UFILIPINO: Rais Duterte atishia kuwaua Polisi wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu na kuwaita 'mizigo'

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Rais Rodrigo Duterte ametishia kuwaua makumi ya maofisa wa Jeshi la Polisi la Ufilipino (PNP) ambao wako chini ya uchunguzi kwa uhalifu katika hotuba iliyojaa dharau akilenga wahalifu ndani ya jeshi hilo.

Baada ya kuwapeleka maofisa wa polisi 102 eneo la Malacañang, Duterte, rais mwenye maneno ya ufedhuli, Jumanne aliwashambulia akisema “hawana maana” (na) mzigo kwa jamii.”

Majina ya maofisa wengi wa polisi waliopelekwa kwa Duterte yako chini ya uchunguzi kwa makosa makubwa ya uhalifu yakiwemo ya ubakaji, kuteka, kupotosha na kujihusisha katika biashara ya dawa za kulevya.

Wengine wanalalamikiwa kwa uongozi wa kizembe kama vile kutoweka kazini bila idhini wala likizo na kushindwa kuhudhuria kwenye majukumu ya kimahakama.

Duterte aliwaonya maofisa hao kwamba ikiwa wataendelea na vitendo vyao vya uhalifu itakuwa vema wakiuawa
 
Kuna nchi lazma uzitwale kibabe bila hivyo utatiwa dole(shule iko zanzibar hii)
 
Huyu Raisi ndo alitakiwa aje huku, maana hawa mapolisi kwa kubambikizia watu kesi na vitendo vya uonevu wanaongoza
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom