Ufahamu wa hisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufahamu wa hisa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Adm, Jul 29, 2011.

 1. A

  Adm Senior Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Jamani wanajf wenzangu,mimi ni mmojawapo kati ya watanzania walio wengi ambao ninaamini kuwa hatuna ufahamu juu ya masuala ya hisa. Sasa jamani naombeni mnisaidie haya machache nisiyoyafahamu, 1.Hisa ni nini? 2.Mtu anaponunua hisa anafaidika vipi na hilo? 3.Nikitaka kujua taarifa za masoko ya hisa nifanye nini?
   
 2. D

  Danniair JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  1.Hisa ni nini? Kila co. huwa inatangaza mtaji wake. mtaji huu waanzilishi wa co. huugawa ktk vipande (hisa). Mf. mtaji wa co. ni Tshs 10,000,000. vipande 1000. kisha waanzilishi kupitia Memorundun & Articles of Association (hizi ni hati za kisheria) hutangaza kiasi cha hisa watakazo miliki/nunua. Kwa mfano 10,000,000/1000 =Tsh 10,000 ndio kusema basi kuna hisa 1000 za kiasi cha Tsh10,000 kila hisa. Tuseme co. ina waanzilishi 3 wanaomiliki hisa kama hivi A 400, B 300, C 200, D Hisa zisizomilikiwa (na waanzilishi) ni 100, ukijumlisha =hisa 1000. Ndo kusema kama kampuni itahitaji kiasi cha tsh. 5,000,000 basi hisa 500 lazima zibadilishe kuwa pesa kwa utaratibu waliojiwekea kisheria. mf. A atanunua /kutoa hisa 150 ambazo ni kiasi cha Tsh 10000 x 150 =1,500,000. B hisa 100 x 10,000 = 1,000,000/=. C hisa 200 x 10,000 =2,000,000/=. Jumla wamenunua wote Hisa 150 +100 + 200 =450. Bado Hisa 50. Kwa hiyo watakwenda kwenye soko la Mitaji kuuza hisa 50 zinazotokana na hisa 100 (D).

  Ukiwa na Tsh 10,000 utanunua hisa moja katikta co. hii, nk.

  2. faida; uanakuwa mmiliki wa co. hiyo na utapata faida inayoitwa dividend. Hii ni faida baada ya kulolewa mahitaji na madeni ya kampuni ktk kipindi muafaka ikiwemo na kodi.

  3.Habari za masoko; Nenda pale Maktaba ya taifa ulizia wapi soko la mitaji lilpo watakuelekeza, humo utapata maelezo.

  NB; umiliki wako wa co. unaendana na kiasi cha hisa ulizonunua hata kama wewe ni mwanzilishi. Waanzilishi hufika mahali wakashindwa au kukataa kununua/kutoa pesa sawa na hisa wanazomiliki, hivyo hisa hizo hupelekwa kwenye soko la mitaji
   
Loading...