Ufisadi Lazima Ufe!

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,868
22,327
Ufisadi lazima ufe

2008-07-04 09:28:38
Na Jackson Kalindimya, Dodoma

Wabunge wamewashambulia mafisadi kwamba mtandao wao umejengwa katika nguvu ya maslahi ya fedha na wametaka ung�olewe na kuuawa kabisa. Pia wamesema kuwa kuna haja ya kuuvunja mtandao huo uoze na kusahaulika.

Mbunge wa Kasulu Magharibi (CCM), Bw. Kilontsi Mporogomyi alisema lazima watawala waache kuamini katika nguvu ya fedha bali nguvu ya hoja maana fedha ni ya muda tu.

Bw. Mporogomyi alisema, mwelekeo wa sasa ni kuvunja mitandao ya ufisadi ili kukisafisha Chama Cha Mapinduzi.

Uhusiano wa wana mitandao haukujengwa juu ya imani wala uelewa au dhamira na maelewano ya dhati, bali katika maslahi yapitayo, yaozayo na kusahaulika. Tushughulikie mafisadi alisema.

Alimpongeza Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, kwamba ameonyesha uwezo mkubwa katika kuyajua masuala muhimu na makubwa ya kitaifa na kimataifa na kwamba majibu yake kwa sasa ni makini na kwa msingi huo serikali ni makini zaidi.

Naye Mbunge wa Mbozi Mashariki, Bw. Godfrey Zambi (CCM), aliwahimiza wabunge wote kupiga vita ufisadi ili iwe ajenda ya kudumu.

Alisema mabilioni ya fedha yanapotea kwa njia za ufisadi na hata kusababisha serikali kushindwa kuwahudumia vyema wananchi ili kusukuma kasi ya maendeleo.

Watanzania watatuelewaje tusipouzungumzia ufisadi. Hivi tukiulizwa kwa nini tunalala hatuzungumzii ufisadi tutakuwa na majibu gani? Tuongeze mapambano ya ufisadi bila ya kuogopa.

Na wanaotuhumiwa kwa ufisadi sheria zichukue mkondo wake,`` alisema.

Mbunge Zambi aliipongeza serikali kwa kutenga Sh. bilioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege Songwe, Mbeya kwamba utachangia kurahisha maeneo ya ukanda wa kusini ikiwa pamoja na kufanikisha lengo la kuwa na ukanda maalum wa uchumi katika eneo hilo.

Akigusia kuhusu Mamlaka ya hali ya Hewa (TMA), alisema kwa sasa ofisi yake imepanga katika jengo la Ubungo Plaza ambapo wanalipa Sh. milioni 400 kwa mwaka na kushauri ni vyema ukaandaliwa utaratibu wa kudumu wa kujenga ofisi na hivyo kuokoa fedha za serikali.

Kuhusu bandari ya Dar es Salaam, Bw. Zambi, alisema ni muhimu ikaimarishwa, kuondoa urasimu na kupunguza msongamano kwa kuimarisha reli ya kati ili iweze kutumia kikamilifu kuinua uchumi wa nchi vinginevyo maendeleo ya nchi ni ndoto.

Mbunge Mporogomyi alisema kama serikali itaimarisha miundombinu ya Mkoa wa Kigoma ikiwemo reli, barabara na uwanja wa ndege kuna fursa kubwa kwa mkoa huo kulitosheleza taifa kwa chakula kwa sababu ardhi ya mkoa huo ni nzuri na wakazi wa mkoa huo wana nguvu na wachapakazi.

Alisema ujenzi wa daraja la Malagarasi mkoani Kigoma utafungulia neema kubwa kwa mkoa huo ambao una hadhi nzuri unaostawisha mazao mengi lakini hayafiki sokoni na wakulima kunufaika na kilimo chao.

Aidha, alishauri kuwa, kukamilika kwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma kutafanikisha mkoa huo kuwa kituo kikuu cha biashara katika ukanda wa Maziwa Makuu.

``Mji wa Kigoma umeainishwa na Benki ya Dunia (World Bank) kuwa ukijengewa miundombinu yake vyema utaongeza utalii kwa kasi na kupunguza umasikini wa wananchi wake,`` alisema. Bi. Joyce Masunga (CCM-Viti Maalum), akichangia mjadala huo alisema kuwa ni muhimu sana barabara za mkoa wa Tabora ambazo ziko katika hali mbaya zikajengwa ili kuwapunguzia mzigo ili kuwatua na usemi usemao ``mzigo mzito mpe mnyamwezi akubebee.``

Mbunge wa Liwale, Bw. Hassan Kigwalilo (CCM), aliiomba serikali ipige marufuku biashara ya vyuma chakavu kwa sababu inasababisha hujuma ya reli na madaraja.

Alishauri ni vyema Mbunge mmoja wa kusini awe mjumbe wa
Bodi ya Mamlaka ya Bandari Mtwara ili kusukuma kasi ya maendeleo ya bandari hiyo na eneo hilo kwa ujumla.

Wabunge hao waliyasema hayo wakati wakichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Miundombinu kwa mwaka wa fedha 2008/9.
  • SOURCE: Nipashe
 
Watanzania sasa ni wakati wa kuwaunga mkono wabunge wote BILA KUJALI CHAMA,DINI WALA KABILA!
MAFISADI WOTE WANAJULIKANA NA KAMWE HATUTAKUBALI WANANCHI WAWAPIGIE KURA KABLA HAWAJAJIBU TUHUMA ZAO MBELE ZA BUNGE NA MAHAKAMA!
 
UFISADI lazima ufe as far as ulizaliwa!hakuna mtu anazaliwa fisadi
 
UFISADI lazima ufe as far as ulizaliwa!hakuna mtu anazaliwa fisadi

Ufisadi utakufa kwa kuwasafisha kwasababu eti hawakuzaliwa mafisadi?
Ufisadi ufe vipi kwa kusafishana?
Vipi kuhusu sheria?
 
Ufisadi hautakufa kama haitapatikana Tanganyika huru yenye mamlaka yake ya ndani kwani ufisadi huu unachochewa kwa kuwepo na Muungano na hivyo mafisadi wanajificha na Chama chao kwenye kivuli cha Muungano ambao Mafisadi wa CCM bara wanaulinda kwa nguvu zao zote kuhakikisha kuwa hauchezewi wala hauguswi na mtu na kutishia kwa yeyote atakae dai kuvunjwa basi huyo ni adui wa Taifa.
Mafisadi wanapeleka majeshi Zenji wanapeleka polisi zenji wanapeleka mamluki Zenji wanaamrisha mapolisi kukimbiza masanduku ya kura yote ni kujilinda na tatizo la kupoteza nguvu ya Zanzibar ndani ya mtandao wao , mafisadi wanawachomeka wahafidhina kwa malipo ya kuwapatia kura zao zote ndani ya kinyang'anyiro cha uchaguzi ndani ya NEC na tiketi ya kuupata Uraisi wa Tanzania.

Hivyo kuwamaliza mafisadi na kuwatokomeza ni kuondoa uchafu huu wa Serikali ya Muungano iliyopo ,vipi itaondolewa ? Bila ya kuvunja Muungano idaiwe serikali ya Tanganyika ,hapo ikishapoatikana itabidi ufanyike uchaguzi mkuu mpya kumpata raisi wa Tanganyika huru yenye mamlaka yake ya ndani.
Kitakachotokea ni kusambaratika kwa mafisadi kugawanyika kwa CCM kwenye chaguzi zake kwa upande wa Tanganyika ule mwega wa kutegemea kura za wahafidhina utakuwa haupo tena ,mimi naamini kabisa mwega ule wa wahafidhina unawaumiza sana wengine ndani ya CCM kwani unatumika kimtandao na baada ya hapo ukimalizika Uchaguzi Mkuu wa mwanzo wa vyama vingi Tanganyika ndipo tutakuja kwenye Serikali ya Muungano ambayo kwa kutmia vile vigezo 11 vya mwanzo kwa kuanzia na kuvifanyia marekebisho kutokana na kuingia serikali ya Tanganyika.Ni mapema kujadili yote hayo kwanza na tulifanye hili ambalo akina Kikwete na wenzake walikwisha fika mbali sana sana na leo hii kama wangefanikiwa kulivusha basi naamini Tanzania ingekuwa ya kupigiwa mfano.
Tuanzie walipopafikisha na ikihitajika tutawakopa mikakati waliyopitia hata wakafanikiwa na kwa hali ilivyo leo walipoishia ni rahisi kupavuka.
 
Maneno matupu ya pinda na wabunge hayatavunja mfupa.Kuna maana gani pinda kuongea kwa umahili na hakuna yoyote inachukulia. Mwana Jf yoyote aniambie ni hatua gani pinda alichukua nami nitatoa pongezi.Otherwise hamna kitu.

Na wabunge tuwapongeze kwa lipi???. Hawajaibana serikali kisawasawa.Ilikuwaje wakapitisha bajeti ya PM wakati hakutoa majibu ya kueleweka kuhusu hoja nzito zilizomo hotuba ya dr. slaa kuhusu ufisadi
 
Kuna waliko upande mzuri watakaoshirkiana na wazalendo...Only kama si wanamtandao!
Na pia quote hio hapo chini ndiyo maneno niliyozingatia haswa haswa kwenye kummaliza ufisadi kwa sheria!

Naye Mbunge wa Mbozi Mashariki, Bw. Godfrey Zambi (CCM), aliwahimiza wabunge wote kupiga vita ufisadi ili iwe ajenda ya kudumu.

Alisema mabilioni ya fedha yanapotea kwa njia za ufisadi na hata kusababisha serikali kushindwa kuwahudumia vyema wananchi ili kusukuma kasi ya maendeleo.

Watanzania watatuelewaje tusipouzungumzia ufisadi. Hivi tukiulizwa kwa nini tunalala hatuzungumzii ufisadi tutakuwa na majibu gani? Tuongeze mapambano ya ufisadi bila ya kuogopa.

Na wanaotuhumiwa kwa ufisadi sheria zichukue mkondo wake,`` alisema.
 
Ufisadi kuuwawa ni kitu kinachowezekana lakini inaelekea nia haipo,Ni kweli huu mtandao c mchezo unaanzia hukohuko juu.
ukitaka kuthibitisha hayo angalia ni muda gani umepita tokea zilipotolewa ahadi za wakati gani mambo ya richimonduli na Epa yatakuwa yameshughulikiwa,
Siku zaenda tu nafikiri ni mbinu ya kuvuta muda wananchi wasahau [/I][/I][/I]
 
Siku zaenda tu nafikiri ni mbinu ya kuvuta muda wananchi wasahau [/i][/i][/i]

Na sasa ni mijadala ya ukabila na udini na watu hawapendi wengine wachangie na wanachongea wengine tufungiwe!
Yani mimi kukemea tabia ya ukabila na udini iliyotapakaa kwenye threads na nikipost kitu cha kupingana na hoja hizo...Basi watu wanalalamika nifungiwe!
Na mimi ninawajuwa watu hao na sitagusa thread zao ten ila na mimi najuwa thread za kuanzisha!
Mambo ambayo nimshafanyiwa hapa jf ni nani wa kumlalamikia mwenzake?
Watu kukufuata hadi kwenye profile na kukukemea kama mtoto na MODS HAMUONI HILO?
 
Ufisadi kuuwawa ni kitu kinachowezekana lakini inaelekea nia haipo,Ni kweli huu mtandao c mchezo unaanzia hukohuko juu.
ukitaka kuthibitisha hayo angalia ni muda gani umepita tokea zilipotolewa ahadi za wakati gani mambo ya richimonduli na Epa yatakuwa yameshughulikiwa,
Siku zaenda tu nafikiri ni mbinu ya kuvuta muda wananchi wasahau [/I][/I][/I]
Walivuta muda,karibia na uchaguzi wakakarabati jela na mikwala kibao.Wakashinda.

Usanii ulipogundulika,wakaja na kujivua magamba,naona hiyo ni gia ya 2015,ufisadi bado unashamiri tu na hakuna aliyewajibika zaidi ya michanga ya macho na kuchanganya watu kwa kutumia karata za udini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom