Ufisadi Madhara Yake Haya hapa

Ufunuo wa Yohana

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
318
67
Jambo F mnatisha mno!!!
Tanzania imegubikwa na mtandao mpana wa ufisadi ambao hata kuuelezea inagharimu mno lakini ipo siku moja tutauondoa. Lakini hebu niseme hivi watu wasiojua madhara ya ufisadi naomba mjifunze ktk huyu!
Mzee mmoja alikuwa na wadhifa mkubwa sana katika mkoa wa Tabora na alikuwa na wanawe watatu ambao walikuwa wanasoma katika shule ya msingi hapo Tabora. Mwaka 1975 mtoto wakwanza alifika darasa la saba wakafanya mtihani akafeli lakini kwa kuwa alikuwa mtoto wa mkubwa wakatafuta jina la mtoto mmoja kule kijijini aliyekuwa amefaulu tena sana mtoto wa masikini wakachukua nafasi yake akaenda sekondari Tabora boys.Yule mtoto wa maskini hata hakujua kilichofanyika akaendelea na maisha yake ya kulima ikiwa ni pamoja na kuoa na kuzaa watoto. Yule mtoto wa bopa akaibiwa pepa form four napo akafaulu hali kadharika na form 6. Alipomaliza form 6 serikali zamani sio sasa ilikuwa na utaratibu wa kutoa schoolarship kwenda nje kwa watoto wenye kufaulu vizuri. Ingawa yeye huyo mtoto hakufaulu vizuli alipewa hiyo nafasi kuja kusoma Marekani na akaachwa tena mtoto wa maskini aliyefaulu sana kwa akili zake mwenyewe. Alifika marekani na kujichimbia kusoma na hakurudi nyumbani kwa kuwa alikuwa na usongo wa kusoma majuu ktk kipindi chote cha miaka 3 ya masomo. Wale wadogo zake nao mzee akafanya vile vile. Aliwapelekea pesa ambazo alikuwa akila rushwa za matumizi kwa watoto wake walio majuu. Alijitahidi kupata pesa kwa njia yoyote hata kwa kulaghai, kusaini cheque feki, kulipa mishahara hewa, kula pesa za misaada kwa masikini ili watoto wake kule majuu wasome. Alikuwa akitamba yeye anasomesha watoto wake majuu hata kwa viongozi wenzake na kufanya hata na wao waanze kufuata nyayo zake.

Mtoto wa kwanza alimaliza masomo akarudi nyumbani na mzee alienda uwanja wa ndege kumpokea ndege ilifika lakini hakumuona mtoto wake na alishtukia tu anaguswa na kijana mmoja nakuambiwa " hallo dingi mambo? mzee wa watu hakuitikia mara ya kwanza kijana akarudia dingi mambo tujikate basi home! mzee alitikisa kichwa na kuuliza wewe ndiye Maganga? kijana akajibu Maganga mwenyewe mimi siku hizi Mob Cruz. Mzee aliumia sana kwanza alikuwa na minyele ya ajabu amesuka cheni shingoni. Ukweli alikuwa ni teja tayari na hana namna ya kumsaidia. Mtoto wake wa pili wa kiume aliporudi alikuwa ni mtoto haliziki na mtoto wake wa tatu wa kike alikuwa changu wa kupindukia. Baadaye mzee alifariki kwa kuuawa na hao wanae ili warithi mali. Walizigawana mali zote na zikawaishia na sasa hao vijana ni mateja na wezi na dada yao ni changu na mhudumu wa baa maarufu sana sinza.

Asignment.
Chunguza watoto wote wa vigogo hasa mafisadi waliokuwa madarakani na ambao wamestaafu uone jinsi maisha yao yalivyo.

Madhara ya rushwa yanaweza yasikupate wewe mwenyewe lakini yakaathiri ukoo wako, taifa lako na jamii yako. madhara haya ya viongozi kusaini mikataba hovyo yanagharimu taifa kwa kuachwa kusomeshwa watoto wenye akili nzuri walio vijijini masikini na kusomesha watoto wa vibopa vihiyo wasiojua kitu. Tafuteni historia ya viongozi wetu hasa hawa wanaofanya vibaya na kuangamiza taifa wazazi wao walikuwa akina nani na walifanya nini! Hapo mtapata majibu kwa nini raisi anabeba cheque yenye utata mbele ya umati mkubwa naye anacheka. Vihiyo tunao wengi mno selikarini. Nakutahadharisha wewe unayeendelea kura rushwa au unapanga kuja kula rushwa mali zote unazozikusanya hazitakusaidia hata kidogo badala yake zitakutokea puani wala hutakuwa na amani ktk nyumba yako. Itakuwa kila siku ugomvi kati yako na mke wako au na watoto ambapo mara nyingi husababisha nyumba nyingi kuvunjika na kuanza kudandia malaya. Angalia watu wote waliohujumu uchumi na wanaoendelea kuhujumu uchumi familia zao na maisha yao ni mabaya hata kama wanaendesha benz na Prado ni makopo matupu.

Ndugu zangu Watanzania ufisadi ni mbaya sana na huu ni wa yule shetani mwovu kajaa ktk vichwa vya watawala. MUNGU NI MWEMA TUMUOMBE YEYE NA ATATUSAIDIA WANA JF KWA KAZI HII NGUMU YA KUWATOA WTZ KTK WIMBI HILI LA MAFISADI

MUNGU IBARIKI JF
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRIKA
AMEN
 
Maneno mazito hayo mkuu. Mwenye macho haambiwi tazama.
 
Ufunuo,
maneno yako na kisa chako sijui ni cha kweli ama cha kutunga lakini maudhui yake ni makubwa sana!

Kwamba Pesa /mali zozote zile zinazo patikana kwa njia isiyo halali hasa ya kuwaibia watu masikini walio stahili haki hiyo zime jaa laana,
Na kwamba mtu akitumia madaraka aliyo pewa na wananchi kuwaibia ama kuwa dhurumu haki yao ya msingi.. siku zote Mungu huingilia kati na kumpatiliza huyo zurumati, na ndo maana watanzania tumeshuhudia visa vya ajabu vya ajali na mikasa juu ya baadhi ya wabunge wa CCM walio shiriki kwa namna moja ama nyingine kunyamazisha sauti za watetezi wa wanyonge bungeni.

Ndiyo maana tuna zidi shuhudia wanavo jichanganya katika kauli zao na utendaji wao hadi wanaonekana vituko mbele ya umma!

MUNGU NI MWEMA SIKU ZOTE!!
 
Mtoto wa pili alikuwa 'haliziki'...mleta uzi kama uko hai njoo unifafanulie.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom