Ufisadi katika nchi za Afrika ni kama utamaduni wetu. Nani hasa mkombozi wa Afrika?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Muda wa saa 2.32 Usiku nilikuwa naangali taarifa ya habari kituo cha Televisheni cha ITV.

Wakati naendelea kutazama nikabahatika kuona na kusikiliza kuhusu UFISADI wa Benki Kuu ya Uganda (BoU).

Wajumbe wa kamati ya Bunge kwamba wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Benk hiyo ,watumishi wa Benk Kuu walinunua peni (biki /kalamu) 35 za kuandikia kwenye sherehe hiyo kwa gharama ya Shilingi milioni 125 fedha za Uganda Yaani ni sawa na peni moja ilinunuliwa Kwa fedha za Uganda zaidi ya shilingi milioni nne ( 4,000,000/=).Huu ni ufisadi.

Kamati ya Bunge ilipomtaka Naibu Gavana wa Benk Kuu ya Uganda kuleta nyaraka na sampuli ya peni hizo zilizonunuliwa Kwa gharama hiyo alibaki kujiumauma tu mbele ya kamati.

Nchi za Afrika zina changamoto na matatizo makubwa ya uhaba wa maji, umeme, miundombinu, umaskini uliokithiri, elimu duni na matatizo chungu nzima lakini Benki Kuu ya Uganda inafanya Ufisadi Kama huo na ni rahisi tu sakata hilo likaisha Kienyeji Kwa wahusika kutowajibishwa kabisa au kulindwa na wanaoitwa wakubwa. Inakera na kuumiza.

Nani atukumboe Waafrika?? Ni kweli Waafrika wazalendo na viongozi wazalendo walikua akina Julius Nyerere, Nelson Mandela, Patrice Lumumba, Jommo Kenyatta, Kamuzu Banda, Kaneth Kaunda, Michael Samora,Joshua Nkomo, Kwame Nkrumah, Milton Obote, Augustno Netto na wengine pekee??. Kwamba watawala wa Afrika wa sasa wote ni wabinafsi, mafisadi, matapeli wa kisiasa na madikteta???

Ni nani atasema na kutetea maskini wa Afrika ambao mlo mmoja Kwa siku ni taabu kuupata?. Nani atawatetea machinga wanaoteseka na kufukuzwa na mgambo na Polisi?. Nani atasimama na kuwasemea mama wajawazito wanaopoteza maisha Kwa kuwa vituo vya afya na zahanati hazina umeme kwa nyakati za usiku? .Nani atawatetea mamantiliye wanaoitwa uchafu katika miji ya bara la Afrika?. Nani atasema na kuwatetea wananchi wachimbaji wadogo wadogo wa madini kule Geita, Kahama, Chunya, Tarime, Nzega, Mererani, Kabulo na kwingineko?. Nani atasimama kulia na walimu na polisi wanaoonjeshwa posho zinazoitwa mishahara?. Nani atapinga ufisadi huu mkubwa ili dawa zipatikane katika hospitali za umma?? Nani atakomesha udikteta na uvunjaji wa sheria na katiba wa nchi za Afrika unaokiuka utawala bora au utawala wa sheria??

Kwa nini Afrika tunafanya ufisadi kuwa utamaduni wa kawaida katika nchi zetu???. Marais wa Afrika walio madarakani na waliostaafu wamejilimbikizia mali na utajiri mkubwa ndani ya nchi zao na nje. Mawaziri wakuu, mawaziri, wabunge na wanasiasa kwa nini wanafanya ufisadi na kuwaacha wananchi wao katika madimbwi na matope ya UFUKARA??

Afrika jamani. Nani wa Kizazi cha leo atasimama kusema haya na kuyakataa hadharani?. Ni Freeman Mbowe na Tundu Lissu pekee?. Je ni Kizza Besigye pekee?. Joseph Malema au Raila Odinga?. Ni nani hasa anaweza kutetea wananchi???. Au ni kweli kwamba "The Beautiful Ones are Not yet Born?? ".Ooooooo au wakoloni wekundu warudi kutawala Kwa kuwa hawa wakoloni weusi ni hatari zaidi, makatiri zaidi, wanyonyaji zaidi na matapeli zaidi??

Oooooooo nimekumbuka, Afrika inahitaji Vijana,Wazee,Wanawake na hata Watoto wazalendo wasio na chembechembe zozote za uoga kuungana na kudai maendeleo na haki. Tundu Lissu anafanya hivyo Tanzania .Kizza Besigye anafanya hivyo Uganda. Joseph Malema anafanya hayo Afrika Kusini. Wewe na mimi tunasubiri nini kusimama na kutetea Taifa na bara la Afrika?

Kwa nini mimi na wewe hatulipi deni tunalodaiwa na mataifa ya Afrika?. Tumeruhusu Ufisadi kutamalaki. Tumeruhusu Uonevu na unyanyasaji kutawala na wananchi kuteseka. Tusimame na kupinga haya. Tuhoji kwa pamoja kwa umoja na mshikamano. Afrika ni moja.
 
Back
Top Bottom