UFISADI: Another 105 billions stolen

Mr. Clean

Senior Member
Aug 7, 2006
194
44
Maskini, Tz yetu (si yao)!

Pamoja na kuyasikia hayo ya TICTS 'Tiscan' huko bandarini kama yalivyoelezwa na kamati ya bunge miundombinu pia kwenye gazeti la Thisday, KUNA NYINGINE NILIKUTANA NAYO MAJUZI HUKO MKOANI LINDI.

Kampuni ya kuwait ya KAFARI inayojenga barabara huko Lindi, ilisaini mkataba na Serikali wa 51bilions, lakini hadi sasa kumalizika kwa kazi imelamba mshiko wa 105bilions!
YAANI hizo 54bilions za ziada yasemekana zilitumika kukampeni SISIEMU.

Lakusikitisha sasa kampuni ikajenga barabara kwa tope lililokataliwa na wataalamu wa barabara. Na SISIEMU wakasema DOLE TUPU! ajabu nikaambiwa ati itadumu kwa miaka 20!

Zaidi majuzi serikali hiyohiyo ya CCM akatengua mkataba wa kujenga barabara eneo la daraja la mkapa kwa kuwa KARAFI haikuwa kwenye nafasi ya kushinda tenda, na sasa wametangaza tena ili mazingira mazuri yatengenezwe kuipatia tena kampuni hiyo tenda kusuport hela ya kampeni 2010, MPOOOOOOOOOOO! Wadanganyika? JE tutafika?
 
Hizi tenda kumbe ni tenda za kutumaliza sisi wenyewe. Sidhani kama kuna rais msafi kwa Tanzania hii, maana kama wanaanza kuandaa mazingira "mazuri" ya mwaka 2010 basi tumekwisha
 
Mr Clean, info nzuri... Lakini kabla hatujaweza kuichambua mada hii naomba utusaidie kutuambia ni barabara gani hiyo unayoiongelea? Sababu hapo jamaa wanaweza wakawa na vielelezo kisha tukaonekana kwamba hatuna facts. Uzuri ukituambia ni barabara gani tutatafuta technical info na kutoa wazi hiyo "so called variation/cost overruns" ni ya kweli au girini tuu!! Pia hawa Kharafi kwa wale tulio katika construction industry tunwajua sana kwa mambo yao ya "kupiga mabao" lakini kwa hili hatuwezi kuwahukumu mpaka tujue kulikoni!!

Sisemi kwamba nakataa kwamba kuna mkono wa mtu kwenye hilo swala lakini siwezi kukubali sababu sina vielelezo.

Hili la pili la abortion ya hiyo tender at last minute naomba uangalie hii "thread" kwani tulishalijaribu kuliweka hapa ili tuambiwe ukweli lakini naona mambo yakawa patupu…… soma

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8699

Ukweli ni kwamba lazima wote tujue kwamba katika miradi yenye pesa nyingi na migumu kuona mazingaombwe ni ya barabara... Nakumbuka kuna wakati ilifanyika Technical Auditing ya Road Funds ambapo nasikia (through the bomba) ni matumbo matupu yalionekana kule ndani (TANROADS, TAMISEMI, RFB, MOW)...... lakini bahati mbaya report wengi tuliisikia tu na sikusikia tena kama hii ilifanyika tena (iklikuwa mwanzoni mwa 2000s)....

Bottom line is ngoja tumalize kwenye BoT, TICTS, CIS tukimaliza huko then tutarudi kwenye hizi barabara zetu kuanzia quality, tender process, financial aspects kisha tuwasulubu wale waliokula mapesa yetu!!!
 
Nasikia kichefuchefu, Nahisi kizunguzungu!! Ndiyo maana waliwatoa maCEO wageni (Yule mzungu na then Mghana) ili waweke mswhili mwenzao then wale vizuri!!!!
 
Morani75,
Nashukuru kwa maelezo yako. Hapa ni baadhi ya data nilizopata:-
= Karafi company inajenga barabara toka Lindi kuelekea Dar, mingoyo hadi Daraja mbenkuru.
= Barabara imeanza kujengwa toka 2003, imemelizika 2008, lakini mkataba ulikuwa imalizike 2005
= Kuna kipindi Lowasa alikwenda huko akiwa na Mramba (by then waziri miundimbinu) mramba akalia kwa Lowasa kuwa mkandarasi ni mjeuri anataka kujenga barabara ya lami kwa kutumia udongo usiofaa! Hatahivyo baadaye ndo umetumika!
= Kama mtakumbuka ajali ya Msanii wa mashairi wabunge letu Mdhihiri wa mdhihiri(kwani tuna washairi watatu hadisasa bungeni 1Lowasa,2Mdhihiri,3Khatibu Seif) ilitokea baada ya mpanda baiskeli kukataa kupita kwenye tope kwani barabara ni nyembamba kwenye lami, ndo aakapita lane ya gari akakoswakoswa na mdhihiri(ingawa nimesoma thread hapa kuwa alifumaniwa......)
 
Jamani,hivi kuna maisha bora kweli nchi hii? Every where ni rushwa rushwa,ufisadi, ufisadi.Tutafika wapi? Mliona data za kutosha zileteni hapa tupate pa kusemea. Miye nimepita barabara hiyo mara nyingi tu,ni kweli ni nyembamba sana,hasa kutoka Lindi kwenda mtwara. Kwa viwango siwezi kusema sana kwani miye sina taaluma hiyo lakini kama barabara inajengwa na baada ya miaka miwili inaanza kutoboka,kuna uwalakini. Nakubaliana na wewe mazingira ya rushwa yalikuwepo,inakuaje mkandarasi anakuwa na nguvu kuliko waziri aliyempa kazi? hapo kuna "GODFATHER". Tuanaomba data zaidi
 
Hii inafanana na ile iliyonikuta kule Holili mwaka 2005 wakati natoka kagari kangu kule .Nilipofika walisema gari lako yatakiwa 2.5m lakini kwa kuwa CCM wana uchaguzi kuna waraka wa kila mmoja kuchangia CCM ishinde .So unatakiwa kuzama kwa 2m more na jumla iwe ni 4.5 utoe gari . Nilipata kichaa na gari liko huko hadi sasa ninatafuta hatua za kisheria nazunushwa tu kisa nilijifanya mjuaji sikutaja kuichangia CCM ishinde . Mramba huyo alikuwa waziri wa fedha .
 
Morani75,
Nashukuru kwa maelezo yako. Hapa ni baadhi ya data nilizopata:-
= Karafi company inajenga barabara toka Lindi kuelekea Dar, mingoyo hadi Daraja mbenkuru.
= Barabara imeanza kujengwa toka 2003, imemelizika 2008, lakini mkataba ulikuwa imalizike 2005
= Kuna kipindi Lowasa alikwenda huko akiwa na Mramba (by then waziri miundimbinu) mramba akalia kwa Lowasa kuwa mkandarasi ni mjeuri anataka kujenga barabara ya lami kwa kutumia udongo usiofaa! Hatahivyo baadaye ndo umetumika!
= Kama mtakumbuka ajali ya Msanii wa mashairi wabunge letu Mdhihiri wa mdhihiri(kwani tuna washairi watatu hadisasa bungeni 1Lowasa,2Mdhihiri,3Khatibu Seif) ilitokea baada ya mpanda baiskeli kukataa kupita kwenye tope kwani barabara ni nyembamba kwenye lami, ndo aakapita lane ya gari akakoswakoswa na mdhihiri(ingawa nimesoma thread hapa kuwa alifumaniwa......)

Hii habari ina mapungufu mengi sana.

Si kweli Kharafi& Sons inajenga barabara kutoka Lindi kuja Dar, usahihi ni wanajenga kipande cha kutoka Mbwemkulu (Lindi) mpaka mnazi mmoja ( Lindi ) kipande hiki kina efu wa kilometa 95 wameshamaliza kazi kwa asilimia 95 ( washaweka lami kote wanamalizia alama za barabarani tu.

Kipande cha Kibiti - Dar cha kilometa 105 kazi wamepewa kampuni nyingine ( jina silikumbuki ) kazi imekamilika kwa asilimia 100

Si kweli Kharafi wameweka lami ya matope (sijawahi kuona lami ya matope maishani mwangu) Usahihi ni kuwa Kharafi ulipofika wakati wa kuweka lami injinia mshauri ( kutoka wizarani ) alikwenda kuangalia aina ya mawe watakayotumia na akayapasisha , Kharafi wakaanza kazi ya kuvunja mlima ili wavune mawe baada ya kazi kukamilika wizara ikasema mawe yale hayajafikia kiwango na wakataka Kharafi watumie mawe kutoka Lugoba (Pwani) ndipo mgogoro ukaanza hapo kwani Kharafi wakataka walipwe gharama za mawe waliyo yatayarisha kwanza vilevile kutoa mawe kutoka Lugoba Gharama zitaongezeka na serikali wakatakiwa kufidia kwani ni uzembe wao.

Kipande cha barabara kutoka daraja la Mkapa mpaka Kilwa Somanga mkandarasi bado hajateuliwa.
 
Sasa Masatu mbona unatuletea habari nusunusu, Sasa kama humkubuki Kandarasi maana yake ni humjui Kandarasi, hapo information zako zinakuwa zina "hang", mimi nilidhani uta counter argue kwa fact zilizo clear, kumbe na wewe unatuachia mashaka tele.
 
Gamba la Nyoka ninaposema kampuni siikumbuki nina maana jina limenitoka kidogo, lakini for sure si Kharafi na kwa taarifa yako hao jamaa walipewa kazi hiyo Kibiti - Dar toka miaka ya 1990's na wamemaliza kazi juzi juzi na I understand walikuwa na matatizo ya malipo na serikali.
 
Heshima mbele.....

1. Naomba nianze kwa kuzungumzia lile swala la Kharafi. Niliweza uliza uliza kule mahala nikambiwa kwamba pale lilikuwa ni kosa la Client (Serikali) kwani mhandisi mkazi (resident engieer) wa serikali alipitisha kutumika kwa jiwe lile. Lakini kwa bahati mbaya ni kwamba jiwe lilikuwa ni hard-limestone ambalo sio gumu na lilipopimwa baada ya kazi kuanza likaonekana halikidhi viwango. Sasa hapa kuna matatu, la kwanza ni kwamba Mhandisi Mkazi hakuwa na ujuzi wa kutosha na uelewa wa contract issues kwani alipoidhinisha na kazi ikaanza then alikuwa ameshamkubalia kandarasi so any changes will result in variation.
La pili ni kwamba, hi ni moja ya zile project wanasema kiingereza wanaziita "Design build"!! Tricky projects especially in our Tz scenario. Pale wale waliotayarisha bidding documents hawakuelezea mambo mengi yakiwemo ugumu wa upatikanaji wa mawe ya ujenzi. Sasa inaonekana (sikuweza kupata bid documents) kwamba waheshimiwa waliweka option mbili tu, moja ya kutumia jiwe la sehemu wanaita Kiwawa (guess am right here) na pili ni sehemu wanaita Mingoyo. Sasa hizi sehemu zote mbili kwa haraka ni kwamba sources ni limestone and zimeanza kuwa exhausted.
La tatu ni kwamba yule Mhandisi inasemekana alipewa kitu kidogo kudhania kwamba njia/barabara itajengwa na hakuna kitakacho onekana na watu watalala mbele, wapambe wakawa wengi then ukweli ukaonekana.
Sasa ukweli ulipoonekana, serikali ikaamuru kwamba litumike jiwe la Lugoba, "Wrong move"... Why, haulage ya hili jiwe (say Dar Mbwemkulu 300km, Dar Lugoba 150km) zaidi ya kilomita 450 ina maanisha ni gharaa tosha manake lori linaweza kufanya sana sana roundtrip in 2 days.... Hapo hebu angalia bei ya mafuta, purchase at sourse, tear and wear ya gari, ubovu wa barabara to site - bila kusahau chakula cha trafiki njiani tunaangalia gharama za kusadikika.

Bottom line hapo sisi kama Serikali tilijipiga bao la kisigino wenyewe. Swali ni kutokujua technical issues au ni kitu kidogo, siwezi kuwa na uhakika!!!

2. la pili ni lile la barabara nzima ya Dar-Kibiti-Lindi (maybe mpaka Masasi). Well kule bwana wacha mchezo linaitwa kapu la walaji. Kuna barabara zilikuwa zikijengwa/zilijengwa na MECCO, kuna za IDA Funding (am not sure but it was some donor body) ambazo hazikuwahi kukamilika na kwenye vitabu vya Ujenzi (nasikia) zimeonyeshwa kwamba zimekamlikaga zamani. So huko bwana ninachosema sio kitu cha kupita na kuangalia bali we need to get into those books and budgets and compare them to actual sitaution on the ground. Ukiambiwa kwamba materials (culverts, equipments, mabati etc) kwa kutosha kujenga njia nzima ya Kibiti-Lindi vilinunuliwa miaka ya 1980 lakini vyote vimekuwa vandalised by locals, wakubwa na Ujenzi wenyewe. Pita Nangulukuru kwenye kambi ya Ujenzi, nyumba za wenyeji Kilwa Masoko na maneneo ya karibu utakuta vile vifaa na materials mengine yametumika kwenye kujenga nyumba za watu (bati, culverts etc)... Pamoja na wizi/ufujaji wa materialz hizo kuna materials nyingi zimebaki lakini cha kushangaza ni kwamba tender zote zilizotangazwa zina vipengele vya "Suply and Install" culverts ambazo mbona tunazo zinaozeana pale Nagulukuru??

3. La mwisho ninalotaka kusema ni planning na kuna mbali.... Ukiangalia kuna report nimeiona pale Kilwa (nasikia Ujenzi wanayo) inayoonyesha study done by some company (sponsored by JICA nasikia) inayotoa ushauri wa namna ya kujenga barabara ya Kibiti-Lindi ikishauri among other things, re-alignment ya hii barabara kuipeleka more to the west sababu ya hali ya udongo. Ripoti hii sijaisoma yote lakini a reliable source confirmed kwamna ukweli katika lile kutokana na kuendelea kubomoka na kupata poor performance ya vipnde vya njia hii ambavyo vinajengwa/vimekamilika kutokana na what they called "poor soil condition due to proximity to the ocean and infuence of Rufiji and Kilwa delta"....... Siwezi kusema kuna uhakika 100% lakini I personally trust my source.

Ushauri wangu kwa Serikali katika haya:
i. Kuwaongezea vipaji wahandisi wanaopewa ajira serikalini haswa pale ambapo kuna decision making ambazo zinainfluence greatly kwenye quality, cost and performance of projects.... Lazima watu hawa wawe Accountable, Responsible and Credible!!!

ii. Serikali ni bora ianze kutumia pesa kufanya surveys za kutafuta construction materials along various routes to avoid "depletion ya Lugoba/Msata quary" na pia kupunguza haul distance za materials especially the case of Kharafi to move granite rock from Lugoba to Mbwemkulu - crazy!! Kwa harakaharaka niliongea na vijana wetu pale Somanga-Matandu project (waTZ wnafanya na wakle waChina) wakasema kuna jiwe wamesikia lipo some 100km from Njia nne (Kilwa Kipatimu) na wamesema linajulikana na Serikali lakini Mchina aligoma kulitumia mwanzoni sababu ni gumu sana?!&^%%$&** - Do the math!! hili jiwe likiwa usable si tutaweza punguza gharama by 100% considering variation ya Kharafi kwa kutumia jiwe from Lugoba!!! Bottom line serikali itumie pesa kwa kufanya hili - MUHIMU SANA

iii. Serikali itabidi itumie external party kufanya what we call "Technical Audit" za miradi inayoendelea na ile iliyokamilika kuhakiki kwamba pesa zilizotolewa na kupewa wakandarasi na wahandisi binafsi zimetumika ipasavyo na tumepata value for money and sio picha ya barabara

iv. ERB ifanye spot checks kwenye qualification za wahandisi/makandarasi katika miradi yote mikubwa kuona kama ni kweli wanajua wafanyacho au ni "VIHIYO".... inawezekana wakuu wa hizo kampuni ni regsitered and qualified lakini bahati mbaya ni kwamba site nyingi ni porini na hawa wakuu wanatumia muda mwingi kuwa mjini na kwenye starehe kuwaachia "VIHIYO" kuendesha miradi.... Pharmacy Board imepitisha kuwa kila phamacy lazima iwe na qualified and registered pharmacist lakini ERB naona bado ni "Mali Kauli mpaka sasa" tembea uone!!!

v. Kuna kipengele cha "Liquidated Damages" ambacho sidhani kama hapa nyumbani tunakitumia sana.... Hiki kina tu cost dearly sababu hawa wakubwa wanajenga barabara at their own leisure Sam Nujoma, Somanga-Matandu, Kharafi project, Singida-Manyoni and the list go on and on and on...... Hizi ni pesa tunapoteza we can recover project costs using liquidated damages pia ni udumazaji wa uchumi pale miradi inapo roll-over for more than twice the contract period......

Nadhani kwa leo hii inatosha ngoja nifanye kazi za wakubwa hapa nisije kosa mkate wa watoto (na wajukuu) ha ha haaaaaa
 
And on top of the above, Serikali pia inabidi ianze kuangalia kwa kupitia elimu ya juu swala la kuhamasisha vijana wa Vyuo va Elimu ya juu (UDSM, DIT, na vingine vyooote) kufanya project zao katika matumizi ya materials mbadala manake tuendapo huko bei ya mafuta, kuisha kwa machimbo kama Lugoba na mengineyo yatatupeleka kushindwa kujenga barabara.... Wenzetu wa nje wameanza na vitu kama "Recycling of Asphalt layers - both in foaming and recycled chipping", matumizi ya by-product ya steel industries, rice husks etc..... Uhamasishaji pia utaongezewa nguvu pale ambapo badala ya kutoa zawadi kwa mwenye GPA kubwa pekee, pia mwenye innovative research akipewa vipesa vya motisha na uhakika wa further studies na kajikazi si mchezo hawa vijana wetu wataacha ule mchezo wa ku "cut and paste" from previous research/projects..... Wale waliopita Mlimani miaka ile wanakumbuka ilikuwa ni manual mwanangu hata mtandao haukuwepo wa kufanya "Google" na kudaka project from Timbuktu kama ilivyo sasa.....

Mungu ibariki Tanzania na Watu Wake..........
 
Morani,

Shukran kwa ufafanuzi wako, maana kama inavyosomeka mtoa hoja kipindisha mambo mengi ili kupotosha.
 
Gamba la Nyoka ninaposema kampuni siikumbuki nina maana jina limenitoka kidogo, lakini for sure si Kharafi na kwa taarifa yako hao jamaa walipewa kazi hiyo Kibiti - Dar toka miaka ya 1990's na wamemaliza kazi juzi juzi na I understand walikuwa na matatizo ya malipo na serikali.

Masatu unasema hukumbuki jian la mkandarasi; sio kwamba hukumbuki ila hakukua na mkandarasi.

Barabara ya Dar - Kibiti imejengwa bila kutumia mkandarasi wa moja kwa moja, ulitumika mtindo wa 'force account', yaani serikali ilinunua vifaa vyake, mitambo yake (lakini haitoshelezi), ikatumia wafanyakazi wake na kufanya ile kazi moja kwa moja.

Katika utaratibu huu serikali inatumia hela zake yenyewe; lakini pia hutangaza na kutoa zabuni kwa wakandarasi wa kuiuzia materials za ujenzi kama lami, mafuta, oil n.k. Nadhani hata baadhi ya mitambo wanakodi kutoka makampuni binafsi.

Wakati wa kuanza mradi serikali iliajiri kampuni moja iitwayo JBG Gauff kwa ajili ya ushauri wa utawala wa mradi wenyewe. Ila kwa sasa hii kampuni haipo tena kwenye mradi huu.

Barabara hii imemalizika kwa kiasi kikubwa, nadhani sasa watakua wanafanya surfacing maeneo ya Kibiti mjini. Kikubwa ninachokiona kinapungua kwenye barabari hii ni alama za barabarani (Road sign & Road markings)
 
Haya ndo maisha bora kwa kila mtanzania... kwi kwi kwi mnataka watu wapate maisha bora wapi?!?
 
Morani75,
Here is my big '5' 2u, u must be an experienced and competent materials engineer based on how u manage 2clarify this thread! Sihaba twapanda sote lile basi letu la kijani "akida" tukienda kula chamaki nchanga!

Masatu,
Shukrani pia, ila sijatoa mada kiupotofu, bali nilisema hapo awali, nilipata taarifa nilipokuwa huko.

Well n' good. maelezo yako Morani75 ni tosha kabisa kutoa mwanga wa ukungu uliokuwepo hata kwangu.

= umesema yasemekana mhandisi mkazi alichukua rushwa toka kwa MAkarafi - kama ndivyo huo si ndio ufisadi mwingine pia? lakini hadi zifike billioni 54?

= na kama ulivyosema barabara ilijengwa kwa jiwe lililokataliwa na wataalamu - hapo si ndio kusema barabara hiyo ya MAkarafi imejengwa kwa tope?

Yaonesha hapa UFISADI ulichukua nafasi yake, kwani kama aliweza kwenda PM kukagua kazi, then Waziri amlalamikie barabara mbovu mkandarasi amekaidi agizo letu, LAKINI PM kauchuna tuu kwakuwa anajua siri ya ubovu huo, sikwamba sisiemu kamakawa walishachukua chao mapema?
 
Thanks Morani kwa maelezo ya kitaalam kabisa,kuna Engineer mmoja mtanzania yuko states sasa alikuwa akinipa story jinsi miradi ya barabara inavyoendeshwa na watu incompetent na kutia hasara taifa mpaka jamaa alikuwa anataka kulia....so painfull ukiwa unaelewa haya mambo huku ukiona jinsi hawa wenzetu wanavyochezea pesa za walalahoi,nasikia CASPIAN ni kampuni ya Rostam Aziz ambayo imepewa tenda nyingi sana huku hawajui wafanye nini..kazi ipo!
 
Koba, hao CASPIAN ndio tunawangojea sasa.... hivi sasa mambo ni TIK TIK TIK.......

Since tayari tumeshamaliza na wale wa Richmond.... Kikubwa hapa sisi tunataka kujua miradi yote ya barabara imeingiwaje, costing, tendering, quality of work, na kikubwa zaidi - "did we get value for money??"

Zipo nyingie tu ambazo kwa kweli ukizipitia utaona madudu meeengi sana......
 
Pia tutakapoangali CASPIAN tusisahau kuwa kuna kampuni nyingine inaitwa Jilanjo yenye uhusiano wa moja kwa moja na CASPIAN. Nimetafuta habari zake sijazipata ila kidogo huko Alibaba: http://www.alibaba.com/company/10618481.html

Wahanusika pia na miradi ya malaria na wanashirikiana kwa karibu na kampuni ya marekani ya Norvatis. Isije ikawa hata hii misaada ya malaria tunapewa na makampuni haya ya kigeni inazungushwa kwa wajanja na mwisho pesa inarudi kwao.
 
Back
Top Bottom