Ufaransa: Kwanini walinzi wa Rais Samia wanavaa Barakoa ya Zanzibar kwenye ziara ya Tanzania?

Magufuli alipendelea Chato tulipoongea mkasema kwani Chato sio Tanzania?

Sasa mama yenu alishasema yeye na jiwe ni kitu kimoja mnashangaa akivaa vya kwao Zanzibar sio Tanzania?

Mlizoea ujinga wa kusema maendeleo hayana chama wala ukanda haya pambaneni sasa MATAGA chipukizi na MATAGA wafiwa
Kunauwongo sana juu ya chato,,hakuna kitu chaaana labda uwanja wa ndege
 
Salaam Wakuu,

Nadhani Walinzi walitakiwa Kuvaa Barakoa zenye bendera ya Tanzania sio Zanzibar kwani, hii ni Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siku wakuambatana na Mwinyi ndo wavae hizi Bara K. Au ni Utalii wa Bluu?

Picha zimepigwa akiwa Paris, Ufaransa, wakati huo Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa akizungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha kuwezesha Wajasiriamali cha Station F Start Up Bi. Roxanne Varza pamoja na Meneja Mawasiliano wa Kituo hicho Bw. Grégoire Martinez kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa Kituoni hapo ikiwemo kutoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kupata elimu ya ubunifu wa kibiashara, fursa za mitaji yenye masharti rafiki pamoja na masoko wakati alipotembelea Kituo hicho leo tarehe 12 Februari, 2022, Paris nchini Ufaransa)
View attachment 2117285View attachment 2117286
View attachment 2118155
Wale walinzi labda ni Wazanzibari. Lakini nilikwenda Ikulu siku moja wakaniuliza kwa nini nimevaa barakoa nyeusi ambayo haifanani na nyingine. Sasa wao wamevaa hiyohiyo. But maybe this is not important. Isipokuwa in vizuri kunotice mambo kama haya. Inaonyesha you are observant.
 
Unaposema kuwa ripoti za tume ya Warioba na Nyalali siyo misahafu unakosea Sana katika kipindi hiki ambacho Wananchi wengi wamepata japo elimu ndogo tofauti Sana na enzi ya Nyerere.

Kumbuka kuwa hata hizo kero zilizoorodheshwa ni matokeo ya tafiti na tume hizo.

Unaposema kero ya Muungano ni suala ambalo kwa uthibitisho wa kitafiti jambo hilo ama linawakera au wanalihitaji watu walio wengi Sana kwa zaidi ya 80% kwa pande zote za Muungano.

Kwa maana hii nyepesi kupuuza uondoaji wa kero za Wananchi walizoziainisha wao wenyewe kupitia tume ni kuongeza kero kubwa zaidi inayohatarisha taifa kwa ujumla.

Matatizo mengi ya taifa letu yamekuwa yakisababishwa na serikali kupuuza mapendekezo ya tafiti na wataalam wa idara husika.
Muungano ni suala lenye baraka na lenye tija kila siku. Watu hutafuta sababu za kuungana, udhaifu kwenye muungano hauwezi kukosekana.

Suluhisho sio kila upande kutanguliza kiburi chake na ufahari wa ukubwa wa eneo lake. Haya yote yanakuja kwa kigezo cha SSH kuwa mzenji.

JPM alivyokuwa anaipendelea Chato hakuna hata mmoja aliyekumbuka kuwa ipo Zanzibar. Tuondokane na kuendekeza chuki kwa kigezo cha tume ya Warioba na ya Nyalali.
 
Bara hamjitambui. Mmekalia majungu, fitina na inda. Hakuna jambo linalowaweka pamoja watu wa bara.

Lkn wazanzibari linapokuja suala linalohusu nchi yao hawanaga uvyama. Wote wanaungana wanakuwa kitu kimoja

Acha wachangamkie fursa ya kuitangazq zanzt kupitia barakoa zao. Ninyi endeleeni na upuuzi wenu wa kumsingizia Mbowe kuwa ni gaidi.
Wazanzibar hawahawa waliowaleta mashehe wa uamsho bara ili wale msoto.
 
Kwa kiasi nakubaliana nawe kwa hoja kwamba Rais SSH amekuza sana tatizo.
Mfano, kero 11 kwanini zimefanywa siri kubwa? Zilijulikana ni 11 lakini hatujui zimeishaje.
Pili, hoja za Waziri Mchengerwa zimechangia sana. Kwa ufupi, kuanzia siku ya kwanza anasema , angalieni ''usawa wa pande zote'' ilionyesha Rais SSH alikuwa na kitu moyoni

Tume zimekusanya maoni ya Wananchi. Kama kuna kitu tofauti ni kipi kutoka kwa nani.

Kama kuna wanaopinga ni vema wakatuonyesha msingi wa kupinga.

Msingi wa hoja za Jaji Nyalali na Mzee Warioba ni maoni ya Wananchi, kuna nyaraka na takwimu. Tupatie kitu tofauti na hicho!!

Ndiyo lakini pia Jiografia inahusu. Kuhusu ukupe hilo halina ubishi.
Ikiwa hawawezi hata kulipa bili ya umeme na juzi wamepewa mkopo wa JMT wa maji, tuntasemaje?

Kumbuka katika muungano hawana mchango wowote kuliko tarafa au kata ya Tanganyika.
Kuhusu utalii kama wanaweza heri na hakuna wa kuwazuia, si kwa gharama ya Tanganyika

Hapana, kinachotokea ni pesa za Tanganyika kutumika kujitanua. Ni ukweli usio na shaka.

Kwa miezi chini ya 10 wamepata zaidi ya Bilioni 500. Kwa bajeti yao ya 1.2M kiasi hicho ni ziada. Pili, kinachoendelea ni kuuza visiwa wakijua ardhi ya bure ipo Tanganyika.

Tatu, ni kupitia uchochoro wa kukwepa kodi kwa mlango wa muungano! kama utakumbuka Magufuli alikataa hilo na kuweka kodi ili kulinda masilahi ya JMT!. Je, bado ipo hiyo?

Pamoja na yote utalii wa Zbar unategemea Tanganyika kama ilivyo soko la bidhaa na ajira.
Sultan wa Zanzibar alistawi kwas biashara ya pembe, utumwa n.k. si kwasababu ya Zbar!

Yes kwasababu wanasimama katika mstari. Kero 11 walizitazama katika jicho lenye busara kwasababu zililenga kumbebesha Mtanganyika mzigo zaidi.
Hebu tuambie kwanini zimemamalizwa Kimya kimya na kwa usiri mkubwa? kulikoni?

Uvumilivu kwa Tanganyika pekee! hapana, wakati umefika Tanganyika irejee kama Wananchi walivyosema wakiwemo Wazanzibar!

Je, si kweli kuwa hoja ya Tanganyika ililetwa na Wazanzibar ? na kwanini leo wapo kimya? Nini kimebadilika? Kero 11 zimemalizwaje? Kwanini kuna usiri mkubwa?
Tanganyika imeshakufa mkuu huko mtaani. Kama walishindwa kuifufua kina Jenerali Ulimwengu kipindi kile wakiwa na wabunge kwa kauli thabiti ya hayati Nyerere haupo uwezekano ikaweza kufufuka leo hii.

Ushauri wangu kwa Zenji ni kukuza sekta ya utalii kwa nguvu zao zote ili waweze kuondokana na hizi dharau humu JF.

Huu utanganyika wetu hauna mashiko, ni nchi inayoundwa akilini mwa watu kihisia zaidi, tukija katika kuifanya iwepo kiuhalisia haina kabisa misingi imara.

Masuala ya sultan ni ya zamani sana, wanaweza kujitegemea na kusimama wao kama wao.

SSH anavyozunguka huko nje ni kwa maslahi mapana ya JMT, hizi akili za kujitenga ni za kimaskini na zinachagizwa na chuki ambayo wenye akili wamekataa kuinunua.
 
Salaam Wakuu,

Nadhani Walinzi walitakiwa Kuvaa Barakoa zenye bendera ya Tanzania sio Zanzibar kwani, hii ni Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siku wakuambatana na Mwinyi ndo wavae hizi Bara K. Au ni Utalii wa Bluu?

Picha zimepigwa akiwa Paris, Ufaransa, wakati huo Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa akizungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha kuwezesha Wajasiriamali cha Station F Start Up Bi. Roxanne Varza pamoja na Meneja Mawasiliano wa Kituo hicho Bw. Grégoire Martinez kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa Kituoni hapo ikiwemo kutoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kupata elimu ya ubunifu wa kibiashara, fursa za mitaji yenye masharti rafiki pamoja na masoko wakati alipotembelea Kituo hicho leo tarehe 12 Februari, 2022, Paris nchini Ufaransa)
View attachment 2117285View attachment 2117286
View attachment 2118155
Mbona sioni tatizo?
 
Una roho ngumu sana hadi barakoa inakutesa ukiizela wewe lazima uwe mchawi

Sent from my VFD 600 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Salaam Wakuu,

Nadhani Walinzi walitakiwa Kuvaa Barakoa zenye bendera ya Tanzania sio Zanzibar kwani, hii ni Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siku wakuambatana na Mwinyi ndo wavae hizi Bara K. Au ni Utalii wa Bluu?

Picha zimepigwa akiwa Paris, Ufaransa, wakati huo Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa akizungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha kuwezesha Wajasiriamali cha Station F Start Up Bi. Roxanne Varza pamoja na Meneja Mawasiliano wa Kituo hicho Bw. Grégoire Martinez kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa Kituoni hapo ikiwemo kutoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kupata elimu ya ubunifu wa kibiashara, fursa za mitaji yenye masharti rafiki pamoja na masoko wakati alipotembelea Kituo hicho leo tarehe 12 Februari, 2022, Paris nchini Ufaransa)
View attachment 2117285View attachment 2117286
View attachment 2118155
Kwani zanzibar sio tanzania

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Ipo wazi kabisa kwa mujibu wa katiba ya JMT tuna dola moja tu la Tanzania na hii imewekwa wazi kwenye ibara ya kwanza ya katiba ya JMT.

Rais wa JMT anapifanya ziara nje ya Tanzania anaiwakilisha JMT na sio Zanzibar. Kwa hiyo ilipaswa kama ni kufanya branding basi bendera ya JMT iwe inatumika kwenye barakoa za walinzi wa rais.

Zanzibar kwa mujibu wa montevideo convetion on statehood ibara ya kwanza sio dora huru na haiwezi kutambulika kimataifa. Ndio maana hakuna balozi wa kudumu wa Zanzibar UN au hata huko Ufaransa.

Haya yanayofanyika kubrand bendera ya Zanzibara wakati kimataifa haitambuliki ni makofa na kuvunja katiba ya JMT.
View attachment 2118141
Hili ni kosa kubwa sana.

Huyo ADC kachemka.
 
Binadamu hamna jema kila kitu kibaya kwa huyu Mama na kwa kila Raisi aingiaye madarakani
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Huwezi kubadilisha Maji kuwa mafuta wala mafuta kuwa Maji Tanzania itabaki kuwa nchi na zanzibar ni sehemu ya Tz
 
Salaam Wakuu,

Nadhani walinzi walitakiwa kuvaa Barakoa zenye bendera ya Tanzania siyo Zanzibar, kwani hii ni ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siku wakiambatana na Mwinyi ndio wavae hizi barakoa au ni Utalii wa Uchumi wa Bluu?

Picha zimepigwa akiwa Paris, Ufaransa, wakati huo Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa akizungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha kuwezesha Wajasiriamali cha Station F Start Up Bi. Roxanne Varza pamoja na Meneja Mawasiliano wa Kituo hicho Bw. Grégoire Martinez kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa Kituoni hapo ikiwemo kutoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kupata elimu ya ubunifu wa kibiashara, fursa za mitaji yenye masharti rafiki pamoja na masoko wakati alipotembelea Kituo hicho leo tarehe 12 Februari, 2022, Paris nchini Ufaransa)
View attachment 2117285View attachment 2117286
View attachment 2118155
Mama Yaoo si Mzanzibari

Kiuchumi wa blue ni wapii???
Ukijua hayo hutouliza swali

Mwisho

Mama yoo katokea wapi ,alipandia ndege wapii
 
Tanganyika imeshakufa mkuu huko mtaani.
Si kweli, fungua katiba ya Zanzibar, Sura ya kwanza ibara ya 2. '' Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania''
Haya ni maneno ya Katiba ya Zanzibar 1984 toleo 2010.
Nchi moja ni Zanzibar , nikuulize ya pili ni ipi ikiwa Tanganyika ilishakufa mtaani?
Kama walishindwa kuifufua kina Jenerali Ulimwengu kipindi kile wakiwa na wabunge kwa kauli thabiti ya hayati Nyerere haupo uwezekano ikaweza kufufuka leo hii.
Hoja hii ni nzuri sana. Wakati wa Mwalimu suala la G55 lilikuwa wazi na liliongelewa kwa uwazi.
Mwalimu alisema ''
Sera za CCM ni serikali 2, wanaotaka sera tofauti waondoke ndani ya chama kwanza ili wakazungumzie huko'' Hapa maana yake hakukataa hoja, alisema kuwa hoja iliyopo ni kinyume cha sera wanayo inadi. Mwalimu alikuwa na nguvu za hoja

Kumbuka kabla ya hapo kulikuwa na hoja ya Watanganyika kwenda Zanzibar kwa Passport. Tanganyika ikasema ikiwa ni hivyo, Wazanzibar waje na Passport. Mwalimu Nyerere aliitazama hoja akaona ina mantiki. Mwl akawasiliana na Jumbe na sharti liliondolewa mara moja.
Mwl hakuwalazimisha Wazanzibar bali Wazanzibar waliona hasara !

Ninachokiona sasa hivi ni tofauti kidogo. Hoja 'hoja zinapigwa rungu hazijibiwi'' kumbuka asilimia zaidi ya 80 ni ya kizazi kilichokuta muungano. Hofu iliyopo ni kuwa wajenga hoja kama Mwalimu, na wasikiliza hoja kama Mzee Warioba hawapo tena. Sasa tuna ''wasifiaji na wakujipendekeza''
Hoja ya anganyika inafukuta na siku Watanganyika wakisema enough is enough hakuna wa kuwazuia. Wao ndio wenye muungano kwa hali na mali. Kuna mahali nimesema, kwa jinsi nionavyo, na ninaweza kuwa wrong! muungano uki survive miaka 5 utadumu miaka 50. Trust me!
Ushauri wangu kwa Zenji ni kukuza sekta ya utalii kwa nguvu zao zote ili waweze kuondokana na hizi dharau humu JF.
Hakuna tatizo la Zanzibar kustawi! kuna tatizo la ustawi wao kupatikana kwa gharama za Mtanganyika na hapo ndipo mjadala ulipo. Zanzibar waende kukopa Trilioni 100 hakuna shida, lakini wakikopa bilioni 280 na kumtupia Mtanganyika mzigo kuna tatizo.
Zanzibr hata wakiuza visiwa hata Ikulu hakuna tatizo, lakini uuzaji wao usibebeshe mzigo Mtanganyika kwa njia yoyote ile.
Huu utanganyika wetu hauna mashiko, ni nchi inayoundwa akilini mwa watu kihisia zaidi, tukija katika kuifanya iwepo kiuhalisia haina kabisa misingi imara.
Katiba ya Zanzibar sura ya kwanza ibara ya 2 na katiba hiyo hiyo imetaja muungano mara 36.
Tueleze wanaJF, ni sheria ipi na ya mwaka gani imetamka kuwa ''Tanganyika imekufa?''
Lakini pia katiba ya mpito ya 1964 ilisema '' ...mambo yote ya Tanganyika yatakuwa ya JMT'' in other word Tanganyika is subsumed by URT. Since
Masuala ya sultan ni ya zamani sana, wanaweza kujitegemea na kusimama wao kama wao.
Ndicho tunataka! Wajitegemee bila kumpa Mtanganyika gharama. Kwasasa Zanzibar inachukua sehemu kubwa sana ya bajeti ya JMT kuliko eneo lolote la Tanganyika ikiwa na mchango SIFURI, zero, Nada, Nil katika muungano
SSH anavyozunguka huko nje ni kwa maslahi mapana ya JMT, hizi akili za kujitenga ni za kimaskini na zinachagizwa na chuki ambayo wenye akili wamekataa kuinunua.
Hoja ni kuwa muungano unageuka kuwa mzigo kwa Tanganyika. Kinachotakiwa na uwajibikaji wa Zanzibar katika muungano. Kuhusu chuki hakuna kitu kama hicho bali zipo hoja kama hizi
1. Nini mchango wa Zanzibar katika JMT?
2. Ikiwa Zbar ambaye ni mshiriki wa JMT yupo, Tanganyika yupo wapi na Zbar inajadiliana na nani?
3. Katika JMT, masilahi ya Tanganyika yanalindwaje na kusimamiwa na nani?
3. Tueleze tamko lililoua nchi ya Tanganyika na ni kwa sheria ipi
4. Kero za muungao zimemalizwaje na kwanini imebaki siri kubwa
5. Tume ya Jaji Nyalali, Jaji Kisanga na Jaji Warioba na maoni ya Wananchi zinataka serikali 3, tueleze ni utafiti au tume gani nyingine yenye maoni tofauti na hizo
 
Back
Top Bottom