Ufisadi Chuo Kikuu Mkwawa

MDANGANYIKAJI

Member
Jan 27, 2011
77
59
UONGOZI wa Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu Mkwawa(Muce), unakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali chuoni hapo.

Ufisadi huo unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wa chuo hicho ni pamoja na wizi wa fedha za chuo kupitia mikataba ya zabuni, upendeleo, kujilipa mishahara mara mbili pamoja na kuendesha akaunti za benki za muda maalum(Fixed Deposit), kwa kutumia fedha za Serikali, au za wafadhili na hivyo kuchelewesha malipo mbalimbali ya watoa huduma na kwa wanafunzi.

Uongozi wa chuo hicho umethibitisha baadhi ya madai na kuyakanusha vikali mengine, huku ukidai kuwa hizo ni njama za baadhi ya watu, au wafanyakazi wanaotaka kuchafua taswira ya taasisi hiyo ya elimu ya juu.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi umebaini kuwa kuna wafanyakazi watatu(majina yao tunayo), wa chuo hicho ambao wamekuwa wakijilipa mishahara mara mbili.

Nyaraka kadhaa ambazo Mwananchi imeziona zinaonesha kuwa mfanyakazi wa kitengo cha computer chuoni hapo (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye ngazi ya mshahara wake ni kati ya Sh318,620 na 339,860 kwa mwezi kwa kupendelewa amekuwa akilipwa mshahara wa Sh750,000 kwa mwezi tangu Agosti 2006 alipoajiriwa.

Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi, mtumishi huyo alipangiwa kiwango hicho cha mshahara na wakubwa wake wakimwambia kwamba mshahara huo "ni kwa ajili yake tu", kauli mbayo haikuwa na maelezo ya kuridhisha.

Mwingine ambaye alikuwa akifanya kazi katika ofisi ya uhasibu (pia jina tunalo), ambaye mshahara wake unapaswa kuwa Sh622,578 kwa mwezi, amekuwa akijilipa au kulipwa mshahara huo pamoja na mshahara mwingine wa Sh700,000 kila mwezi.

Mfanyakazi huyo hulipwa mishahara hiyo kwa ustadi mkubwa kwa kupitia akaunti za chuo hicho za benki mbili tofauti ambazo ni CRDB tawi la Iringa na NBC tawi la mjini humo, japokuwa hikufahamika mara moja ni benki gani kati ya hizo hutumika kumlipa mshahara wenye utata.

Kadhalika uchunguzi unaonyesha kuwa mfanyakazi wa tatu ambaye tayari amekwishaacha kazi katika chuo hicho (jina lake pia tunalihifhadhi), licha ya kwamba mshahara wake ulikuwa wa Sh911,060 alikuwa akichota mshahara mwingine wa Sh507,590/- kupitia akaunti za chuo hicho za CRDB na NBC.

Taarifa kutoka Muce zinadai kwamba hivi sasa wafanyakazi wote watatu wanaotuhumiwa kujipatia fedha kwa kujilipa au kulipwa mishahara miwili kila mwezi hawapo chuoni hapo kutokana na sababu mbalimbali.

Mmoja wa watuhumiwa hao inadaiwa yuko mkoani Tanga ambako amekwenda likizo, wakati mwingine anadaiwa kuacha kazi ghafla, kitendo kinachotafsiriwa kuwa anakimbia mkono wa sheria baada ya kuvuja kwa taarifa zinazomuhusisha na ufisadi huo. Mtuhumiwa wa tatu inadaiwa kuwa yuko rumande ambako anashikiliwa na polisi wa jijini Dar es Salaam akikabiliwa na kesi nyingine.

Akizungumzia madai ya watumishi hao kulipwa mishahara mara mbili, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Phillemon Mushi alikiri kufanyika kwa ufisadi huo lakini akasema tayari hatua zimechukuliwa dhidi ya wahusika.

Hata hivyo, uchunguzi unaonesha kuwa watuhumiwa hao hawajachukuliwa hatua za kisheria zaidi ya kuondolewa katika idara walizokuwa wakifanya kazi na kuhamishiwa idara nyingine tofauti za chuo hicho.

Madai mengine yanayoukabili uongozi wa chuo hicho ni wizi wa fedha za umma kupitia mikataba ya mzabuni aliyekuwa akitoa huduma ya mtandao (jina tunalo).

Taarifa zinaonesha kuwa, kulingana na mkataba wake, malipo ya mzabuni huyo kwa mwezi ilikuwa dola za Marekani 13,040 lakini baadhi ya watumishi wa Idara ya Uhasibu na Ugavi walikuwa wakishirikiana kulipa mara mbili kiasi hicho cha fedha.

Wizi huo ulikuwa unafanikishwa kwa ustadi mkubwa kwa kuandika hundi mbili zenye kiasi cha dola za Marekani 13,040 sawa na Sh19,951,200 kwa kila hundi huku zikionesha kuwa anayelipwa ni mzabuni huyo na kwamba wizi huo unadaiwa kufanyika kati ya mwaka 2006/2007 na 2008/2009.

"Lakini baada ya hundi hizo kuwa zimepita kila mahali kwa ajili ya kuidhinishwa, hundi moja ilikuwa inawekwa kwenye akaunti tofauti na wafanyakazi hao kugawana fedha hizo,” anasema mtoa taarifa wetu.

Mwananchi lilifanikiwa kupata namba za hundi na akaunti iliyokuwa inatumika kufanikisha wizi huo, ambapo vyanzo vyetu kutoka ndani ya benki za CRDB na NBC Iringa mjini vimethibitisha kuchukuliwa kwa fedha hizo kwa kutumia hundi hizo.

Hata hivyo, Professa Mushi alipoulizwa juu ya suala hilo alisema ni jambo la zamani (anataja mwaka 2009) na kwamba kwa sasa hilo siyo jambo la kujadiliwa.

"Jamani hebu mtuache nasi tufanye kazi basi hata kidogo hiyo 'issue' (hilo suala) ni la zamani mno, hata huyo (anataja jina la mzabuni) hayupo tena hapa chuoni,” alisema Professa Mushi na kuongeza:

"Unajua inaonekana mmeiba taarifa ya ukaguzi ambayo hata haikuwa imekamilika na ilikuwa siri, huyo mtu anayekuletea mambo hayo anatapatapa tu”.

Wakati Profesa Mushi akielezea kuhusu madai hayo, Muce pia inakabiliwa na tuhuma za kutumia fedha umma kuendesha akaunti za muda maalum (Fixed Deposit Account) bila kuweka wazi faida inayotokana na akaunti hizo.

Uchunguzi unaonesha kuwa, mpaka Juni mwaka jana, chuo hicho kilikuwa kinaendesha akaunti zaidi ya nne za muda maalum (namba za akaunti hizo tunazo) ambazo zilikuwa na zaidi ya Sh500 milioni.

Akaunti nne ambazo zipo kwenye benki moja yenye tawi mjini Iringa zinaonesha kuwa akaunti ya kwanza ilikuwa na kiasi cha Sh10,090,999.55, nyingine ilikuwa na kiasi cha Sh201,247,671.23, pia ilikuwepo akaunti yenye Sh252,853,107.40 na ya mwisho ilikuwa na kiasi cha 75,195,042.70 ambapo jumla yake ni Sh 539,386,820.88.

Alipohojiwa kuhusu akaunti hizo, Professa Mushi alisema aulizwe Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho (Fedha na Utawala),Professa Machiwa kwa maelezo kuwa ndiye alikuwa anafahamu vyema suala hilo.

Professa Machiwa alipoulizwa alidai kuwa akaunti hizo hazikuwa kwenye orodha ya akaunti za chuo hicho na kwamba hakuwa anazifahamu wala kuwa na taarifa nazo.

"Hata nikikuonyesha taarifa yangu ya kila siku akaunti hizo hazimo labda kamwone mhasibu wa chuo anaweza kuwa ana taarifa zaidi,” alisema Professa Machiwa lakini kabla mwandishi hajaondoka akaamua vinginevyo:

"Hebu ngoja nimpigie mhasibu aende benki naye akaangalie ili atuletee taarifa kama akaunti hizo ni za Mkwawa University, kwa hiyo njoo baadaye nitakupa taarifa,” alisema.

Hata hivyo, mwandishi aliporejea mchana wa Januari 28 mwaka huu, Professa Machiwa alisema watu wa benki walikuwa wamegoma kutoa taarifa za akaunti hizo mpaka waandikiwe barua.

"Nimeandika barua nimeshawapelekea hivyo naomba uje wiki ijayo na kwa kuwa sitakuwepo, utakuta taarifa kwa katibu muhtasi wangu,” alisema .

Mwananchi lilifuatilia kwa siku tatu mfululizo bila kupata majibu kwa katibu muhtasi wake na kuamua kumtafuta tena Professa Mushi kwa simu ambaye baada ya kuulizwa suala hilo alisema: "Mbona Professa Machiwa ameshakujibu, usinisumbue,” alisema kwa kifupi na kukata simu.

Hata hivyo, baadaye alipiga simu kwa mwandishi wa Mwananchi na kueleza kuzifahamu akaunti hizo na kudai kuwa pia zilikuwa za zamani na kwamba hivi sasa hazipo tena kwani zimeishafungwa.

"Unaziona kama ni nyingi lakini akaunti ni moja tu yaani kila akaunti ya kwanza inapokuwa tayari faida inachukuliwa na kufunguliwa akaunti nyingine,” alisema.

Professa Mushi alifafanua kuwa fedha zilizokuwa zimewekwa kwenye akaunti ya muda maalum zilitoka kwa wafadhili ambao hata hivyo hakuwataja na kwamba zilikuwa kwa ajili ya ukarabati wa majengo lakini baada ya mkandarasi kusuasua, waliamua kuziweka kwenye akaunti ya muda maalum ili kuepusha kuzitumia kwa shughuli zingine.

-------------
Ndio maana nilijiuliza siku ile Mkwawa walivyogoma then kesho yake hela ikatoka, je ilitoka wapi? Kwa hiyo inawezekana wanafanyia ufisadi hata hela ya wanafunzi ! Wakigoma Slaa amechochea ama kweli this is Tanzania! Na utaona hakuna measure yoyote itakayochukuliwa ni funika kombe mwanaharamu apite:hungry::hungry:
 
Tupe source kiongozi hasa kwenye swala la zabuni na mishahara maana mishahara inalipwa na serikali kama inafanywa tofauti basi kuna uwalakini. Tusaidie source mkuu au utupe mwelekezo tu maana ofisi ya Hesabu za serikali (Auditor Generala) inafuatilia kwa makini hesabu za matumizi ya fedha za umma vyuo vikuu vyote TZ baada ya UDOM.

Swala la njaa halihusiani na chuo kabisa mwanafunzi anatoka nyumbani anakuja kusoma swala la ada na fedha za matumizi ni la mwanafunzi na chuo hakihusiki na ni wapi mwanafunzi anapata fedha ila chuo kitatoa ushirikiano pale tu kitakapohitajika. Siku mikopo ilichelewa nilifuatilia kwa undani na swala lilishajibiwa na Bodi ya Mikopo kwamba Mkwawa walichelewa kupeleka majina ya wanafunzi ndiyo maana cheki ikachelewa kufika kwa siku moja, hela ilipaswa kuwafikia wanafunzi tarehe 15/01/2011 siku waliyogoma badala yake wakapata 17 baada ya Cheki kumature (banking system) kwa ujumla naweza sema mambo mawili moja Mkwawa na vyuo vingine tujali muda (punctuality) na pia wote tuwe wavumilivu.

Kwa swala la kusema slaa nauhakika slaa hawezisema watu wagome ila ndiyo sera ya Mbowe ameshanukuliwa na media mara kadhaa akisema atahakikisha serikali ya ccm inapatashida mwaka huu kwa namna yoyote. Kwa hilo hata kama chadema haihusiki basi doubts zitaenda kwao tu.
 
UONGOZI wa Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu Mkwawa(Muce), unakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali chuoni hapo.

Ufisadi huo unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wa chuo hicho ni pamoja na wizi wa fedha za chuo kupitia mikataba ya zabuni, upendeleo, kujilipa mishahara mara mbili pamoja na kuendesha akaunti za benki za muda maalum(Fixed Deposit), kwa kutumia fedha za Serikali, au za wafadhili na hivyo kuchelewesha malipo mbalimbali ya watoa huduma na kwa wanafunzi.

Uongozi wa chuo hicho umethibitisha baadhi ya madai na kuyakanusha vikali mengine, huku ukidai kuwa hizo ni njama za baadhi ya watu, au wafanyakazi wanaotaka kuchafua taswira ya taasisi hiyo ya elimu ya juu.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi umebaini kuwa kuna wafanyakazi watatu(majina yao tunayo), wa chuo hicho ambao wamekuwa wakijilipa mishahara mara mbili.

Nyaraka kadhaa ambazo Mwananchi imeziona zinaonesha kuwa mfanyakazi wa kitengo cha computer chuoni hapo (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye ngazi ya mshahara wake ni kati ya Sh318,620 na 339,860 kwa mwezi kwa kupendelewa amekuwa akilipwa mshahara wa Sh750,000 kwa mwezi tangu Agosti 2006 alipoajiriwa.

Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi, mtumishi huyo alipangiwa kiwango hicho cha mshahara na wakubwa wake wakimwambia kwamba mshahara huo "ni kwa ajili yake tu", kauli mbayo haikuwa na maelezo ya kuridhisha.

Mwingine ambaye alikuwa akifanya kazi katika ofisi ya uhasibu (pia jina tunalo), ambaye mshahara wake unapaswa kuwa Sh622,578 kwa mwezi, amekuwa akijilipa au kulipwa mshahara huo pamoja na mshahara mwingine wa Sh700,000 kila mwezi.

Mfanyakazi huyo hulipwa mishahara hiyo kwa ustadi mkubwa kwa kupitia akaunti za chuo hicho za benki mbili tofauti ambazo ni CRDB tawi la Iringa na NBC tawi la mjini humo, japokuwa hikufahamika mara moja ni benki gani kati ya hizo hutumika kumlipa mshahara wenye utata.

Kadhalika uchunguzi unaonyesha kuwa mfanyakazi wa tatu ambaye tayari amekwishaacha kazi katika chuo hicho (jina lake pia tunalihifhadhi), licha ya kwamba mshahara wake ulikuwa wa Sh911,060 alikuwa akichota mshahara mwingine wa Sh507,590/- kupitia akaunti za chuo hicho za CRDB na NBC.

Taarifa kutoka Muce zinadai kwamba hivi sasa wafanyakazi wote watatu wanaotuhumiwa kujipatia fedha kwa kujilipa au kulipwa mishahara miwili kila mwezi hawapo chuoni hapo kutokana na sababu mbalimbali.

Mmoja wa watuhumiwa hao inadaiwa yuko mkoani Tanga ambako amekwenda likizo, wakati mwingine anadaiwa kuacha kazi ghafla, kitendo kinachotafsiriwa kuwa anakimbia mkono wa sheria baada ya kuvuja kwa taarifa zinazomuhusisha na ufisadi huo. Mtuhumiwa wa tatu inadaiwa kuwa yuko rumande ambako anashikiliwa na polisi wa jijini Dar es Salaam akikabiliwa na kesi nyingine.

Akizungumzia madai ya watumishi hao kulipwa mishahara mara mbili, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Phillemon Mushi alikiri kufanyika kwa ufisadi huo lakini akasema tayari hatua zimechukuliwa dhidi ya wahusika.

Hata hivyo, uchunguzi unaonesha kuwa watuhumiwa hao hawajachukuliwa hatua za kisheria zaidi ya kuondolewa katika idara walizokuwa wakifanya kazi na kuhamishiwa idara nyingine tofauti za chuo hicho.

Madai mengine yanayoukabili uongozi wa chuo hicho ni wizi wa fedha za umma kupitia mikataba ya mzabuni aliyekuwa akitoa huduma ya mtandao (jina tunalo).

Taarifa zinaonesha kuwa, kulingana na mkataba wake, malipo ya mzabuni huyo kwa mwezi ilikuwa dola za Marekani 13,040 lakini baadhi ya watumishi wa Idara ya Uhasibu na Ugavi walikuwa wakishirikiana kulipa mara mbili kiasi hicho cha fedha.

Wizi huo ulikuwa unafanikishwa kwa ustadi mkubwa kwa kuandika hundi mbili zenye kiasi cha dola za Marekani 13,040 sawa na Sh19,951,200 kwa kila hundi huku zikionesha kuwa anayelipwa ni mzabuni huyo na kwamba wizi huo unadaiwa kufanyika kati ya mwaka 2006/2007 na 2008/2009.

"Lakini baada ya hundi hizo kuwa zimepita kila mahali kwa ajili ya kuidhinishwa, hundi moja ilikuwa inawekwa kwenye akaunti tofauti na wafanyakazi hao kugawana fedha hizo,” anasema mtoa taarifa wetu.

Mwananchi lilifanikiwa kupata namba za hundi na akaunti iliyokuwa inatumika kufanikisha wizi huo, ambapo vyanzo vyetu kutoka ndani ya benki za CRDB na NBC Iringa mjini vimethibitisha kuchukuliwa kwa fedha hizo kwa kutumia hundi hizo.

Hata hivyo, Professa Mushi alipoulizwa juu ya suala hilo alisema ni jambo la zamani (anataja mwaka 2009) na kwamba kwa sasa hilo siyo jambo la kujadiliwa.

"Jamani hebu mtuache nasi tufanye kazi basi hata kidogo hiyo 'issue' (hilo suala) ni la zamani mno, hata huyo (anataja jina la mzabuni) hayupo tena hapa chuoni,” alisema Professa Mushi na kuongeza:

"Unajua inaonekana mmeiba taarifa ya ukaguzi ambayo hata haikuwa imekamilika na ilikuwa siri, huyo mtu anayekuletea mambo hayo anatapatapa tu”.

Wakati Profesa Mushi akielezea kuhusu madai hayo, Muce pia inakabiliwa na tuhuma za kutumia fedha umma kuendesha akaunti za muda maalum (Fixed Deposit Account) bila kuweka wazi faida inayotokana na akaunti hizo.

Uchunguzi unaonesha kuwa, mpaka Juni mwaka jana, chuo hicho kilikuwa kinaendesha akaunti zaidi ya nne za muda maalum (namba za akaunti hizo tunazo) ambazo zilikuwa na zaidi ya Sh500 milioni.

Akaunti nne ambazo zipo kwenye benki moja yenye tawi mjini Iringa zinaonesha kuwa akaunti ya kwanza ilikuwa na kiasi cha Sh10,090,999.55, nyingine ilikuwa na kiasi cha Sh201,247,671.23, pia ilikuwepo akaunti yenye Sh252,853,107.40 na ya mwisho ilikuwa na kiasi cha 75,195,042.70 ambapo jumla yake ni Sh 539,386,820.88.

Alipohojiwa kuhusu akaunti hizo, Professa Mushi alisema aulizwe Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho (Fedha na Utawala),Professa Machiwa kwa maelezo kuwa ndiye alikuwa anafahamu vyema suala hilo.

Professa Machiwa alipoulizwa alidai kuwa akaunti hizo hazikuwa kwenye orodha ya akaunti za chuo hicho na kwamba hakuwa anazifahamu wala kuwa na taarifa nazo.

"Hata nikikuonyesha taarifa yangu ya kila siku akaunti hizo hazimo labda kamwone mhasibu wa chuo anaweza kuwa ana taarifa zaidi,” alisema Professa Machiwa lakini kabla mwandishi hajaondoka akaamua vinginevyo:

"Hebu ngoja nimpigie mhasibu aende benki naye akaangalie ili atuletee taarifa kama akaunti hizo ni za Mkwawa University, kwa hiyo njoo baadaye nitakupa taarifa,” alisema.

Hata hivyo, mwandishi aliporejea mchana wa Januari 28 mwaka huu, Professa Machiwa alisema watu wa benki walikuwa wamegoma kutoa taarifa za akaunti hizo mpaka waandikiwe barua.

"Nimeandika barua nimeshawapelekea hivyo naomba uje wiki ijayo na kwa kuwa sitakuwepo, utakuta taarifa kwa katibu muhtasi wangu,” alisema .

Mwananchi lilifuatilia kwa siku tatu mfululizo bila kupata majibu kwa katibu muhtasi wake na kuamua kumtafuta tena Professa Mushi kwa simu ambaye baada ya kuulizwa suala hilo alisema: "Mbona Professa Machiwa ameshakujibu, usinisumbue,” alisema kwa kifupi na kukata simu.

Hata hivyo, baadaye alipiga simu kwa mwandishi wa Mwananchi na kueleza kuzifahamu akaunti hizo na kudai kuwa pia zilikuwa za zamani na kwamba hivi sasa hazipo tena kwani zimeishafungwa.

"Unaziona kama ni nyingi lakini akaunti ni moja tu yaani kila akaunti ya kwanza inapokuwa tayari faida inachukuliwa na kufunguliwa akaunti nyingine,” alisema.

Professa Mushi alifafanua kuwa fedha zilizokuwa zimewekwa kwenye akaunti ya muda maalum zilitoka kwa wafadhili ambao hata hivyo hakuwataja na kwamba zilikuwa kwa ajili ya ukarabati wa majengo lakini baada ya mkandarasi kusuasua, waliamua kuziweka kwenye akaunti ya muda maalum ili kuepusha kuzitumia kwa shughuli zingine.
 
Kudai haki za msingi bila kuvunja sheria kama kugoma kwa wanavyuo ni haki yao kwani hawawezi soma bila kula namahitaji mengine ya msingi,hivyo serikali isisubiri mgomo ndipo watafute suluhisho kama UDOM.changamoto zinazotolewa na wapinzani ni manufaa kwa waathirika wa bodi ya mikopo,haikidhi mahitaji ya wanafunzi bora ivunjwe na kuundwa upya na washirikishwe wahadhiri nawanafunzi wa vyuo vyote
 
yaleyaleeeeeeeeeeee yaani wafanyakazi hawabadiliki jamani sasa sijui hata tufanye nini ili kuliokoa taifa hili mishahara mtu anachukulia kwenye benki mbili na bado uongozi unamfuga tu mbaya zaidi hii ni sehemu ambayo tunaamini imejaa vichwa vya wasomi kweli kazi ipo!
 
source ya habari hii ni Gazeti MWANANCHI: 11TH FEBRUARY 2011, Uk 1 na 4! yapo mengi tu yameelezwa humo ambayo inabidi yapewe uzito na serikali! na inawezekana yapo mengi tu yameachwa, mfano source moja inasema kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi walinyimwa hela za kujikimu (subsistance allowance), wengine wamekopeshwa mishaara yao, na wengine wamepewa promotion kutoka ngazi moja kwenda nyingine e.g. FROM TA kwenda ASSISTANT LECTURERS lakini wamekaa zaidi ya mwaka bila badiliko la mshahara, na wengine bado! inasemekana hakuna maelezo ya kuridhisha! kuna mengi sana ndani ya MKWAWA:twitch:!
 
Baada ya miaka 7 ndio anakuja kuzungumziwa Profesa Mushi ambae kwa sasa hivi ameshasepa
Profesa Mushi wa MUCE achezea sharubu za Rais Magufuli kwa ufisadi. Vyombo vya dola vyaagizwa kumchunguza
 
Na kuna watu walikuwa wanayatetea haya kwa kuwaita wazushi wanaosema!ila leo wanajifanya nao wanapambana!kweli tumetoka mbali
 
Tutaambiwa sababu Prof Mushi Ni mchaga ndiyo maana anasumbuliwa na awamu hii wengine watatuambia Ni siasa za chuki na visasi.

Ya Ngoswe haya.
 
Alieleta kihelehele Cha kutaka Mkuu aje azindue Chuo kawagharimu wenzie
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom