Ufanyike utafiti dhidi ya ukabila katika sehemu za kazi

kabindi

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
333
120
Pamoja na kwamba Tanzania inasifika kwa kutokuwa na ukabila na athari zitokanazo na ukabila, unaitajika utafiti wa kutosha kuthibitisha hayo!. Zamani wahaya walizungumzwa sana kwa tabia hiyo lakini kwa ujumla kuna tatizo kubwa kwa makabila mengi nchini. Fanyeni utafiti mdogo ambapo kiongozi ni Mchaga, Mpale, Myakyusa, Mhehe, Msukuma, Mungoni na mengine mengi, chunguza waajiriwa utagundua ninachomaanisha. Kua visingizio vya elimu na kufaulu Interview ambavyo siyo issue kwa sasa kwani Wasomi wamekuwa wengi kila kona na wenye sifa. Kuna mchezo mchafu wa ajira za upendeleo ambapo watu kabla ya kuajiliwa wanaanza kama ajira za muda ambazo huwa hazitangazwi na hasa Serikalini kwa kisingizio cha uhaba wa watumishi. wanapopata kibali cha kuajiri kutoka Utumishi uzitangaza nafasi hizo na wanaopewa kipaumbele ni wale waliokuwa wanafanya kazi kwa ajira za muda ambao waliingizwa kwa kujuana. Kupata kazi Serikalini ni Issue kubwa ndugu zangu! Unamjua nani ndo utapata kazi!
 
Back
Top Bottom