Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi kwenye Kamusi {Dictionary}

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nikupateje, Nov 14, 2010.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nimeamua kutoa darasa kuhusu hizi mnazoita kamusi ambazo kwa kiingereza huitwa "dictionary". Naamini wanopenda tujione hatuko sahihi kimbilio lao ni kamusi.

  Lakini wasidhani hizo kamusi sisi hatuzisomi na nitakapomaliza hii post ndipo tutaona kuwa Dr. Slaa alikuwa sahihi alioptumia msamiati huo na wanaotaka tuubadilishe ni wavivu wa kutafiti.

  Hapa nilipo nimeshikilia "Oxford Advanced Learner's Dictionary-New 7th Edition". Kwenye ukurasa wa vii utaona Proffessor Henry Widowson ameandika foreword akieleza mabadiliko ya maneno. Ameeleza kwamba first edition ya dictionary kama hii ilitoka miaka 250 iliyopita.

  Hivyo akawaasa wasomaji wa hii edition kwamba wasishingae kukuta edition hii maneno yana tafsiri tofauti na zile previous editions.

  Maana yake ni nini? Anakiri wazi jamii ndiyo yenye mamlaka ya kubadili maana na matumizi ya neno. Inaelekea mama Makinda hajui au hasomi vitu rahisi kama hivi.

  Tunajjijua watanzania ni wavivu kil sekta na huenda uvivu huu umewafanya hata walio-update kamusi kushindwa tafiti hizi ndogo.

  Wana-kiswahili wasingekuwa wavivu wa kutafiti leo hii neno "walokole" lingekuwa limeshaingizwa kwenye kamusi.

  Nimalizie kwa rejea nyingine ambayo ni "A standard Swahili-English Dictionary, Edition 2008" kwenye ukurasa wa 97. Humu neno fisadi limetafsiriwa kwenda kwenye kiingereza kama ifuatavyo:

  Fisadi: a corrupter, especially of women, seducer, immoral person.

  Wote tuchambue definiton hii.

  Maneno ya msingi ni yale niliyoyakolozea na rangi ya red. Hivyo neno corrupter, seducer, na immoral person ni maneno yanayojitosheleza kwa kutoa definition ya neno fisadi.

  Mbele ya neno corrupter kuna statement isemayo especially of women. Basi hapa ndipo wengi wanataka tukazanie kama ndiyo maana mpya ya neno fisadi lakini wanaofanya hivyo ni kwa mapenzi yao na si mapenzi ya dictionary.

  Ingekwa ni mapenzi ya dictionary basi hapa pangeandikwa {a corrupter of women}, lakini hapa ni wazi pameandikwa {a corrupter, especially of women}.

  Tofauti hapa ni kwamba neno ?? ni msisitizo unaoonyesha kwa mara nyingi fisadi inamaanisha ku-corrupt mwanamke. Hii ni tahadhari kwa mtumiaji kwamba asiishie kudhani fisadi ni corrupter tu bali kuna sehemu ataenda na kukuta fisadi ina maana ya kuchukua mwanamke. Na hapo ni kumchukua mwanamke yeyote, awe ameolewa au hakuolewa.

  HIvyo hii statement especially of women hata isingekuwepo isingefuta maana ya kwanza yaani fisadi ni corrupter. Ndiyo maana kwenye neno immoral hakuweka gender emphasisi yoyote kwani immoral ni mtu asiye muadilifu.

  Tukumbuke kwamba Dr. Slaa alitumia msamiati huo pale Mwembeyanga. Mnaotaka tuamini maana mpya ya ufuska basi watajwa wale walitakiwa kufungua mashtaka kwa kesi ya kusingiziwa ufuska kama waliona cha moto kufungua ya kukashifiwa kwa fedha za EPA.

  Kesi ingekuwa rahisi sana. Ni kiasi cha advocate kumuuliza Dr. Slaa ebu taja wanawake waliofanyiwa ufisadi na mafisadi unaowadai. hakuna aliyedokeza kushitaki kwa dai hilo badala yake waote walikazania kutishia kushtaki kuhusiana na fedha.

  Mimi nimefurahishwa na kauli ya Spika wa zamani Samwel Sitta alipomwambia Anna Makinda kwamba bunge la sasa hivi lina changamot kubwa. Moja ni kwamba sasa hivi watu wana uelewa mkubwa. Sitta alijua anamaanisha nini nadhani hakutaka tu lakini angeweza kusema yeye mwenyewe yalimkuta alipoletwa hoja ya EPA akaipga chini et kwa vile ni ushahidi wa internet.

  MImi naona hapa Sitta anakiri kabisa usidhani watu kushinda kwenye Jamii Forum au blogu hawana kazi. Hukohuko ndiko kwenye vyanzo vya uelewa na vyanzo vya kuumbuana.

  Haikupita masaa mama yetu (kimuri ni mama yangu) Anna Makinda hakuzingatia ushauri wa Sitta akaja na definition yake ya ufisadi. Inaelekea Anna Makinda haju mitandano ina-search haraka na haikupita siku nzima watu tayari wameshafukua hotuba yake ya mwaka juzi alipowakemea wanaowatetea mafisadi.

  (Link hii hapa: www.freemedia.co.tz/daima/2008/7/7/habari3.php)

  Huyu mama yetu na wengine dada yenu huu ni mfano tosha kuwa akicheza ni kizazi chetu matokeo yake ataona jamii inamchukia wakati ni yeye mwenyewe anashindwa kuwa muangalifu.

  Hata waiosoma JF si lazime waje humu. Kauliza zake mbili ni rahisi kuzituma kwa marafiki walioko kwenye simu yako na kama hawaamini kuwa Makinda aliwahi kutaja vile basi waape na website kwenye simu zao ili wakienda internet cafe wakajionee na kama simu zao zina internet mchezo unaisha mapema.

  Na nyinyi mnaotete humu JF, mara ningine mnadanganyika na majibu ya mkato na utani au matusi yasiyo na hoja. Matokeo yake mnadhani JF ni mfuriko wa kigenge cha wasio na hoja.

  Zinapokuja data kama hizi sijui utetezi wenu unakuja kwa misingi gani.

  Narudia mama Makinda ajue kwamba dunia ya sasa hauwadanganyi watu hata kwa saa moja kama ulishawahi kutoa kauli tofauti hata miaka 10 iliyopita, na kusoma vitabu wapo tunasoma asivyodhani.
   
 2. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #2
  Nov 14, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 469
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Swahili to English - 10 results in 1.83s.
  5 suggested literal translations
  • corrupt person
  • libertine
  • seducer
  • destroyer
  • evil person

  5 definitions
  fisadi (fisadi) { corrupt person } noun detailed view
  fisadi (fisadi) { libertine } noun detailed view fisadi (fisadi) { seducer } noun detailed view fisadi (fisadi) { destroyer } Swahili: fisadi

  [​IMG]
  Noun Class/Verb Class 5/6an
  Part of Speech noun
  Terminology general
  English Plural corrupt people
  English Headword corrupt
  English Word corrupt person
  Regular Plural mafisadi

  [​IMG]ReviewedCite
  fisadi. . In Swahili. Retrieved 12:44 AM June 23rd, 2008, from fisadi - Swahili | fie.nipa Dictionary
   
 3. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,369
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ukichukua maelezo, kamusi zote mbili utagundua muafaka mmoja kuwa Mtu Fisadi;
  Ni Mwanadamu aliyepoteza UTU wake!..."This is human disoder"

  Muathirika huwa anajisikia mtupu na aliyefilisika kimwili na kiufahamu ...
  Na atajitibu au atajikamilishaje kwa kile kilichopotea ndani yake..?

  Atafanya yote yaliyoelezwa kwenye kamusi...corrupt, seducer, esp of women etc
  Mh Speaker aelimike kuwa Fisadi ni tatizo la kiutu na kibinadamu lenye dalili zaidi ya moja...
   
 4. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mfano halisi wa nchi iliyotafunwa kwa ufisadi ni TANZANIA......nani anabisha????????????????
   
 5. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,500
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  nashukuru wadau kwa ufafanuzi na rsferences..........
   
 6. m

  mchotamaji JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2015
  Joined: Sep 22, 2015
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninaomba kwa wenye ufahamu mpana watupe tafsiri sahihi ya neno "FISADI" Tafsiri hiyo itatusaidia watanzania kujua maana sahihi kuliko sasa kwani neno hili limekuwa linatumika isivyo sahihi.
   
Loading...