Ufisadi bado watutafuna | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi bado watutafuna

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaka, Mar 6, 2008.

 1. Kaka

  Kaka JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2008
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 705
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 80
  SERIKALI BADO NI LOWASSA ROSTAM NA KIKWETE

  Fukuto lafukuta, moshi wafoka, mapovu yanamwagika, CCM imefika njia panda! Ama isuke au inyoe!

  Hili vurugu la Richmond , likizingirwa na BOT EPA, BOT CIS, BOT Minara, Rada, Kiwira, Buzwagi na moto kutoka Upinzani, unafanya mambo kadhaa tujiandee kutokea.

  1. Wabunge ambao si mtandao, wenye uchungu wa kweli wa CCM, kuendelea kusulubisha viongozi wao na Serikali
  yao iwe wazi. Hawa wabunge, mwokozi wao na nguzo yao ni Wastaafu Malecela, Kawawa, Mwinyi, Salim na Msuya. Huku wako hawa walioshupalia RDC;-Mwakyembe, Kilango-Malecela, Seleli, Kimaro, n.k.

  2. Team Mkapa; huku ni wale wajanja wa Che-Nkapa ambao bado wanatibu majeruhi ya mchakato wa kugombea Urais 2005 na kunyang'anywa tonge la Hatamu za Chama. Hapa kuna Mang'ula, Ngwilizi, Kigoda, Kinana, Warioba na Ruhinda. Katika kundi hili, pia wapo wale waliotajirika na mradi wa Ujasirimali Ikulu; Yona, Mramba, Mgonja, Mkono n.k.

  3. Mtandao; Kundi hili lina majeruhi wengi kutokana na kuvunjwa kwa baraza la mwazirina mwegemeo wa kashfa za ufisadi kuwa kwenye shingo zao. Kundi hili, limegawanyika katika sura mbili;

  1. Team Kikwete ambayo wamebakia Makamba, Chiligati, Membe, Migiro, Karume
  2. Team Rostwassa(Rostam/Lowassa); Karamagi, Msabaha, Nchimbi, Apson, Meghji, Kamala, Masha Diallo, Chenge,

  4. Wasiofungamana lakini wana nguvu na ni tishio; Pinda, Mwandosya, Sumaye, Balali, Salmin, Magufuli, Msekwa na Sitta.

  Serikali mpya na baraza lake la mawaziri bado ni ya Kikwete Lowasa na Rostam.

  Masha-Mambo ya ndani , bila Lowasa Bw. Mdogo Masha asingekuwa hapo alipo, ni lowasa aliyemshika mkono na kumwingiza kwenye siasa, kwani yeye Masha na Business partner wake Magai walikuwa private lawyers wa mamvi, na hata Magai aliwahi kupatiwa ujumbe wa bodi ndani ya city water wakati huo Lowasa ni waziri wa maji. Je unategemea Masha atasahau alikotoka kama JK asivyomtupa Hussein Mwinyi???? Hao polisi, Manumba na Magereza vyote viko chini ya Masha. Sasa je, nani atamkoma Nyani giradi????


  Ngeleja-Nishati na Madini- Huyu alikuwa mwanasheria mkuu wa Vodacom Tanzania LTD ambako Rostam na lowasa wana hisa japo mamvi ni silent share holder. Ni Rostam aliyemshika mkono Ngeleja akagombee Sengerema na kumpatia fungu la kutosha ashinde. Na ndio maana ameachwa madini ili aendelee kulinda
  migodi ya Rostam. Hivyo tusitarajie mabadiliko makubwa.


  Mkullo-fedha - Huyu akiwa mkurugenzi wa NPF sasa NSSF alichota mapesa kibao kumuunga mkono JK mwaka 1995, hivyo ni senior mwanamtandao. Na ndio maana Mkapa alipoingia madarakani akamtema NSSF.

  Chenge- Miundombinu, JK hana namna, hampendi Chenge lakini anakuwa forced na Lowasa na Rostam. Mikataba yote kuanzia IPTL n.k imesainiwa wakati wa Chenge na yeye anaelewa nani ni nani katika hayo makampuni yanayozidi kuutafuna utajri wa taifa hili na kutuacha watanzania tukilalia chips kavu. Eti JK atamtosa Chenge! THUBUTU! Atasema kila kitu ! Na ndio maana wakamuwahi Salome mbatia wakamuua ili asiendelee kutoa
  siri kwa wapinzani kuhusiana na pesa za BOT, kwani yeye ndo alikuwa Mweka hazina mkuu wa chama wakati wa uchaguzi


  Kutokanana kuwepo makundi haya makubwa na utata unaotambaa angani hasa baada ya Lowassa kuangushwa na minong'ono kuwa naye Lowassa ana ushahidi wa kujikosha, linalobakia kwetu watazamaji ni kupima upepo na kuomba dua wapigane na wagawanyike ili tujue nani ni kwa manufaa ya Taifa na nani ni mnyonyaji.

  Je ni kweli? LAKINI LISEMWALO LIPO

  CCM si salama, na hata kama wakitoka nje ya ukumbi wakiwa wamekumbatiana, tusiwaamini.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  very true
   
Loading...