zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,267
- 3,898
Ufisadi Tanzania haukuanzia awamu ya nne, ufisadi Tanzania umeanza wakati wa mkuu Nyerere na ndio unaendelea mpaka leo.
Ikiwa ni suala la BoT, sijasikia ikikumbushwa habari ya kuchomwa moto BoT wakati wa Nyerere, jee uchunguzi gani ulifanyika? au wale wenye umri wa kujuwa hilo hawamo humu? au limefutika kwenye historia kwa kuwa ilikuwa ni wakati wa "baba wa taifa" na yeye hana dhambi? (mimi nadhani yeye ni baba wa madhambi na si baba wa taifa) baba mwema hufanya kila njia akawapatia wanawe elimu nzuri, afya bora, mazingira mazuri ya kukuwa.) Na si kutuwachia mahospitali yananuka, mashule hayana hata vyoo, mazingira mabovu ya kukuwa, mpaka leo tunatamba na mavalio ya wazungu waliyoyachoka (mitumba)na masalio yamagari waliyayachoka wa japani. Hayo ndiyo aliyetuwachia bwana nyerere!
Kama mfumo unaotuongoza ndio huo, uliyeachwa na Nyerere, cha kushangaza ni nini? Ikiwa awamu ya kwanza ilikokowa BoT mpaka ikaichoma moto na hakuna kilichojiri baada ya hapo, tunategemea nini? au tumesahau methali ya kiswahili isemayo "mtoto wa nyoka ni nyoka".
Wanaoiongoza Tanzania ya leo ni aidha wale wale waliokuwamo toka awamu ya kwanza (kina Kingunge, Sitta, JK mwenyewe) na ndio haohao walioifanya nchi hii kuwa masikini wa kutupwa na ndio hao hao wanaozidi kutushindilia katika umasikini usio na mfano.
Nilipata mgeni kutoka mashariki ya kati mnamo mwaka 1991, katika kumtembeza nikampeleka Rufiji Kwa kuanzia, njiani akaniambia maneno ambayo mpaka leo sijayasahau, kwa mshangao aliniambia "hivi nilikuwa nasikia Tanzania ni nchi masikini, lakini kwa niionavyo hii mandhari tuu, naona kuwa umasikini wenu umo vichwani mwenu na si kwenye hii ardhi". Jee, si ukweli huo?
Nani hii leo ni nani asiyejuwa kuwa Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kwa utajiri usiyo na mfano, kuanzia bahari, mito, maziwa, ukijani (mazingira), madini na vito vya kila aina, gesi asilia, mafuta, ustaarabu, na mengine mengi ambayo nchi zingine "tajiri" nyingi tuu duniani hazina sifa zaidi ya moja katika tuliokuwa nazo sisi.
Jamani, ukiwa fisadi, huna unachovuna ila ni umasikini tu, kwani fisadi anataka apate na kulimbikiza yeye tuu kwa kudhulumu wengine wengi, baraka zitatoka wapi? Utajiri tunao lakini ni wa kuuona, kuusikia na kushuhudia wengine wakineemeka nao (si tunaona wazungu tuliowaita mabepari wakati wa nyerere wanavyorudi na kuvuna, tena kwa kuwabembeleza wenyewe, "njooni jamani, njooni muwekeze", sasa wanawekeza na kukomba kisawasawa).
Hii ni laana ya ufisadi aliyoianzisha Nyerere kwa kudhulumu mali za watu, ni laana kwa kuwapeleka watu maporini kuliwa na simba, kutafunwa na chui na kugongwa na majoka na wengine tulikuwa tunampigia makofi (kwa umasikini tulionao vichwani mwetu), ahsante babaaaa, ahsante babaaa. Sasa hii ndio malipo yake.
Hospitali mbovu, huduma za jamii mbovu, watu wanakufa hovyo kwenye mahospitali yetu na rasililimali tunazo, wenzetu mafisadi, wakijisikia uchovu kidogo tuu, wanakimbilia hospitali za Ulaya na India na South Afrika, na huku wanatangaza, "leo nyerere anakwenda wingereza kupimwa afya yake", "leo mkapa anaenda uswisi kupunguzwa mafuta mwilini", leo JK yupo marekani akipata dawa za flu", "balali baada ya kufanya balaa, yupo marekani anatibiwa".
Jamani huo wote si ufisadi? kwa nini kuanzia nyerere, mwinyi, mkapa na hawa wa sasa, wasitibiwe hapa hapa tunapo-kandamizwa sisi?
Mengi tuu, hayajaanza leo. Hayatakwisha leo.
yatatuondokea hapo tutapoikubali system, jee tunaijuwa system ni nini?