beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1646046145625.png

Unasababishwa na Kirusi cha Polio kinachoambukizwa kutoka kwa mtu aliyeathirika kwenda kwa mwingine kwa kunywa/kula chakula au kinywaji kilichochafuliwa na kinyesi chenye vimelea vya Ugonjwa.

Virusi huzaliana katika utumbo na huweza kuathiri mfumo wa fahamu ikiwa ni pamoja na viungo kupooza ghafla, na hata kupelekea kifo. Watoto chini ya miaka mitano huathiriwa zaidi na Ugonjwa huu.

Ugonjwa huu hauna tiba. Nja kuu ya kuzuia ugonjwa huu ni kuwapatia watoto chanjo ya Polio iliyotengenezwa maalum kukinga ugonjwa huu. lli kupata kinga kamili dhidi ya ugonjwa wa Polio, chanjo hutolewa kwa dozi 4 ambapo dozi ya kwanza hutolewa mtoto anapozaliwa, ya pili anapofikisha umri wa wiki 6, ya tatu wiki 10 na ya nne wiki 14.

Ni muhimu mtoto akamilishe ratiba ya chanjo kama inavyotakiwa ili apate kinga kamili na ni muhimu pia watoto wote walioko katika jamii zetu wawe wamekamilisha upataji wa chanjo hiyo. Njia nyingine za kuweza kuzuia ugonjwa huu ni kutumia maji safi na salama na kuzingatia usafi wa mikono na mazingira.

Chanzo: Wizara ya Afya

=====

Poliomyelitis (polio) is a highly infectious viral disease that largely affects children under 5 years of age. The virus is transmitted by person-to-person spread mainly through the faecal-oral route or, less frequently, by a common vehicle (e.g. contaminated water or food) and multiplies in the intestine, from where it can invade the nervous system and cause paralysis.

In 1988, the World Health Assembly adopted a resolution for the worldwide eradication of polio, marking the launch of the Global Polio Eradication Initiative, spearheaded by national governments, WHO, Rotary International, the US Centers for Disease Control and Prevention (CDC), UNICEF, and later joined by the Bill & Melinda Gates Foundation and Gavi, the Vaccine Alliance. Wild poliovirus cases have decreased by over 99% since 1988, from an estimated 350 000 cases in more than 125 endemic countries then to 175reported cases in 2019.

Of the 3 strains of wild poliovirus (type 1, type 2 and type 3), wild poliovirus type 2 was eradicated in 1999 and no case of wild poliovirus type 3 has been found since the last reported case in Nigeria in November 2012. Both strains have officially been certified as globally eradicated. As at 2020, wild poliovirus type 1 affects two countries: Pakistan and Afghanistan.

The strategies for polio eradication work when they are fully implemented. This is clearly demonstrated by India’s success in stopping polio in January 2011, in arguably the most technically challenging place, and polio-free certification of the entire WHO Southeast Asia Region in March 2014.

Source: WHO
 
Mtoto Wangu ana miaka minne naa alishamaliza hizo chanjo zote za Polio mwaka 2018. Je anatakiwa kupata tena chanjo? Maana shuleni Kwao wametuletea Barua ya Kukubali au kukataa.
 
Nipo hapa chamazi kuna mtu anapita na spika. Wenye uelewa na hii taarifa naomba ufafanuzi.
 
Unataka uhalali wa chanjo au uhalali wa taarifa? Kama ni matone ya chanjo ni halali, Ila kama ni uhalali wa taarifa serikali ya mtaa inahusika kwa uzembe ikiwa hukuwa na taarifa.
 
Polio imerudi kwa kasi sana, Kama una mtoto chini ya miaka mitano ni vizuri apate matone hayo.

Usikatae ni kwa ajili ya mtoto
Polio mbaya sana
 
Zoezi la chanjo ya porio linasimamiwa na wenyeviti na ndiyo wahamasishaji wakuu katika maeneo yao, sasa ulitaka magari ya matangazo yapite kila mtaa ili Hali kuna zoezi jingine la Sensa linafanyika.
 
Mleta mada una kiwango Cha elimu mpaka ushindwe kujua maana ya chanjo na utendaji wa serikali ya mtaani kwako. Umewahi kushiriki mkutano wa maendeleo mtaani kwako au hujui nini maana ya serikali ya mtaa.
 
nyie ndio wale wa mawazo ya marehemu jiwe ya kujifukiza na kula tangawizi na malimao, science never lie ,acheni ujinga watoeni watoto wapewe matone
 
Back
Top Bottom