Ufanisi kazini(biashara)

misha

Member
Nov 19, 2010
59
7
Miaka zaidi ya kumi iliyopita, nilikuwa likizo DSM jumapili moja nilikwenda Kanisani nikakutana na ndugu yangu ambaye tulikuwa hatujaonana muda mrefu,basi tukakubaliane nikamwone kesho kutwa yake kazini kwake saa saba kasoro; jumatatu nilikuwa nazunguka mitaani nikakutana na muuza vitabu-vilivyotumika tukaongea kidogo akanieleza biashara yake ilikuwa haitoki na kunieleza kuwa alinunua mali kwa elfu 40,ingawa sikuvipenda vitabu vyote niliona ni muda wa kujijengea maktaba, tukakubaliana nikanunua kwa elfu 50. Kulikuwa na kitabu cha ufanisi kazini nikakisoma usiku mzima na kukifanyia notisi,kesho yake nikawa nacho ili nikipitie zaidi na niziangalie tena notisi nilizotengeneza,saa sita muchana niliondoka Maktaba ya Taifa na kwenda kwenye 'appointment' yangu na ndugu yangu,bila kujua jamaa yangu alikuwa 'busy' na alikuwa amepanga kunisalimia na kunieleza tukutane nyumbani kwake,baada ya kusalimiana nikampatia stori ya mabadiliko yaliyokuwa yakitokea katika shirika la Bima-baadhi yake ilikuwa mfanyakazi akichelewa Meneja wake alikuwa anapaswa kumchukua mapokezi na kujilizisha na sababu alizopewa,kama hazikumpendeza, mfanyakazi alirudishwa nyumbani na kupewa onyo;nikamweleza jamaa yangu kutofurahishwa kwangu na mtazamo huo,tukaishia kuongelea ufanisi kazini kwa kina,cha ajabu akanieleza kazini kwao kulikuwa na shinikizo kama hilo na baada la lunch(saa nane) walikuwa na mkutano wa management akanishukuru na kuniomba azitumie notisi nilizoandika kama nondo kwenye kikao--kwa bahati nzuri akawashawishi wakurugenzi wenzake wasianzishe sera hizo. Majuzi jamaa yangu alinikumbusha kuhusu maongezi yetu,na kunieleza kuwa shirika la Bima bahati mbaya lilikuwa mahututi na motisha wa wafanyakazi hoi. Tulichojifunza(mimi na jamaa yangu) ni kuwa ufanisi unategemea mambo mengi ukiwemo kuvumiliana,ubunifu na zaidi ya yote ufundi wa kuibashiri na kuisoma hali halisi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom