Ufaransa kuandamana kupinga sheria mpya inayowalinda polisi wanapowakamata watu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Maandamano yanafanyika nchini Ufaransa katika maeneo kadhaa hii leo.

Hayo ni baada ya serikali kutangaza sheria mpya ambayo itazuia watu kutumiana picha za maafisa wa polisi wanapowakamata watu.

Sheria hiyo imetangazwa siku chache baada ya video kusambaa kote nchini humo ikimuonesha polisi aliyekuwa akimpiga na kumtukana kwa maneno ya kibaguzi mwanamume mweusi.

Tukio hilo limeishtua Ufaransa nzima huku watu mashuhuri pamoja na wanasiasa wakimlaani afisa huyo wa polisi. Tukio hilo pia limezua mjadala mkali juu ya sheria hiyo mpya ya Rais Emmanuel Macron.

Macron hapo jana, alisema kitendo cha afisa huyo wa polisi ni shambulio lisilokubalika na kuitaka serikali yake kutafuta njia za kukabiliana na tatizo la ubaguzi.

Moja ya mambo yenye utata zaidi ya sheria hiyo mpya ni Ibara ya 24, ambayo imesema ni kosa la kihalifu kuchapishaji picha za maafisa wa polisi wakiwa kazini kwa nia ya kudhuru uadilifu wao wa kikazi au kisaikolojia.
 
Back
Top Bottom