Ufaransa: Mkulima aandikisha Kondoo shule ili kuzuia shule isifungwe kutokana na uhaba wa Wanafunzi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Mkulima mmoja nchini Ufaransa amewaandikisha shule kondoo wake 15 ili kuongeza namba ya wanafunzi baada ya mamlaka za kijiji kimoja kutangaza kutaka kusitisha masomo.

IMG_20190508_204737.jpg


Shule ya Jules Ferry iliyopo kwenye kijiji cha Crêts-en-Belledonne, kwenye safu za milima ya Alps karibu na jiji la Grenoble, kimekuwa kikikumbwa na tatizo la kushuka kwa namba ya wanafunzi wanaoandikishwa kwa masomo.

Hali hiyo inatishia kufungwa kwa shule hiyo.

Lakini kama hatua ya kupinga kufungwa kwa shule, mfugaji na mkulima Michel Girerd ameamua kuwaandikisha baadhi ya kondoo wake kama wanafunzi.

Baadhi ya kwanafunzi hao ambao ni kondoo wanafamika kwa majina kama Baa-bete, Dolly na Shaun.

Bw Girerd alienda shuleni hapo akiwa na kondoo 50 kuhudhuria sherehe maalumu iliyohudhuriwa na watu 200 wakiwemo wanafunzi, walimu na maafisaa wengine.

IMG_20190508_205659.jpg


Meya wa eneo hilo, Jean-Louis Maret alikabidhiwa vyeti vya kuzaliwa vya 'wanafunzi' hao wapya. Pia akaonesha kukerwa kwake na suala la kutishia kufunga shule hiyo kutokana na uhaba wa wanafunzi.

"Sasa hakutakuwa na tishio la kufungwa kwa kitu chochote," moja ya wazazi Gaelle Laval amesema, na kuongeza kuwa mfumo wa elimu "hauangalii hoja zilizopo katika eneo hilo, na badala yake unaangalia idadi (ya wanafunzi) tu."

Wanafunzi waliohudhuria sherehe hiyo walibeba mabango yalikuwa na ujumbe kuwa: "Sisi siyo kondoo".
 
Haya mambo ya family planning yanawatesa wazungu. Magufuli alisema tuachane nayo.
 
Ubalozi wa ufaransa si wanipe visa jamani. Hapa nina watoto 10,na bado nipo fertile ninaweza kuzaa ishirini wengine. Hebu watupe visa tukasaidie shule isifungwe.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom