inachokifanya uongozi wa Nyamagana bila kujali kwamba walimu hawa wanaendelea kusota bila mishahara haijulikani wanaishi vipi, wanalipia vipi pango za nyumba wanazoishi, haijulikanii wanakula kwa hela gani na ndiyo kwanza wanaanza maisha wakitokea vyuoni.
Kama kawaida habari hii hajaandikwa wala kufuatiliwa na chombo chochote cha habari ikiwemo mbunge wa Nyamagana.
Ndiyo kwanza inawaslishwa hapa JF ambacho ndiyo chombo kinachoongza sasa kwa kufumua wazi madudu kama haya.
Keep it JF, the place we dare talk openly.