Ufisadi katika wilaya ya Kigoma (v) Idara ya Elimu

mnyonge wa hali ya chini

JF-Expert Member
Feb 12, 2017
869
1,000
Kwa wahusika, tarehe 10 na 11 kulikuwa na mitihani ya Mock drs la 7 ambapo kila shule iliamliwa kutoa sh. 5000/= kwa kila mwanafunzi wa darasa la 7.

Kuna shule moja ina wanafunzi 60 wa drs la 7, hivyo walitoa Tshs 300,000/= kutoka kwenye fedha ya uendeshaji wa shule kifungu cha mitihani ambacho ni asilimia 10 (10%).

Sasa ajabu ni kuwa asilimia 10 ya fedha inayotolewa kwenye shule hiyo kwa mwaka mzima ambayo ni fedha ya mitihani kwa madarasa yote ni Tshs 340,000/= tu.

Hii inamaana kuwa fedha iliyobaki kwa ajili ya mitihani ni Tshs 40,000/=tu ambayo kimsingi haiwezi kutosha kwa maandalizi ya mitihani ya mwaka mzima kwa madarasa yote.

Lakini kinachoshangaza zaidi ni kuwa wilaya nyingine wamechangia kiasi kidogo tofauti na wilaya ya Kigoma vijijini mfano wilaya ya Uvinza wamechangia Tsh 1900/=kwa kila mwanafunzi, Kasulu Tsh 1000/= kwa kila mwanafunzi Kakonko Tsh. 1200/= kwa kila mwanafunzi.

Cha kushangaza zaidi ni kuwa ndani ya wilaya hizi zote wasimamizi wa hiyo mitihani wamelipwa Tsh.10,000/= kwa siku.

Wahusika liangalieni hili kwa jicho la tatu.

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
 
k-star

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
538
500
Huku kwetu kila mwanafunzi ni sh 750/=.
Haoo wanaotoza sh 5000 kwa @ mwanafunzi ni majipu hayo yanatakiwa yatumbuliwe upesi haraka sanaa mkuu.
 
Cannibal OX

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
2,853
2,000
Kwa wahusika, tarehe 10 na 11 kulikuwa na mitihani ya Mock drs la 7 ambapo kila shule iliamliwa kutoa sh. 5000/= kwa kila mwanafunzi wa darasa la 7.

Kuna shule moja ina wanafunzi 60 wa drs la 7, hivyo walitoa Tshs 300,000/= kutoka kwenye fedha ya uendeshaji wa shule kifungu cha mitihani ambacho ni asilimia 10 (10%).

Sasa ajabu ni kuwa asilimia 10 ya fedha inayotolewa kwenye shule hiyo kwa mwaka mzima ambayo ni fedha ya mitihani kwa madarasa yote ni Tshs 340,000/= tu.

Hii inamaana kuwa fedha iliyobaki kwa ajili ya mitihani ni Tshs 40,000/=tu ambayo kimsingi haiwezi kutosha kwa maandalizi ya mitihani ya mwaka mzima kwa madarasa yote.

Lakini kinachoshangaza zaidi ni kuwa wilaya nyingine wamechangia kiasi kidogo tofauti na wilaya ya Kigoma vijijini mfano wilaya ya Uvinza wamechangia Tsh 1900/=kwa kila mwanafunzi, Kasulu Tsh 1000/= kwa kila mwanafunzi Kakonko Tsh. 1200/= kwa kila mwanafunzi.

Cha kushangaza zaidi ni kuwa ndani ya wilaya hizi zote wasimamizi wa hiyo mitihani wamelipwa Tsh.10,000/= kwa siku.

Wahusika liangalieni hili kwa jicho la tatu.

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
Rudi tena ufafanue zaidi huo ufisadi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom