Ufaransa: Kwanini walinzi wa Rais Samia wanavaa Barakoa ya Zanzibar kwenye ziara ya Tanzania?

Pamoja na kujadili wajumbe wa ziara walivyovaa, muhimu zaidi tujue nini kilichojadiliwa na kukubaliwa. Isije kuwa masuala ya ulinzi wa bahari yetu wakapewa Wafaransa kwa hoja kuwa wanatusaidia kulinda uchumi wa buluu. Manowari za Wafaransa zikiruhusiwa kuja kuweka kambi huku kwetu basi itakuwa ngumu sana kuwadhibiti iwapo wataamua kutuhujumu. Ni angalizo tu....
 
Salaam Wakuu,

Nadhani walinzi walitakiwa kuvaa Barakoa zenye bendera ya Tanzania siyo Zanzibar, kwani hii ni ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siku wakiambatana na Mwinyi ndio wavae hizi barakoa au ni Utalii wa Uchumi wa Bluu?

Picha zimepigwa akiwa Paris, Ufaransa, wakati huo Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa akizungumza na Mkurugenzi wa Kituo cha kuwezesha Wajasiriamali cha Station F Start Up Bi. Roxanne Varza pamoja na Meneja Mawasiliano wa Kituo hicho Bw. Grégoire Martinez kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa Kituoni hapo ikiwemo kutoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kupata elimu ya ubunifu wa kibiashara, fursa za mitaji yenye masharti rafiki pamoja na masoko wakati alipotembelea Kituo hicho leo tarehe 12 Februari, 2022, Paris nchini Ufaransa)
View attachment 2117285View attachment 2117286
View attachment 2118155



Raisi ame ingia mikataba huko mikubwa badala ya kuulizia mikataba ina nini? Mikataba ya nini? Tunaongelea majina ya barakoa halafu mnataka hawa watu watuone tupo serious.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom