Ufisadi: Je - Tanzania inahitaji yaliyotokea Ghana 1979? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi: Je - Tanzania inahitaji yaliyotokea Ghana 1979?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jul 28, 2009.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Ufisadi: Je - Tanzania inahitaji yaliyotokea Ghana 1979?


  Wana-JF, na hasa wale wanaoupinga ufisadi kwa dhati naomba mtafakari iwapo nchi yetu imefikia mahala ambapo pengine linahitajika tukio kama lile la Ghana la June 1979 ambalo kwa kiasi kikubwa limetokea kuwa ni fundisho kubwa kwa mafisadi na wale wanaowalinda.

  Mapema mwezi huu Rais Barack Obama alitembelea Ghana, nchi ya kwanza kusini mwa Jangwa la Sahara kupata heshima ya kutembelewa na kiongozi wa Marekani mwenye chimbuko la Bara hili. Hakubahatisha katika kuichagua Ghana – na hasa kutokana na yale aliyoyatamka nchini humo kuhusu Afrika na viongozi wake. Aliwapasha kikweli kweli – kwamba wao ndio wahusika wa kwanza kwa yote yaliyo mabaya ndani ya tawala zao.

  Kwa hivyo asingeweza kutamka hayo kama angekuwa Tanzania, Nigeria au Kenya kwa mfano. Alichagua nchi angalau aliona inaweza kuwa mfano kwa wengine.

  Aliisifia sana Ghana kwa demokrasia iliyojijengea na inayoridhisha, uongozi mzuri na utawala bora, pamoja na udhati katika kupigana na ufisadi.

  Lakini yote haya hayakuja bure, kwani ule msemo usemao “Usione vinaelea, vimeundwa” unaelezea vizuri sana hali hiyo ya sasa ya Ghana.

  Baada ya kupinduliwa kwa Kwame Nkrumah mwaka 1966, Ghana iliingia katika kipindi cha tawala za kijeshi na za dhulma. Hata ule wa kiraia uliokuwapo kwa muda mfupi (wa Dr Kofi Busia mwanzoni mwa miaka ya 70) ulikuwa hivyo hivyo -- ufisadi na kulindana ulikithiri kwa kiasi kikubwa sana – kama vile ilivyo hapa Tanzania.

  Hatimaye mwaka 1979 serikali ya kijeshi ya Jenerali Fred Akuffo iliamua kurudisha utawala wa kiraia. Vyama vya siasa vikaruhusiwa, ikatayaarishwa katiba mpya na uchaguzi ukafanywa. Lakini kabla ya rais mpya wa kiraia, Hilla Liman kuapishwa, Luteni Jerry Rawlings wa kikosi cha Anga naye alifanya mapinduzi.

  Akawakamata majenerali wote waliokuwa wakipinduana huko nyuma, kuanzia Akwasi Afrifa, Ignatius Acheampong na Fred Akuffo na maafisa wengine watano. Mahakama maalum iliundwa, na kwa haraka haraka iliendesha kesi na kuwahukumu kuuawa kwa kupigwa risasi, tukio lililofanywa katika ufukwe wa Accra mapema June 16, 1979.

  Baada ya tukio hilo, tarehe 24 Septemba 1979 Rawlings aliruhusu utawala wa kiraia uendelee na hivyo Hilla Liman aliapishwa kuwa rais.

  Rawlings alisema ilibidi majenerali hao wahukumiwe vile kwa sababu siyo tu waliipora nchi na kuifilisi huku wakilindana, lakini pia walishinikiza kuwepo kipengele cha “kinga” katika Katiba ya Kiraia waliyoiunda, kwamba wasiweze kushitakiwa kwa makosa yoyote – ya rushwa na utawala mbovu – walipokuwa madarakani.

  Rawlings alisema alijitolea kufanya hivyo kwa sababu, ungeingia tu utawala wa kiraia, watawala wale wa zamani wasingewajibishwa, kwa maana ya kushitakiwa, wangeendelea kutanua na mapesa na mali waliziowaibia wananchi.

  Kwa hivyo utawala bora iliopo Ghana sasa hivi umetokana na fundisho kubwa la kihistoria lisilosahaulika na limekuwa kama “onyo kali” (deterrent) kwa wengine.

  Ingawa Rawlings alirudi kuipindua tena serikali ya Liman, hiyo haikuondoa kile alichokifanya kwa nchi yake, kubadilisha mwelekeo wa nchi yake liyoonekana ikienda kusiko, na kikubwa ni kupiga rungu kubwa ufisadi kwa vitendo na siyo kwa maneno.

  Sisemi kama ufisadi hakuna Ghana, upo, lakini unashughulikiwa vilivyo kwa vyombo husika vilivyo huru, visivyoingiliwa na mamlaka za juu. Hivi majuzi waziri wa Nje wa zamani chini ya utawala wa Rais aliyeondoka John Kuffuor alikamatwa kwa rushwa kuhusiana na uagizaji wa mchele kutoka nje. Alikamatwa kimya kimya bila hata ya umma kupiga kelele sana kwanza – kama ilivyo hapa kwetu.

  Kuna baadhi wanasema kitu kama hicho kingefaa pia hapa, kwani ufisadi umekithiri kupindukia, na kulindana kwa hali ya juu na kusafishana kwa wakubwa ndiyo umekuwa kitu cha kawaida na huku umma hauna nguvu zozote za kuweza kurekebisha mambo.

  Mimi naona tulijadili hili.


   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Naogopa kutoa maoni yangu yasije yakanipata yale yaliyompata yule Muiraq aliyesema Mwinyi kaliua azimio la Arusha na Mkapa kauza nchi.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kuwapiga risasi mafisadi si kitu kigeni, kwani China kuna utaratibu huo, ingawa mahakama huchukua mkondo wake kwanza. Kilichotokea ghana ni tofauti, mahakama ilikuwa ya kijeshi, bila ya watuhumiwa kujitetea n.k. Lakini pengine tukio limesaidia kuleta hofu kwa wale wanaofanya vitendo vya kifisadi.

  Cha ajabu ni kwamba jerry rawlings mwenyewe hajashitakiwa kutokana na tukio hilo la ukiukaji wa sheria. Huenda umma uliona kwamba matokeo yaliyotokana na tukio yalikuwa yenye manufaa makubwa kwa nchi hiyo.

  Ila inabidi niseme kwamba kitendo kama hicho si cha kuigwa pamoja na kwamba mafisadi wanaleta zahama kubwa sana katika nchi. Sheria lazima ifuate mkondo na umma daima ipiganie kuwapo kwa utawala wa kufuata sheria.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Zak,
  Sheria zinaweza tu kufuata mkondo wake katika nchi zinazoheshimu rule of law.
  Can we say the same about our beloved Tz?
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wapigwe risasi, hakuna njia nyingine. Nchi inaelekea kubaya sana, na hili si uongo, kudra tu ya Mwenyezi itatuponesha. Wakubwa wanalindana, wanasafishana kwa hujuma wanazotenda. Bora wafe wachache kuliko taifa zima kutumbukia katika farakano ambayo itachukuwa muda mrefu kulimaliza.
   
 6. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nchi yetu inahitaji utawala wa kieshi ili kuweka mambo yaende sawa.
  Hivyo mafisadi kushughulikiwa hadharini ni fundisho kubwa sana hasa
  kwa mfisadi ili wa aache tabia hiyo.
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hapa haiwezekani. Nigeria walijaribu kufanya kama Ghana ikashindikana kwa sababu waliodhamiria kukomesha ufisadi walitegemea zaidi kufuata sheria.

  Mwaka 1983 utawala wa kiraia wa Alhaji shehu shagari uliopinduliwa na jeshi, mapinduzi yaliyoongozwa na Muhammed Buhari na Ibrahim Babangida. sababu yao kubwa ilikuwa kama ya Rawlings, kukomesha ufisadi kwanu utawala wa Shagari ulijaa rushwa kupindukia. Uliingia madarakani mwaka 1979 katika uchaguzi ambao mafisadi walimchangia pesa nyingi ili ashinde.

  Na kweli, baada tu ya mapinduzi hayo, walikamatwa mawaziri kadha na maafisa wengine wa serikali na kufunguliwa mashitaka -- katika korti za kawaida. Baadhi yao waliweka wanasheria na kushinda kesi, lakini wengine walifungwa.

  Wachunguzi wa mambo walisema kuwa hiyo haikuwa fundisho tosha na ndiyo maana hadi leo hii ufisadi unaitafuna nchi hiyo yenye utajiri mkubwa lakini kuna umasikini wa kupindukia. sasa hivi Nigeria na Ghana ni kama usiku na mchana.
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kwa hapa bongo ni ngumu kwa sababu serikali inahakikisha wizara ya ulinzi ''wale senior staff'' hawana shida.wao wanatumika kuwamanage wadogo kwao.laiti kama dhuluma wanazofanyiwa walimu wa primary na sec wangefanyiwa wanajeshi....TUNGEWEZA KULIFIKIRIA HILO!

  kwa hapa bongo may be,MAANDAMANO MAKUBWA KAMA YA UKRAINE MIAKA ILE!
   
Loading...