Ufisadi Bila Majibu: Rais Kikwete na Lowassa sasa jiuzuluni ndani ya siku 90 kupisha uchunguzi huru

Marais Nane sherehe ya miaka 50 katika dimbwi la kashfa za UFISADI zaidi ya 8 zilizotikisha misingi ya maendeleo katika nchi yetu ni aibu hakuna mfano wake!!
 
Kwa misingi ya hulka zetu Wa-Afrika kupenda sana anasa, ngoja uje usikie bajeti itakayokua imetumika na nchi masikini kama yetu hii kujisherehesha; ndio yale yale ya Tsvangirai kulipa mahari ya Dollar 36,000 mke wa pili.
 
KIGUGUMIZI NA UNDUMIRAKUWILI KWINGI MAGOGONI KUTUBARIKIA WATANZANIA KATIBAMPYA MURUA YA WANANCHI NDANI YA MIAKA 10 TOKA SASA

Tanzania kupata 'Katiba Mpya' mbili ndani ya kipindi cha miaka 10 toka sasa;

moja ikiletwa kwa hisani ya mtutu na kulazimishwa kinywani mwetu wananchi kuimeza tupende tusipende - lengo likiwa ni kumrithisha uongozi wa nchi mtu atakayeweza kulinda mali zilizokusanya KIFISADI na tawal zilizopita lakini baada ya ule wa Mwalimu NYERERE. Katiba hii itatumwagisha sana damu Wa-Tanzania tusiposhikamana na kuipinga kwa nguvu zote na mi-mbeleko yake.

Katiba Mpya ya pili italetwa na wananchi wenyewe tukiwa ushukani kwa kila kitu sawa na ilivyotokeapale Afrika Kusini na hapo juu Kenya. Katiba hii japo itacheleweshwa sana kupatikana lakini italeta matunda mazuri sana kote nchini na kuchangia kuharakisha shughuli za maendeleo kote Bara na Visiwani.

Hata hivyo katiba hii ni lazima iwe ni matunda ya WAPENZI WA MAADILI YA MWALIMU NYERERE, WATETEZI WA UZALENDO, HAKI NA UTU WA MTANZANIA kote nchini wakishirikiana nje ya himaya za itikadi za kisiasa.

Aminini haya nawambieni leo; upepo wa mabadiliko kamwe hautozuilika na urefu wa jengo la Magogoni.
 
HOJA YA KUDAI TANGANYIKA NDIO HIYO IMEHUISHWA NA RAIS KIKWETE PAMOJA NA PROJECT-MEMBE

Pindi tu unapoviingiza vyombo vya utawala vya Tanzania Visiwani kuja kutunga sheria za muungano na pia kuandika 'Katiba Mpya' ya ikulu bila ya kuweka wananchi wote kushika ushukani kwa vikundi vyetu vya washikadau kama inavyoainishwa kikatiba nchini.

Hakika, SIONI NAMNA YOYOTE AMBAYO ATAWEZA KUKWEPA LAWAMA ZA KUFUNGULIA 'KOPO LENYE WADUDU WA MIAKA NENDA RUDI VUNGUNI' WATU KUDAI TANGANYIKA BILA KUSIKIA CHA MTU WALA KUGEUKA NYUMA SAFARI HII.


Ushauri wa CHADEMA usipozingatiwa kwa dhati, Tanzania kama taifa tutalia sana kwa kuchagua kusamehe busara katika hili.
 
Mkitaka ajiuzuru basi wote wataisha maana hata makatibu wakuu wote alioshauliana nao kuhusu Richmond wataondoka, basi kama ni hivyo awahi sana maana Ruhanjo bado siku chache , naye tunataka hii jiuzuru imkute ili akose mafao ya kustaafu.
 
MUNGI NYAMAZA NA UACHE KULIA SANA JUU YA MCHAKATO NAJISI KWANI MUNGU BADO YUPO UPANDE WETU DHIDI YA MAFISADI NA KUTAFUTA KWAO KWA NGUVU KULINDANA

Afande Mungi acha kulia juu ya Mchakato uliotekwa na kunajisiwa kiasi kile, Mungi ukilia unaliza wengi. Cha msingi kazi iendelee tukiwa na utaifa mbeeelee kama tai mioyoni mwetu!!!

Remember, even in and amongst a hord of 'Devils' there would always exist
LESSER DEVILS (people only smeared with devilish ideal simply because of their being in company of the well established heathens) with whom we can very well work together toward a common national endeavours based on a set of known body of unquestioned principles.


The way nilivyo na negative attitude na CCM naona kila mwanaccm ni feki tu!
 
MUNGI NYAMAZA NA UACHE KULIA SANA JUU YA MCHAKATO NAJISI KWANI MUNGU BADO YUPO UPANDE WETU DHIDI YA MAFISADI NA KUTAFUTA KWAO KWA NGUVU KULINDANA

Afande Mungi acha kulia juu ya Mchakato uliotekwa na kunajisiwa kiasi kile, Mungi ukilia unaliza wengi. Cha msingi kazi iendelee tukiwa na utaifa mbeeelee kama tai mioyoni mwetu!!!

Remember, even in and amongst a hord of 'Devils' there would always exist
LESSER DEVILS (people only smeared with devilish ideal simply because of their being in company of the well established heathens) with whom we can very well work together toward a common national endeavours based on a set of known body of unquestioned principles.


The way nilivyo na negative attitude na CCM naona kila mwanaccm ni feki tu!
 
MTATIRO HAYUKO PEKE YAKE KATIKA USINGIZI HUU ULIOTUTANDA KWINGI JUU YA 'MUSWADA WA MAKINDA' KUCHUKUA MIMBA HARAMU NA SASA KUZAA 'SHERIA PROJECT-MEMBE'

Wala Katibu Mkuu Msaidizi wa CUF, Julius Mtatiri si peke yake kati ya watu ambao hadi hivi sasa wamesoma huu muswada wa Makinda, kuelewa undani wake na mapungufu hatarishi kwa usalama wetu kama taifa na hivi sasa wenyewe kwa wenyewe kuanza KUJIHOJI NAFSI ZAO juu ya kitu gani walichokipitisha Bungeni Dodoma, watu hawa ni wengi mno nchini na pengine watakapobaini ukweli wa mambo huenda wakaageuka mbogo zaidi kuliko hata sisi hivi sasa.

Si Mtatiro Juliasi tu ndiye anaayeamka na kutambua madhara yaliomo kwenye huu mchakato uliotekwa na ikulu huku wachache wakijiandaa kutuchomolea katiba yao toka mfuko wa nyuma na kuimwaga mezani mara baada ya geresha mbili tatu hivi, japo hawasemi kwa kinywa kipana hadi sasa hivi ila ukweli wa mambo ni kwamba hata baadhi ya wabunge wa CCM hivi sasa wameanza kulia na kusema walicholetewa bungeni ni tofauti kabisa na kile Kashilila lichokipeleka Magogoni.

Mara baada ya kumwagiwa hela za Jairo wao walichokifanya ni kuwasonya wabunge wa CHADEMA na kuwaita majina yote duniani bila kujua kwamba mwisho wa siku mambo ndio kama haya ya 'Muswada wa Makinda' kugeuka ghafla na kuwa sheria ya Project-Membe.
 
nyie wazee wa jf mlio nyuma ya pazia mnao waogopa hao wakubwa mbona hii post hamjaitoa, lakini ile ya 100 days mkaitoa fast? haya sasa shika kitufe muitoe faster.

moja, mbili, tatu,


bado tu,

au leo usalama wa taifa hawapo humu?

SHAME, SHAME ,SHAME,


 
CHADEMA, shitaka sasa iwe mikononi mwao wananchi kila pembe ya taifa hili huku tukiweka sawa swala la 'A LESSER DEVIL' to work with toward permanent stopping of the infamous Project-Membe endapo itagundulika kuwa utekelezaji wake ni sharti sisi wananchi kunyimwa fursa ya kujitungia katiba tukiwa usukani.
 
RAIS KIKWETE NA MJUMBE WA NEC CCM TAIFA EDWARD LOWASSA SASA NI WAKATI MWAFAKA MJIUZULU MARA MOJA KUPISHA UCHUNGUZI WA TUME HURU KUWATATISHENI MAJINA MBELE YA UMMA NA JUMUIYA YA KIMATAIFA:spy:

Kufuatia sakata la ufisadi juu ya ufisadi katika serikali hii ya awamu ya nne na viongozi kuzidi kutupiana mpira bila matokeo yoyote ya kubadilisha sura ya mambo, wananchi sasa tunasema kwa sauti kuu; Rais Kikwete na Lowassa mjiuzulu sasa hivi nyadhifa zote kupisha uchunguzi wa kujitegemea ili kutakasha majina yenu mbele ya umma.

Wananchi tunayo haki ya kuhoji vitendo vyenu, tunayo haki ya kujua kwa kina kitu gani kinaendelea ndani ya uongozi wetu kiserikali na vyama vyao vinavyowafadhilini nyinyi kushika nyadhifa hizo.

Ndio, nasema wananchi sasa tunataka majibu ya ki-uchunguzi juu ya Richmond, Dowans, Meremeta, IPTL na nyinginezo ili sote tupate kuanza upya katika ukurasa mpya kama taifa. Ndio,pale ambapo vyama vinavyowafadhilini kushika nyadhifa za umma zinaposhindwa kutolea maamuzi mambo nyeti na kero kubwa kama haya kwa taifa maana yake ni kwamba sasa maamuzi lazima yapatikane toka nje ya hicho chama fadhili.

Na hiyo ndi sababu sasa umma wa Tanzania kwa ujumla wetu tumeamua kuwaombeni kupisha uchunguzi ufanyike haraka.

Nasema hizi kelele mnazoendelea kutupigia makanisani, misikitini, na kwenye vikao vyenu vya maswahiba kuuziana chai wala hazitusaidi kupunguza ukali wa maisha ambamo vitendo vya rushwa vimetufikisha kama taifa hadi dakika hii.

Kama hamnielewi bado nasema hivi, Jogoo akijinyea mwili mzima bandani hata siku moja kamwe hapati tu kutakata eti kwa kuzidisha sana kasi ya kuwika na kuwika kila mahala akitangaza utakatifu wake huo.

Rais Kikwete, Lowassa na wengine wenye shutuma kama hizi za rushwa chonde mtusamehe na hizi siasa uchwara, Wa-Tanzania hivi sasa TUNADAI MAJIBU kwa haraka na kina zaidi. Endapo mlikua bado hamjui, uvumilivu wote sasa umeanza kutushinda na kweli Wa-Tanzania sasa tumechoka visivyo kifani na hizi 'bembeleza mwana' zenu hizi juu ya dhamira zenu kushughulikia rushwa nchini.

Ni wazi tena mkumbuke ya kwamba mambo haya yote yamekua yakiendelea huku wananchi tukiendelea kuumia zaidi na zaidi kwa gharama ya maisha inaendelea kupanda ajabu, watoto kufa bila dawa hospitalini, vijana hatuna ajira, shughuli za ukulima mashambani yamekwama na haki kutoweka ofisi za umma kutokana vitendo vya rushwa mnazoshutumiwa nazo nyinyi hapo. Kwa nini muendelee kushikilia nyadhifa za umma wakati kila kona kuna kilio??

Kwa kuwa hata na nyinyi hatupendi kamwe muonewe kutokana na vitendo vya rushwa ambavyo pengine hamkuzifanya, basi ndio maana tunawaelekezeni kwamba njia ya kistaarabu ni kujiweka kando na nyadhifa zote za umma hadi hivi sasa ili uchunguzi wa kina upite na baadaye historia ikawaamueni vizuri na kwa haki zaidi.

Ndio, kufuatia sakata la ufisadi kila kona nchini bila ya wananchi kupewa majibu ya kuridhisha juu ya kila tukio, kupuuzwa kwetu sana, watu kurushiana mipira kusikoisha juu ya hili saratani linalorudisha nyuma maendeleo, na hata vikao rasmi vya baadhi ya vyama vikongwe nchini kushindwa kutolea jibu KERO HILI KUBWA KITAIFA, wananchi sasa tunasema Rais Kikwete na Waziri Mkuu uliyejiuzulu kwa kashfa hizi hizi za rusha sasa mjiuzulu nyadhifa zote kupisha uchunguzi wa kina juu ya mambo haya yote na kuweka wazi kodi zetu zilipo.

Kwa kuhitimisha hoja yangu hii hapa, napenda kusema nafasi zote za umma watu huzishika kutokana na ridhaa na imani kubwa ambayo wananchi wanao kwa viongozi wao. Kwa kusema kweli hadi sasa wananchi hatuna imani kwenu tena mpaka siku tume huru itakapotupa sababu za kina za kutufanya kurejesha tena matumaini, heshima na imani kuendeleaa kutuongoza tena.

Hebu fanyeni hima juu ya hili kabla taifa nzima hatujalazimika kutumia silaha yetu ya mwisho ya maandamano dhidi yenu mpaka kieleweke. Penye ustaarabu wananchi hatutosita kurudisha ustaarabu hata kama shutuma dhidi yako ni nyekundu kama damu, na kinyume chake pia ni kweli tena bila ajizi.
:spy:
Nyege zinakusumbua wewe tafuta mwenza ukalalwe then utaacha kufikiri kwa kutumia makalio na kuota ndoto za alinacha na alinanuswe!!
 
Tz wapole sana. Lowasa kasema kila kitu kuwa jk ni ssehemu ya richmund. Hata akitembea bila suruali hakuna shida. Lipi baya unataka afanye ajiuzulu! Hana hata aibu kwanza huyu ni mswaili wa stand. Hana moral authotity!anacheka tuuuuuuuuuuuuuuuuuuu. Ujinga ni faida
 
MJUMBE WA JF HAPO JUU:
NAKUPONGEZA SAAANA KWA KUTOFAUTIANA NA MAWAZO YANGU NA HIVYO NDIVYO DEMOKRASIA NA UHURU WA MAONI UNAVYOTUTAKA TUENENDE HAPA JUKWAANI


Ewe mjumbe wa Jamvi la JF, hongera kwa kutoa maoni yako jukwaani na hata kuonekana kukereka kule mada ya UFISADI NA WATUHUMIWA WA UFISADI nchini kuguswa.

Jisikie huru zaidi kutokubaki na dukuduku moyoni kwani utayari wa kukutetea wewe kuyatoa maoni kama hayo ulioyatoa tayari ubaoni; usipime, nitakutetea hadi mwisho huku nikikuhimiza tu kusukutua kidogo maji mdooni ili kusiendelee kukuponyoka maneno yanayoanguka chini ya kiwango hapa JF na vile vile kuondoa staha.

Nguvu ya hoja zaidi kuliko matumizi ya hoja za nguvu mkuu maana wengine kwa upande wa hiyo ligi ya pili tulishatoka huko siku nyingi sana 'wa-ubani'. Katu nisingependa MODS wakuvute shati kwa aina ya lugha uliotumia hapo juu.

Hawa ni viongozi wetu na ni lazima tuendeleze
CHECKS AND BALANCES dhidi yao (wao wanaelewa haya yote hivyo wewe kuchagua kujinyonga mguu na kuacha shingo juu ya haya ...) wakati wote tena kwa ukali hasa ndio mambo yaweze kwenda bila wengine kujisahau na kugeuza majukumu ya umma lele mama tu! Tukutane wakati mwingine kuendeleza mjadala usiokua na hata chembe cha ulevi kichwa mkuu, au sio?
 
HATA VIJANA NAO WAKINAWA VEMA HURUSIWA KUSHIRIKI MLO MEZA KUU NA WAZEE: DR SLAA KAZI YAKO CHADEMA IMETAMBULIKA KWA VIJANA!!

"Hata kijana akinawa vizuri na vile vile kuonekana kusafisha mikono yake vema katika jamii yake inayomzunguka, kuna uwezekano mkubwa akakaribishwa meza kuu na kushiriki mlo kwa pamoja na Wazee," mwisho wa kunukuu toka kwa Profesa Chinua Achebe, (katibu chake cha 'Jamii Msambaratiko').

Vivyo hivyo, ni wazi kwamba malezi ya utaifa na ujasiri katika vijana hasa wa CHADEMA umemgusa Mhe Kasi na Viwango.

Kamanda Lema kama ulikua hujui, msimamo wako thabiti wa kutetea pasipo kurudi nyuma dhana ya heshima kwa '
UBINADAMU, HAKI NA UTU WA MTANZANIA'ni dira hiyo nzito ambayo hadi sasa inawafanya MAFISADI viti kutokukalika na amani kwao kutoweka baada ya kuuona uungwaji mkono unavyopatikana toka kwa vijana wote nchini bila kujali itikadi.

Mhe Dr Slaa, hongera sana kwa uongozi thabiti na malezi bora kwa vijana wa CHADEMA wakiwa na dira ya kueleweka na mtazamo wa kitaifa zaidi.

Ni ukweli usiopingika kwamba hadi sasa umeweza kuwapa vijana kuanzi Mhe Mbowe, Zitto Kabwe, Regia, Halima Mdee, Kiwelu, Tundu Lissu, Ben, Heche, Wenje, Mushi, John Mnyika na wengine wengi ulwe mwelekeo hdimu ya
KUZUNGUMZA NA KUISHI SIASA ZA KITAIFA ZAIDI (Vijana CHADEMA kwao chauvinist politics hupewa kisogo) kuliko zile siasa za vitongojini na zile za 'Maslahi ya Chama Chetu'.

Hakika mtu akitazama saaaana atagundua kwamba mafunzo ya uongozi imara toka kwa Dr Slaa kwa Ma-Kada wa CHADEMA huenda ikawa kwao wao umewaambia kwamba siri ya mafanikio kisiasa kwa kipindi kirefu zaidi ni kuendeleza SIASA ZA KUTETEA TU MASLAHI YA UMMA.

Mh Samweli Sitta ameyasema hayo wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa la Mt.

Teresia jimbo kuu katoliki Arusha. Amesema kuwa Mh Nyalandu na Mh Lema ni vijana ambao taifa linawahitaji na wao kama wazee wameshaanza kuwaridhisha uongozi wakiwa na matumaini makubwa kuwa watatufikisha kwenye nchi ambayo baba wa taifa alitamani tufike!

Nawasilisha
 
CCM: Hoja ya uvuaji gamba haina mbadala wake wala njia ya mkato; ni ama mnakubali kutangazia umma kwamba UFISADI ni sehemu rasmi ya sera za chama hiki au kuchagua kujitenga kabisa na janga hili la taifa na wananchi nasi kuweza kujiridhisha kwamba kweli CCM na ufisadi sasa ni mbali mbali na wala si dam dam.
 
JF itajitenga vipi na harufu za kuwakingia kifua baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi nchini hadi hivi sasa?
 
Watu hata tukiamka na kuanza kulewea undani wa jambo nyeti kama hii ya SHERIA YA PROJECT-MEMBE KUWA RAIS, kwa makubaliano ya kingizwa kinguvu 'MAHAKAMA YA KADHI' ambayo ki-uhakika ndio mpango mzima ulivyo kwa Rais Kikwete kujihodhisha madaraka yasio yake kikatiba kutunga Katiba Mpya, yote bado tu ni kule kule kuamka bado!!

Na mjadala uendelee na mambo yakae sawa kabla hakujachelewa sana juu ya hiki kilichokua 'Muswada wa Makinda' na sasa 'Sheria ya Project-Kamiliusi-Membe' huku akiwa na kibandiko na rosari mikononi zote kwa wakati mmoja ilmradi tu mwisho wa safari kuje kuhalalishe mchakato mzima wa ufikaji huko penye malengo yenyewe binafsi hayo.

Tafakarini sana jjuu ya hili na jambo la ajabu lililozazimu hata serikali ya CCM kudiriki kuwahonga wabunge wetu 'Nyongeza ya Posho' ilmradi tu Rais Kikwete apewe KISHERIA (Bungeni) Madaraka yasio yake ki-Katiba (na kuwekewa kinga ya KUTOKUHOJIWA na mtu na au taasisi yoyote) ilmradi tu Project-Membe (Rosari-Kibandiko mchanganyiko) na Mahakama ya Kadhi kwa pamoja inapita bila kupingwa - kuwa sehemu ya Katiba ya nchi na Kamilius kuwa mlinzi wake!!!!!!!!!!!


***************************************

SOURCE: TANZANIA DAIMA
DATE: DECEMBER 08, 2011 (Today)
PAGE: FRONT PAGE
SUBHEADINGS: Wahofia kuvunjika amani, Washangazwa na Uamuzi wa Bunge, Wasema Nyerere amesahaulika

***************************************

Kanisa Katoliki nchini (TEC) limeshtushwa na hatua ya Rais Jakaya Kikwete kusaini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011, harakharaka kwa kuwa kunaweza kuipeleka nchi pabaya.

Akizungumza jijini juzi na TANZANIA DAIMA muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa kitabu cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kilichoandikwa na John Kasembo, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Askofu Mkuuu Jude Thadaeus Ruwa'Ichi alisema Watanzania wengi walitaka muswada huo usisaniwe, na kwamba mkuu huyo wa nchi alipaswa kusikiliza mawazo ya wananchi wake, na si kuwahi kusaini na kuwa sheria, Rais huyo wa TEC alisema kitendo cha Serikali kukusanya maoni mikoa ya Dodoma, Dar-Es-Salaam na Zanzibar peke yake, haitoshi kujenga hoja ya kusaini ama kupitisha muswada huo wa Katiba.

Askofu Ruwa'Ichi alisema suala la kuundwa kwa Katiba mpya si hiari ya Rais wala kikundi na tabaka Fulani bali ni la watanzania wote.

Rais huyo wa TEC ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza alisema hatua ya kulipeleka suala la Katiba mbindembinde linaweza kuipeleka nchi kubaya na Kanisa Katoliki halitaki Watanzania wafike huko.

Alisema walitegemea Kikwete angethamini na kujali maoni ya wadau wengine, lakini katika namna ya ajabu hakuonekana kujali chochote. Ruwa'Ichi ambaye alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika uzinduzi wa kitabu hicho, alieleza kushangazwa na kitendo cha Bunge kupitisha harakaharaka muswada huo.

"Hivi Bunge linashughulika na maslahi ya nani? Wabunge wamepewa dhamana na wananchi, hivyo ni lazima wawasikilize wanachotaka, halafu ndicho wakifanyie kazi, na si kuonekana kama ushabiki fulani", alisema Askofu Mkuu Ruwa'Ichi.

Alipoulizwa kuhusu suala la udini linaloonekana kutumiwa na baadhi ya wanasiasa nchini, Askofu Ruwa'Ichi alikiri kuwapo kwa jinamizi hilo, na kusema ajenda ya udini kwa sasa imekuwa kama kichaka cha watu Fulani kuficha maovu yao.

Alionya kwamba iwapo serikali itaruhusu mijadala ya dini kutawala nchini, basi taifa lipo hatarinikupoteza ustawi wake, na akataka watu wasitumie mgongo wa dini kuficha madhambi yao.

Katika hatua nyingine, TEC imesema mambo yote mema yaliyotendwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere yametupiliwa mbali, na sasa kila mtu anatenda lolote linaloonekana kuwa na manufaa kwake.
 
MHE LOWASSA NI KWELI GAMBA LA CCM NI KAMA LILE LA KITUNGUU HIVYO MPANGO MZIMA HAPA UWE NI KUNG'AO KABISA 'MAGAMBA YOTE NA MIZIZI YAKE' ILI JAMII TUWE TUMETENDA HAKI KWA WOTE

Kweli swala zima la Gamba la UFISADI huko CCM haina tofauti na Kitunguu na MAGAMBA yake yalioumana tangu nje ha mle kati kati kabisa ambapo wengi wengi wangetarajia kusiwepo na biashara yoyote ya aina hiyo hata kidogo.

Na ni kwa sababu hii ndio maana narudia hapa kwamba Umma wa Tanzania kwa hasira kali juu ya ufisadi na hivi sasa utekwaji wa madaraka yetu kujitungia Katiba Tuitakayo, tunakusudia kufyeka idadi kubwa ya wabunge wa CCM tangu sasa hadi huko 2015 toka kwenye 250 hadi viti 78 tu!!!!!!!!!!!

Na hilo liko njiani, shauri yao wale wanaoamini tu mambo kwa kuona kwa macho bila kujichukulia tahadhari mapema!!!!!!!!

kumbu mhe lowasa alisema mengi nec na kufananisha dhana ya ccm kujivua gamba na kitunguu eti kila hatua ina gamba ukiamua kuvua patabaki patupu kadhalika ccm wakiamua kuvuana gamba habaki mtu
 
CHADEMA ' HOMA KALI KWA MAFISADI NDANI YA CCM' NA MIPANGO YAO MIZIMA YA KUTAKA KUJIHODHISHA MADARAKA ISIO YAO KULINDA 'MASLAHI YA VIKUNDI' BADALA YA MASLAHI YA UMMA

CHADEMA moto mkubwa wa mabadiliko ya kweli usambae kote nchini; kijiji hadi kijiji, kichwa hadi kichwa mpaka somo zima litakapoeleweka.

Ndio, nasema kwamba nalo somo la aina ya BIASHARA iliofanyika siku za hivi karibuni kati ya Bunge kupitisha Muswada Haramu kwa manufaa ya wachache kule Ikulu Magogoni kwa maelewano ya wabunge wa CCM na CUF waliopitisha hiyo sheria haramu kurudishiwa asante kwa Rais Kikwete kuwapandishia posho zaidi ya mara 3 kwa kutimiza wajibu wao tu kukaa bungeni.

Maslahi ya Umma mbeeeele kama tai katika mafunzo haya kote nchini!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom