Ufaransa Yashikilia Akaunti 9 za Benki za Rais wa Gabon | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufaransa Yashikilia Akaunti 9 za Benki za Rais wa Gabon

Discussion in 'International Forum' started by Pdidy, Feb 28, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,610
  Likes Received: 5,782
  Trophy Points: 280
  Ufaransa Yashikilia Akaunti 9 za Benki za Rais wa Gabon


  Rais Omar Bongo wa Gabon Friday, February 27, 2009 8:00 AM
  Mamlaka za Ufaransa zinashikilia akaunti tisa za benki za rais wa Gabon Omar Bongo zilizopo nchini Ufaransa zenye kiasi cha fedha kinachokadiriwa zaidi ya euro milioni nne.
  Hatua hiyo imefikiwa baada ya mahakama ya Bordeaux nchini Ufaransa kumuamuru rais Bongo kurudisha fedha alizopewa ili kumuachia huru mfanyabiashara wa Ufaransa Rene Cardona.

  Akaunti tisa za Rais Bongo katika mabenki ya Ufaransa zina kiasi cha fedha kinachosemekana zaidi ya euro milioni 4.

  Mfanyabiashara huyo wa Ufaransa aliachiwa huru baada ya mtoto wake kuingiza dola 580,000 kwenye akaunti ya rais huyo aliyekaa madarakani kuliko viongozi wote wa Afrika.

  Mwaka 1996, Rene Cardona alifungwa katika jela za Gabon baada ya kutokea kutokuelewana katika masuala ya biashara kati ya Rais Bongo na Cardena ambaye alimuuzia kampuni ya uvuvi na usafirishaji wa meli.

  Mtoto wa Cardona alipeleka malalamiko yake kwenye mamlaka za Ufaransa baada ya kumlipa fedha hizo rais Bongo ili baba yake aachiwe huru.

  Mwezi septemba mwaka jana mahakama ya Bordeaux, Ufaransa ilisema kwamba malipo aliyolipwa rais Bongo yalikuwa kinyume cha sheria na kumuamuru rais Bongo arudishe fedha alizolipwa na pia alipe fidia na gharama za kesi hiyo.

  Hukumu hiyo ilithibitishwa jumatatu na mwakilishi wa upande wa mashitaka Jean-Philippe Le Bail, alisema kwamba kwa mahesabu ya haraka haraka malipo yatakuwa zaidi ya euro milioni moja.

  "Akaunti tano za rais Bongo katika benki ya Credit Lyonnais na akaunti nne katika benki ya BNP zinashikiliwa na mamlaka za Ufaransa hadi hapo malipo yatakapofanyika.

  Wakili wa rais Bongo alisema kwamba mahakama ya biashara ya Libreville, Gabon ilimuhukumu Cardona kumlipa rais Bongo euro 900,000 kama fidia ya uharibifu wa kibiashara aliomsababishia.

  "Hali hii ilitokea baada ya kutokuelewana kibiashara kwa watu wawili ambao wamejuana kwa miaka mingi" alisema wakili huyo wa rais Bongo.

  Cardona, 75, alisema hana kinyongo na rais Bongo pamoja na kumtupa katika jela ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa siku 48 wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa ebola.
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa mafedha yote hayo ameweka nje, wakati nchini kwake watu ni masikini. Kwa kuwa si fedha halali hawaweki katika mabenki ya nchi zao ili wasijulikane, wangewekeza nyumbani ingesaidia mzunguko wa fedha. Wacha zizuiliwe, kwanza imesaidia wananchi kujua. Bado mijizi yetu ya TZ, ikitokea kama hii itakuwa poa sana, kwanza wakisikia habari kama hizo roho juu.
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Na ni tu mzee sasa..je mapesa yote atapeleka wapi???

  Halafu kwa nini majuu wanaruhusu hawa madikteta kufungua hizi ac ktk nchi zao in the 1st place?
   
 4. N

  Ng'wanamalundi Member

  #4
  Feb 28, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 90
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 25
  Labda hilo litakuwa fundisho kwa wengine wanaokuwa na mawazo kama hayo. Itafaa kama nchi nyingine zitaiga mfano huo.
   
Loading...