#COVID19 Ufahamu ugonjwa wa COVID 19

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
19,526
37,941
Mwezi uliopita nikiwa jikoni naandaa chakula cha jioni kwa ajili ya familia kulitokea ubishani mkali kati yangu mimi na mwanangu Mcdonald kuhusu umuhimu wa yeye kunawa mikono akitoka kwenye michezo yake katika mabishano hayo kijana wangu alijaribu kubishana na mimi asiamini chochote nachomuelekeza kuhusu COVID 19 mpaka kupeleka mwanangu swalehe aamke kuja kuona kulikoni huku jikoni ni mboga zimeungua tena au kaka mkubwa kashaiba tena nyama.

McDonald alikua mbishi alikua haamini, moja kuhusu chanjo za corona na mbili alikua anaamini kabisa kwamba corona ni ugonjwa wa kutengeneza nlipojaribu kumchunguza zaidi niligundua hizi ni story ambazo yeye na mwenzake huwa wanapiga wakiwa shule na story hizi huwa na taarifa nyingi ambazo sio sahihi kutokana na wao kusikia story nyingi ambazo sisi wazazi huwa tunaziongea nikagundua kwamba tatizo ni Jamii kukosa elimu na taarifa sahihi kuhusu ugonjwa huu.

Nilitumia muda wa kula chakula kuwaelekeza yeye na mdogo wake COVID 19 ni nini haswa, ukweli kuhusu chanjo yake na njia kadhaa za kujikinga na ntatumia jukwaa hili kutoa elimu niliyowapa wanangu ili tujikinge na tuwakinge wengine.

COVID 19 NI NINI?
COVID 19 husababishwa na kirusi cha "SARS COV 2 '' ambacho kipo katika kundi la virusi aina ya CORONA VIRUSES, kundi hilo ni kubwa lina virusi zaidi ya mia moja na katika virusi hivyo virusi vya aina nne ndio husababisha magonjwa ya upumuaji na vingine magonjwa mengine ambayo sio ya upumuaji, watu wengi katika jamii yetu hufikiri kwamba corona ni ugonjwa ambao umetokea ghafla tu lakini ukweli ni kwamba dunia imekua na virusi vya corona tangu enzi na enzi na virusi hivi vimekua na tabia ya kujibadilisha badilisha ili viweze ku stahimili mazingira mbali mbali (SURVIVING )

Mwaka 2002 na mwaka 2012 kulitokea milipuko ya SARS na MERS (middle eastern respiratory syndrome) na milipuko yote ilipelekea matatizo ya upumuaji MERS ilikua inasambazwa kwa kupitia wanyama haswa ngamia.

Kwahiyo tunaona kwamba CORONA VIRUS sio kirusi kipya bali ni kirusi ambacho wanasayansi tumekua tukikiTAFITI kwa muda mrefu mpaka sasa

COVID 19 HULETAJE MATATIZO YA KUPUMUA?
Kirusi hichi kinapoingia kwenye mwili wa binadamu , kinga ya mwili hujaribu kupambana nacho hii ni tabia ya kawaida ya mwili pale unapovamiwa na kitu ambacho mwili huhisi ni adui mwili hupeleka kinga zake za asili kupambana na hicho kitu kisayansi huitwa " INFLAMMATORY REACTION "

Madhara ya kirusi hichi huonekana sana kwenye mapafu kwani huko ndiko hupenda kwenda kuweka makazi yake na kinga za mwili huamua kuvifuata virusi vya korona huko huko.

na mfumo wa utendaji wa kinga za mwili huhusisha maji kutoka kwenye mishipa ya damu na kwenda hilo eneo kwa hiyo maji hutoka kwenye miishipa ya damu iliyopo kwenye mapafu na kujikusanya kwenye mapafu hivyo mtu hushindwa kupumua pia virusi hivi vinaweza kusambaa kwenye mwili na kwenda kuleta madhara sehemu nyingine (SEPSIS )

VIPI JE KUHUSU CHANJO?

Kumekua na maswali mengi kuhusu chanjo mfano wa maswali hayo ni

1.
Kwanini hizi chanjo zimetumia muda mfupi kutengenezwa ukilinganisha na zingine? Kujibu hili swali inabidi tukumbuke hapo juu tumesema kwamba virusi hivi viligunduliwa muda mrefu umepita kidogo takribani miaka hamsini iliyopita, wanasayansi tulielewa mengi kuhusu virusi vya korona na kulikua kuna juhudi za kutengeneza chanjo ya kundi la MERS tuliloliona hapo juu . taarifa za kundi hilo lilipelekea chanjo ya virusi vinavyosababisha COVID 19 igunduliwe haraka.

Mwaka 2019 tarehe 31 DECEMBER kirusi hichi kilipongunduliwa wuhan kwa kutumia teknolojia ya "GENOMIC TYPING" PIA MATUMIZI YA " SUPER COMPUTER" yalifanya muundo wa kirusi hichi kijulikane haraka sana

2.
Kwanini wanaopata chanjo bado wanaweza kupata maambukizi mapya? Unapopata maambukizi seli nyeupe baadhi hupambana na yale maambukizi yaliyokuja na zingine hutengeneza kinga mwili kwamba yule adui akija tena tumtambue haraka na tumuondoe , kinga mwili zinazotenezwa na mwili baada ya mavamizi ya virusi vya korona hukaa kwa muda mfupi na hapo ndipo tunahitaji chanjo ya COVID 19 kwa sababu kinga mwili zake zitakaa muda na zitasaidia zaidi kupambana na virusi hivi. Kwahiyo hii chanjo haikukingi wewe usipate COVID 19 lakini inakukinga wewe usipate madhara makali zaidi iwapo utaumwa COVID 19 hii ni muhimu sana kwa sababu itapunguza viifo na usambaaji wa huu ugonjwa na pia mahitaji ya mitungi ya gesi itapungua mahospitalini

3.
Je, ni kweli chanjo hubadili muundo wa vinasaba vyetu DNA ", sio rahisi kwa chanjo kufikia kiini cha seli (nucleus) kwani hapa ndipo DNA zilipo, chanjo zinapoingia kwenye mwili wa binadamu huishia kwenye cytoplasm na haziweki kufika kwenye kiini cha seli ni sawa na wewe mgeni akija nyumbani kwako ataishia sebuleni (CYTOPLASM) na hatoingia chumbani kwako wewe na wife (NUCLEUS, KIINI CHA SELI)

Chanjo pia inashauriwa wapate wazee kwa sababu wazee kinga zao za mwili zinakua zimepungua kwa kiasi kikubwa hivyo watahitaji chanjo ili kupandisha kinga mwili zao na wazee wetu ndo kundi linalopata changamoto zaidi

MWISHO VAA BARAKOA, FANYA MAZOEZI, NAWA MIKONO MARA KWA MARA, JARIBU KUTAFUTA WATAALAMU WAKUELEKEZE ZAIDI

TUTAMSHINDA ADUI HUYU MDOGO ASIYEONEKANA
 
Wewe baba ina maana mambo ya familia unayaleta huku?

Anyway, mimi na mdgo wangu Swalehe tushasema atuchanjwi.

Chanjwa wewe na mama inatosha.
#NasimamaNaGwajima
 
Wafuasi wa Kanisa la ufufuo na uzima wanakuja kwa sipi kali sana kuchangia hii maada baada ya kumaliza mafunzo ya semina iliyofanyia Kawe mapema leo hii🤣🤸🐒
 
Wewe baba ina maana mambo ya familia unayaleta huku?

Anyway, mimi na mdgo wangu Swalehe tushasema atuchanjwi.

Chanjwa wewe na mama inatosha.
#NasimamaNaGwajima
Na pia kwanini wanatumia nguvu kubwa sana kwenye hili la corona je unafanya hivi kwa faida ya nani?
 
Moderator uzi wa jukwaa la change mnauleta huku jamani

Jamii forum mna shida gani aisee
Sasa tatizo ni lipi kwenye huu ugonjwa ni udhaifu wa kinga ndio unakukufanya kuwa kwenye hatari ya huu ugonjwa mfano wazee ambao kinga zao ni dhaifu au tatizo ni aina ya mashambulizi ya hivyo virusi vyenyewe? maana tunaambiwa wengine wanaweza kupata maambukizi(hasa vijana) ila wakaumwa tu kawaida bila kuhitaji kulazwa na wakapona na wengine wakawa na maambukizi ila wasioneshe hata dalili na wakawa wanaambukiza wengine.
 
Back
Top Bottom