Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,372
- 6,078
Baada ya Mfalme Salman bin Abdulaziz kutengeua nafasi ya mrithi wake Crown Prince Mohamed Bin Nayef na kumteua mtoto wake Waziri wa Ulinzi Mohamed bin Salman kuwa mrithi wake kumeleta mtafaruku mkubwa katika familia hiyo ya kifalme toka nchi hiyo iasisiwe mwaka 1932.
Mfalme wa sasa Salman bin Abdulaziz ndio mtawala wa mwisho kutoka watoto wa mwaasisi wa ufalme huo Abdualiziz bin Saud. Kuteuliwa kwa mwana mfalme huyo kuwa mrithi wa kiti cha ufalme imeonekana kama Mapinduzi dhidi ya kurithi ufalme huo kwani wakati Mfalme Salman alipochukua Kiti hicho mwaka 2015 alimteua Prince Mohamed Bin Nayef kuwa mrithi wake.
Mohamed bin Salman mwenye umri wa miaka 31 ni mtu ambaye ameleta utata mkubwa kwenye sera za nje za nchi hiyo kwani mpaka sasa anaendesha vita dhidi ya Yemen na ametishia kuanzisha vita na Iran. Pia anadaiwa ndio muhusika mkuu kwenye mgogoro wa Qatar na Saud Arabia.
Uko wa kifalme wa Saud Arabia unakisiwa kuwa idadi ya watu 15000 lakini wenye utajiri mkubwa kwenye familia hiyo inakisiwa ni watu 2000.