Ufaransa yatuhumiwa kutaka kuipindua Serikali ya Mali

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,887
Ufaransa yatuhumiwa kutaka kuipindua serikali ya Mali

Wanajeshi walioko madarakani nchini Mali wameituhumu serikali ya Paris kuwa imefanya ujasusi na njama za kuipindua serikali ya nchi hiyo. Hii ni kufuatia hatua ya jeshi la Ufaransa ya kuonyesha mkkanda wa video inayoonyesha harakati za jeshi la Mali katika kambi moja ya kijeshi katikati ya nchi hiyo.

Wanajeshi wanaoongoza Mali wametoa taarifa wakiwatuhumu wanajeshi wa nchi za kigeni hasa Ufaransa kuwa wameingia kwenye anga ya nchi hiyo kinyyume cha sheria zaidi ya mara 50 tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi sasa.

Mali imesema kuwa ndege isiyo na rubani (droni) ya wanajeshi wa Ufaransa, Aprili 20 mwaka huu wa 2022 iliruka kinyume cha sheria katika anga ya kambi ya kijeshi ya nchi hiyo.

Taarifa zinasema kuwa, picha iliyopigwa na droni hiyo inawaonyesha wanajeshi wa Mali wakisaidiana na mamluki wa nchi ajinabi kuzika miili ya watu karibu na kambi ya kijeshi ya Gossi, katikati ya Mali.

Siku moja baada ya kuonyeshwa video hiyo, jeshi la Mali nalo lilitangaza kuwa limegundua kaburi la umati karibu na kambi ambayo huko nyuma ilikuwa ikitumiwa na wanajeshi wa Ufaransa.

Wanajeshi wa Mali wanawatuhumu wenzao wa Ufaransa kuwa wamehusika katika umati ya raia kwa kisingizio cha mapambano dhidi ya ugaidi. Mwedesha Mashtaka wa Jeshi wa Mali pia ametoa habari ya kuanza uchunguzi kuhusu kaburi hiyo la umati lililopatikana karibu na kambi iliyokuwa ikitumiwa na wanajeshi wa Ufaransa nchini humo.

Mali ilikumbwa na hali ya mchafukoge tangu mwaka 2012 ambapo wanajeshi wa nchi ajinabi walioelekea nchini humo chini ya mwavuli wa kupambana na ugaidi wameshindwa kurejesha amani na kuyasambaratisha makundi ya kigaidi na waasi. Aidha nchi hiyo imekumbwa na mapinduzi mawili ya kijeshi tokea Agosti mwaka juzi hadi sasa.
 
Mali ni nchi masikini ya kiafrika lakini ni mwiba kwa Ufaransa.Inaendeshwa puta kisawasawa.
 
Huu mzozo ni baada ya Mali kukodisha mamluki wa Urusi kapambana na ugaidi.

Ina maana nchi zinazoendelea hazina haki ya kuchagua mshirika mpaka wakubwa wapende?
 
Hao Ufaransa washachokwa si waachane na Nchi za Afrika
 
Back
Top Bottom