Ufinyu wa Mambo

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,554
1,382
(Angalia picha iliyoambatanishwa. Imetoka kwenye ippmedia.com, ikiambatana na habari kwamba Polisi wamekamata mashua (dhows) 8 zenye magogo mabayo yalikuwa yanapelekwa kusikojulikana)

It is pleasing to see that the Marine Police have finally found something they could outrun! You could probably stand on the shore, with gun at the ready, and order eight dilapidated dhows to sail back!

The picture tells quite a story. I see more rubbish than logs in there! Is the officer counting the number of logs or what? There are hardly thirty! I suspect that we are simply looking at a case of some villagers trying to transport a couple of logs to build huts with. Why should the impounding of that make headline news? Doesn't the Guardian have real crime to report?

5582d1250226381-a-ferrymagogo.jpg
 
Attachments

  • FerryMagogo.jpg
    FerryMagogo.jpg
    20.8 KB · Views: 155
Last edited:
Mwl umesahau ule usemi kuwa ukikamata vya ukweli nchi itatikisika.....na usalama wa nchi utakuwa at jeopardy
 
Naona hawa jamaa wakiwa hawawezi kinachotakiwa kufanyika, hutengeneza visa vya Mzee jongo na kuwarubuni wananchi kwamba wanafanya kazi.Ilimradi picha zionekane kwenye gazeti na wasikikwe wanafanya kazi. Sadly this is becoming a trend in bongo, longolongo nyiiiiingi, kazi hamna.

Unataka kuniambia sasa hivi hamna issues za maana kuliko hii? Where is their sense of priority? Where is their sense of economic resource allocation? Do they even know these concepts?
 
Thanks Mwl.
Ila hawa jamaa wanapindisha ukweli, magogo halisi huwa yanapitishiwa bandarini yakiwa ndani ya makonteina!

Nadhani ni kale katabia ka askari wetu kukimbilia wanyonge.
 
Thanks Mwl.
Ila hawa jamaa wanapindisha ukweli, magogo halisi huwa yanapitishiwa bandarini yakiwa ndani ya makonteina!

Nadhani ni kale katabia ka askari wetu kukimbilia wanyonge.

Nadhani ni ule ukweli kwamba wasionacho watanyanganywa hata kile kidogo walichonacho.

Hivi inakuwaje Polisi (ambaye ni masikini wa kutupwa) hupiga ua anapokamata mwizi wa simu ya mkononi, lakini humwonea haya mwizi wa bilioni 2 serikalini?
 
Wako watu walishukiwa kuwa wezi kwenye kituo cha mafuta Arusha na polisi wakawapiga risasi. Hukusikia hilo? Wako wafanyabiashara wadogo toka Mahenge walipigwa risasi na kuawa na polisi Dar es Salaam kwa kushukiwa kuiba fedha milioni chache. Hukusikia hiyo?

Polisi wanapokamata mtu anaitwa kibaka wanampiga kipigo cha mbwa. Lakini wezi wa mabilioni ya BoT, Ubalozini, na kwingineko serikalini hawapigwi hata kofi moja. Hujui hayo?
 
Mwalimu Augustine, na wewe unaboa wakati mwingine. Inakuwaje hujui tofauti ya kibaka wa kiselula na mjumbe wa kamati kuu ya CCM (NEC)? Hii ni sawa kabisa na mtoto wa miaka sita kuiba sukari jikoni na mzee wa nyumba kutumia pesa kuhudumia nyumba ndogo au kumtia mimba hausigeli. Yote ni makosa kwa wanafamilia: lakini utaanzia wapi bana? Mkubwa ni mkubwa tu siku zote hata ufanye nini kwenye jadi na mazingira ya Kiafrika.
 
(Angalia picha iliyoambatanishwa. Imetoka kwenye ippmedia.com, ikiambatana na habari kwamba Polisi wamekamata mashua (dhows) 8 zenye magogo mabayo yalikuwa yanapelekwa kusikojulikana)

It is pleasing to see that the Marine Police have finally found something they could outrun! You could probably stand on the shore, with gun at the ready, and order eight dilapidated dhows to sail back!

The picture tells quite a story. I see more rubbish than logs in there! Is the officer counting the number of logs or what? There are hardly thirty! I suspect that we are simply looking at a case of some villagers trying to transport a couple of logs to build huts with. Why should the impounding of that make headline news? Doesn’t the Guardian have real crime to report?

5582d1250226381-a-ferrymagogo.jpg

A picture says a thousand words, so it is known!

The picture tells quite a story. I see more rubbish than logs in there! Is the officer counting the number of logs or what? There are hardly thirty! I suspect that we are simply looking at a case of some.................................................................................."Ufinyu wa Mambo"
 
Wako watu walishukiwa kuwa wezi kwenye kituo cha mafuta Arusha na polisi wakawapiga risasi. Hukusikia hilo? Wako wafanyabiashara wadogo toka Mahenge walipigwa risasi na kuawa na polisi Dar es Salaam kwa kushukiwa kuiba fedha milioni chache. Hukusikia hiyo?

Polisi wanapokamata mtu anaitwa kibaka wanampiga kipigo cha mbwa. Lakini wezi wa mabilioni ya BoT, Ubalozini, na kwingineko serikalini hawapigwi hata kofi moja. Hujui hayo?

Sasa wakipiga risasi wahutumiwa wa ufisadi, tutabakiwa na nini?
 
....Inakuwaje hujui tofauti ya kibaka wa kiselula na mjumbe wa kamati kuu ya CCM (NEC)? ....

Tofauti yake kubwa ni kuwa wa kwanza (kibaka) anaiba kiselula ili akanunue unifomu za watoto,chakula, dawa hospitalini (hata Aspirini), ili aweza walea(mtunza) mama, baba mjomba na shangazi yake kijijini.

Mjumbe wa NEC ni ili ajenge hekalu lingine (la pili au la tatu) la mabilioni ya shilingi, halafu awapeleke watoto wakasome ulaya madigirii ya juu (Masters etc), ili wakirudi awahalilishie kupewa madaraka ya juu halafu nao waendelee kukomba zaidi ili nao wawapeleke watoto wao (wajukuu wa Mjumbe wa NEC) majuu na warudie kilichoanzishwa na babu au bibi yao!
 
Sasa wakipiga risasi wahutumiwa wa ufisadi, tutabakiwa na nini?
Tutabakiwa na vibaka wa simu barabarani na baada ya muda wataacha kuiba kwani hali ya maisha itakuwa si ngumu hivyo, kwani wale waliokuwa wanasababisha iwe ngumu hivyo kwa kukomba kila kitu watakuwa wamekwisha.
 
Tofauti yake kubwa ni kuwa wa kwanza (kibaka) anaiba kiselula ili akanunue unifomu za watoto,chakula, dawa hospitalini (hata Aspirini), ili aweza walea(mtunza) mama, baba mjomba na shangazi yake kijijini.

Mjumbe wa NEC ni ili ajenge hekalu lingine (la pili au la tatu) la mabilioni ya shilingi, halafu awapeleke watoto wakasome ulaya madigirii ya juu (Masters etc), ili wakirudi awahalilishie kupewa madaraka ya juu halafu nao waendelee kukomba zaidi ili nao wawapeleke watoto wao (wajukuu wa Mjumbe wa NEC) majuu na warudie kilichoanzishwa na babu au bibi yao!

Duuh! Hii kali! Ila naona wote ni vibaka tu ingawa nia yao moja: kuhudumia watoto, mke na familia kwa ujumla, au siyo?
 
Nadhani ni ule ukweli kwamba wasionacho watanyanganywa hata kile kidogo walichonacho.

Hivi inakuwaje Polisi (ambaye ni masikini wa kutupwa) hupiga ua anapokamata mwizi wa simu ya mkononi, lakini humwonea haya mwizi wa bilioni 2 serikalini?

Nchi hii ndio ilivyolaaniwa; wezi wa mabilioni wakienda mahabusu wanapewa vitanda na magodoro!! Kama huamini uliza kuwa wale wezi wa EPA na wakina Mramba mahabusu yao ilikuwaje?
 
Duuh! Hii kali! Ila naona wote ni vibaka tu ingawa nia yao moja: kuhudumia watoto, mke na familia kwa ujumla, au siyo?

Hapana mkuu, kundi la kwanza twawaita vibaka, na kundi la pili twawaitwa mafisadi!

Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa ingawa malengo yao yanafanana kwa juu juu, ki undani ni tofauti kabisa. Kundi la kwanza wanaiba ili waweze kuishi, na kundi la pili wanaishi ili waendelee kuiba, au tuseme wanaiba kwasababu tu wanaweza kuiba.:confused:
 
Makala iliyoambatana na picha ya polisi wanaoshikilia magogo ilisema Waziri husika ameahidi kufukuza watumishi kazi. Mbona miezi michache iliyopita kontena la meno ya tembo toka Tanzania lilikamatwa Manila na sikumsikia waziri akifura hivyo? Ni kwa vile wahusika wa hilo dili walikuwa wakuu wenzake?

Na ni tangu lini magogo yemkuwa "nyara za serikali"? Nina mitiki yangu michache nimeotesha Dar. Ikikomaa nikaikata na kuweka kwenye lori nikasafirisha kwenda Moshi nitakuwa nimetorosha nyara za serikali?

Hiyo mitumbwi haikuwa kwenye international waters. Kwa nini polisi waikamate? Ni kosa kwa wanavijiji kutumia usafiri wa majini? Na kwa nini waseme ilikuwa inakwenda kusikojulikana? Ilikuwa Tanzania, na ina uhuru wa kwenda popote Tanzania.

Acheni kuonea watu wadogo!

I support who says he can see rubbish than what is writen, IPP wanapenda sifa tu inawezekana hiyo ni show off tu, huyo police alitaka kupose apigwe picha atoke kwenye mtandao.

Its more than rubbish.
 
Kiukweli haya malalamiko hayatatusaidia kitu endapo wanajamii tusipobadilika na kuwa serious kwa huu utawala wetu wa kijanja janja!

Week end iliyopita kuna mjomba wangu mmoja amepigwa marungu na Askari wa kituo cha Kigamboni kwa kosa la kuuliza kwa nini alikuwa anakamata pikipiki na kuzuia raia wasipande na kusafirishwa!

Sasa haya ni baadhi ya matukio yanayodhihirisha kwamba, kumbe bongo mwizi mkubwa au jambazi mkubwa anatukuzwa, na wale wanaohoji haki zao wanaingia matatizoni!

Kilichobaki ni wananchi kuamka na kutafuta ukweli juu ya hawa tunaowaita wanausalama wetu, ambao tumewapa jukumu la kulinda mali zetu na usalama wetu kwa ujumla, asilimia 90 miongoni mwao hawana maadili ya kazi na wapo kibiashara zaidi!
 
Week end iliyopita kuna mjomba wangu mmoja amepigwa marungu na Askari wa kituo cha Kigamboni kwa kosa la kuuliza kwa nini alikuwa anakamata pikipiki na kuzuia raia wasipande na kusafirishwa!

Ni tumaini langu kwamba kulikuwepo na mashahidi. Mjomba wako awashikishe adabu hao maaskari kwa kuwashitaki kwa kosa la "attempted murder".

Hii kawaida ya Polisi wa Tanzania kukamata pikipiki au magari sijui wameileta wapi. Kunapokuwepo na traffic violation, kwa nini chombo kikamatwe? Ni mtu amekosa, sio chombo. Na chombo kinaweza kuwa cha mtu mwingine.

Traffic infringement (kama pikipiki kusafirisha abiria bila ruhusa) si kosa la jinai. Hakuna cha kukamata mtu au kitu hapo. Inatakiwa itolewe traffic ticket basi.

Lini tutaanza kuwa na utawala wa kisheria?
 
Back
Top Bottom