Ufisadi Magari Chadema, Fedha ACT; Wananchi Wataka CAG Azidishe Ukaguzi wa Vyama

blix22

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
213
645
Na Waandishi Wetu, Dodoma, Dar

BAADA ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukabiliwa na kashfa ya kupotea katika mazingira ya utata kwa magari mawili yenye thamani ya shilingi milioni 172,227,083 kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2017/2018 na gari moja la Chama kumilikishwa kiutata kwa mbunge mmoja, sasa wananchi wametoa maoni yao.

Wananchi hao wametoa maoni hasa baada ya kubainika katika vyama kadhaa vya upinzani tena vinavyohsbikia utawala bora na matumizi sahihi ya fedha za umma kumeanza kushamiri tabia za kifisadi jamno ambalo haliashirii mema kwa nchi.

Mbali ya Chadema, Chama cha ACT Wazalendo cha Mbunge Zitto Kabwe kimeelezwa kupoteza mamilioni ya fedha za ruzuku, kikitajwa pia NCCR ya Mbatia. Aidha, Halmashauri ya Kigoma Ujiji inayoongozwa na ACT Wazalendo imeendelea kupata hati chafu badala ya kuwa mfano bora wa usimamizi wa fedha za umma.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ukaguzi huo kwa upande wa Chadema umebaini kuwa magari hayo hayakuwepo katika himaya za chama hicho hadi kufikia Juni 30,2018 hali inayoashiria kuwa yamemilikishwa kwa viongozi wa chama kama mali binafsi kinyume na taratibu.

" Timu ya Ukaguzi haikupewa nyaraka na mchakato wa manunuzi ya magari hayo hali inayoonesha kuwa taratibu za manunuzi hazikuzingatiwa lakini taarifa ya fedha ya chama ilionesha kuwa yalinunuliwa," Inasisitiza ripoti hiyo ya CAG kuhusu Chadema.
Taarifa hiyo imeendelea kubainisha kuwa kuna malipo yamekuwa yakifanyika kwa viongozi bila kuwa na nyaraka muhimu kudhibitisha uhalali wa malipo hayo hali inayoonesha kuwa viongozi hao wamegeuza chama hicho kuwa kama taasisi binafsi.

Aidha, matumizi ya chama hicho kwa mujibu wa ripoti hiyo kwa mwaka unaoishia Juni 30,2018, yalijumuisha kiasi cha shilingi 10,948,000 sawa na asilimia 67 ya matumizi yote ya kiasi ambacho hakikuwa na nyaraka muhimu za kudhibitisha uhalali wake.
Mbali ya hayo ripoti hiyo inaonesha utawala bora ni mtihani katika vyama vya siasa hasa vya upinzani kwani baadhi ya vyama vya siasa ikiwemo ACT Wazalendo kilishindwa kuzingati taratibu mbalimbali ikiwemo kuitisha mikutano ya Bodi ya wadhamini, kufanya matumizi ya fedha kwa kuzingatia sheria na taratibu nba kutoendeshwa kwa uwazi.

“Chama cha ACT Wazalendo kilifanya mkutano mmoja tu (1) kati ya mikutano 14 kwa mujibu wa miongozo ya Bodi ya Wadhamini hivyo hiki ni kiashiria kuwa chama hiki ni kama asasi ya Kiongozi wa Chama hicho,” anasema mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili katika Baiashara kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiichambua ripoti hiyo.

“Hii ni aibu ya mwaka kwa sisi wafuasi wa siasa za upinzani. Kama tunapigania uwazi halafu hatujui hata jinsi ya kuutekeleza; tunapigania utawala bora halafu sisi wenyewe hatuutekelezi itakuwaje siku tukiingia madarakani kuongoza nchi kubwa hivi?” amehoji mwanachama wa Chadema, Peter Kisoki wa Mbeya Mjini.

Naye Omari Baruan wa Kisarawe akijitambulisha kuwa mfuasi wa CUF alisema: “Nimemshangaa CAG hakuikagua CUF akisema ina mgogoro, yeye angekagua waliopokea ruzuku tujue matumizi yake basi.

“Lakini kwa ujumla ripoti hii, ukiaxcha siasa, imeutia aibu upinzani. Hatujawahi kuona madudu ya wapinzani hivi. Mara zote tumesikia ya Serikali na hatua inazofanyiakazi. Najisikia aibu sana kuwa mfuasi wa upinzani. Naomba CAG aendelee kukagua hivi hivi kila mwaka tujue zaidi kuhusu vyama hivi vya upinzani.”

*Chadema, ACT Wahaha Kujinasua*

Badala ya kufanyiakazi madudu yaliyobainishwa katika taasisi zao, vyama viwili vya upinzani vimejitokeza hadharani kufanyia siasa ripoti ya CAG. Kiongozi wa Chadema Benson Kigaila yeye amedai gari wanalodaiwa kuliandikisha kwa jina la mwanachama ulikuwa mkopo.

“Tulimkopesha mwanachama (hakumtaja jina) ili alipe taratibu lakini gari lilibaki kwa Chama kwa makubaliano apewe akishamaliza kulipa mkopo,” alidai bila kuzungumzia magari mengine mawili ambayo hayaonekani.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Chama cha ACT, Zitto Kabwe alikwepa kuzungumzia masuala ya Halmshauri yake kupata hati chafu wala fedha ambazo hazionekani katika chama chake, badala yake, akaendeleza utaratibu wake ule ule wa kuilaumu Serikali.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
@blix22 kuhusu zile Billion 3 ambazo CCM hawakuwasilisha NSSF vipi wananchi hawajasema chochote?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom