Ufanye nini ili usikate tamaa na upate nguvu ya kusonga mbele?

Kila Jambo na wakati wake, wakati unakuwa haujafika. Mafanikio huja taratibu baada ya kuanguka na kuinuka mara kadhaa ndio maana ya usikate tamaa. Kila unalolifanya hata kama hujafanikiwa ni hatua kuelekea kwenye mafanikio kwani utakuwa umejifunza kitu na unaporudia tena kinakuwa Bora zaidi na zaidi hatimae utafanikiwa.
Mfano mdogo mtoto anapojifunza kutembea huanguka mara Kwa mara lakini hatima anaweza na kuwa mkimbiaji hodari. Kitu cha kujiuliza je angekata tamaa baada ya kuanguka mara kadhaa na aseme siwezi tena kutembea ingekuwa?. Tusikate tamaa mafanikio ni mchakato tusiishie njiani Hadi pumzi itakapoishia.
 
Kukata tamaa ni akili yako kufikia mwisho wa kutatua tatizo
Suluhu ni kuwa na watu wa karibu unaowaamini tu.
Yawezekana ulipoishia wewe ndo mtu wako wa karibu alipoanzia, au tatizo ulilo nalo amewahi kukutana nalo.
Ndiyo maana katika maisha inatakiwa uwe na watu au mtu unayemwamini na unaweza mwambia baadhi ya siri zako
Kwa kuongeza ni kuwa usisubiri mpaka ukate tamaa ndo utafute suluhu, kadili unavyokwenda kama huoni mbele unaomba mwanga kwa nduguyo.
 
Andika sehemu ambayo kila siku utakua unaona ukichoandika....au kila siku ukiamka jinenee maneno unayotaka wewe...
Jambo likikushinda lipunguze punguze liwe dogo uendelee nalo!(usitamani kuwa na lavish life kumbe hata mshahara unaopata haufiki tarehe 1.

Au biashara uliyonayo faida unamalizia kwa starehe..unatamani kuwa mwanafunzi bora unapuyanga tu husomi ..)
Ingia Youtube huko utakutana na inspirations za kutosha( mie ni mfuasi mkubwa wa platform ya TedEx)
Soma kila siku kitabu.

Angalia wapi unakosea(hapa ukweli wengi tunajikosea sana lakini hatupo tayari kukiri). Kiri kila unapoharibikiwa mambo yako..yaan hii itoke ndani ya nafsi yako(andika kabisa...mie fulani nikipata hela ni dhaifu sehemu hii na hii..je nitaiachaje? Anza sasa kupangua mwenyewe utajichomoaje! La mwisho unayoyaandika kila wakati yasome kila mara

Jinuie kabisa...binafsi mie kwa siku nadhani naongea neno hilo hilo kuwa sitaki umaskini... Iwe na nayemjua au la! Siupendi umaskini na siutaki! Pia la mwisho kbs achana na marafiki wasio na msaada wowote kwako...achana na mitandao isiyo na lazima kwako haikusaidiii kitu..! Be postive....kuwa smart! Jifunze kwa walio mbele yako...hakika utaona njia yako ina mwanga mbele!(usiwe na tamaa)!acha woga!
Nimekuelewa mkuu
 
Kukata tamaa ni akili yako kufikia mwisho wa kutatua tatizo
Suluhu ni kuwa na watu wa karibu unaowaamini tu.
Yawezekana ulipoishia wewe ndo mtu wako wa karibu alipoanzia, au tatizo ulilo nalo amewahi kukutana nalo.
Ndiyo maana katika maisha inatakiwa uwe na watu au mtu unayemwamini na unaweza mwambia baadhi ya siri zako
Kwa kuongeza ni kuwa usisubiri mpaka ukate tamaa ndo utafute suluhu, kadili unavyokwenda kama huoni mbele unaomba mwanga kwa nduguyo.
Ahsante ndugu kwa ushauri mzuri.
 
Kila Jambo na wakati wake, wakati unakuwa haujafika. Mafanikio huja taratibu baada ya kuanguka na kuinuka mara kadhaa ndio maana ya usikate tamaa. Kila unalolifanya hata kama hujafanikiwa ni hatua kuelekea kwenye mafanikio kwani utakuwa umejifunza kitu na unaporudia tena kinakuwa Bora zaidi na zaidi hatimae utafanikiwa.
Mfano mdogo mtoto anapojifunza kutembea huanguka mara Kwa mara lakini hatima anaweza na kuwa mkimbiaji hodari. Kitu cha kujiuliza je angekata tamaa baada ya kuanguka mara kadhaa na aseme siwezi tena kutembea ingekuwa?. Tusikate tamaa mafanikio ni mchakato tusiishie njiani Hadi pumzi itakapoishia.

Umeandika vyema mkui...sure success is a process
 
Nilishawahi kufanya biashara ya partnership ile biashara mwisho wake haukuwa mzuri, biashara ambayo niliwekeza mtaji wa milioni 6, ule mwisho nilijikuta na Tsh laki 2 tuu mkononi.

Ile partneship ikavunjika, nilijihisi nimebeba dunia kichwani, maswali yasiokuwa na majibu nitasurvive vipi, nilikata tamaa ya kuishi, nilijilaumu sana kuingia kwenye ile biashara.

Ni miaka kama 6 imeshapita tangu huo mkasa utokee, Leo najitegemea kibiashara na nimejipanua zaidi.

JIBU NI KWAMBA SIKUKATA TAMAA

Pole na hongera..! Mie nimekuwa na ngozi ngumu sana yaani!>bora kuikubali hali mapema na usonge mbele..! Daily nasem kikubwa ni afya!.hongera ulipofikia
 
Imepita takriban miaka miwili tangu tumeijadili Topic hii, na mchango wenu umeweza kuwa msaada mkubwa sana kwangu, kila nlipokua naona nakwama na kuvunjika Moyo, nlikua narudi hapa kujikumbusha mambo kadhaa, Napata nguvu mpya, kisha naendelea na Mapambano!
MUNGU ni mwema sku zote Maisha yanaendelea,

Tuzidi kupambania "Good life"
 
Kingine jiburudishe na yale yanayokufurahisha ili kupunguza uchungu wa magumu unayopitia
Mf mazoezi,mziki,gardening,kupika,usafi,ibada nk...ama waweza muona therapist hali ikizidi kuwa mbaya

Bora uhai, ishi tu kwa ratiba maalum inayokupendeza
Nothing is constant
 
Back
Top Bottom